Ajali MV Nyerere: Waziri Mkuu amsimamisha kazi Mtendaji Mkuu wa TEMESA kupisha uchunguzi. Aunda Tume ya uchunguzi

Kwa utawal huu tume itakuwa imeishaandaliwa majibu ya kutoa kwa walioiteua
 
Mbunge huyu alistahiri kuwa ni sehemu ya tume hiyo kwa sababu ni mtu anayefahamu matatizo ya kivuko kwa miaka yote. Je, watamkubali?
 
Wengi tumepokea kwa furaha agizo la kujenga kivuko kipya kitakachowahudumia wakazi wa Ukerewe na visiwa vya jirani.
Ila mimi ninonelea vyema hiyo pesa itumike kujenga vivuko viwili vya tani 25-30.
Hii itasaidia wakati wa low season kuweza kujaza kivuko kimoja.
Pia wakati hiki kinaenda hiki kingine kitakuwa kinarudi.Hii itarahisisha na kuharakisha huduma ya usafiri...
Kujenga kivuko kimoja kikubwa kunaweza kusababisha kikaendeshwa kwa hasara wakati ambapo mahitaji ya usafiri ni madogo (low season).
Otherwise pongezi nyingi zimfikie mheshimiwa kwa jinsi alivyolishughulikia suala hili...
 
Kwa nini watendaji wa wizara hawajapisha uchunguzi?
Je vip wale waliotakiwa kuokoa je walirespond kwa muda mwafaka?
Inashangaza PM awapa pongezi watu kibao hasa vyombo vya ulinzi na usalama ......... ila kwenye picha zote nimeona ni wananchi wa kawaida tu wakiwajibika ........ Hii sijui imekaaje!!
 
Haya ndo tunalalamikia. Naangalia utendaji kazi za kila siku kwa majeshi yetu. Hivi kweli mstaafu wa jeshi alipewa kuwa M/kiti wa bodi ya ushauri wa TEMESA! Ana uzoefu gani kazini, amewahi kufanya utafiti gani, ni wapi amewahi kujieleza kitaalamu na baadaye kustaafu ni wapi utaalamu wake unahitajika kiasi hicho?

Tunaliangusha taifa wenyewe kwa kuamini kuna watu fulani lazima wapewe kazi ya kufanya bila kujali gharama kwa taifa na sasa maisha ya watu.
 
Hizi zote ni propaganda za kisiasa......serikali huwezi wewe ndo mmliki wa kivuko tena wewe ndo msimamizi na regulator wa usafiri huo huo, hu nimgogano wa maslahi....la kufanya ni kwamba serikali itoke kwenye hiyo biashara hasa kuendeshe yenyewe iachie ma compuni binafusi, yenyewe ibaki kusimamia ku regulate kuadhibu na kushauri muendeshaji..lkn hapo tuna jidaganya huwezi kua "hakimu katika shauri lako" watu wataendelea kufa nakuendelea kutulaghai na tume za uchanguzi.
 
Apewe Mbowe akiendeshe.
 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi Mtendaji Mkuu wa Temesa, Mussa Mgwatu kupisha uchunguzi.View attachment 876120
Huyu sio Dr. Mgwatu...very sad he has gone down with the catastrophe.

Ukiangalia sana, hizi shake up ni muhimu kweli. Kwasababu ya kufanya kazi kwa mazoea na kukosa ubunifu na uadilifu. Vitengo nyeti kama Temesa vina maslahi mapana kwa Taifa. Watu wengi wananenepa kwa kula bila kufanyia kazi.

Yes, sasa tujenge utamaduni wa uwajibikaji ili kuondoa matatizo haya yanayojirudia sababu za uzembe na kukosa uwajibikaji
 

Unajuaje labda alikuwa NAVY, Usilalame tu
 
Ameagiza kutangazwa zabuni ya kutengeneza kivuko kipya cha Ukara-Bulogora kitakachobeba abiria zaidi ya 200 na uzito tani 50

Watu 200 na uzito tani 50

Kwa hiyo watu hawahesabiki katika uzito.

Li nchi la watu waliosoma shule za kata, tutaendelea kufa kwa kushindwa hesabu za ku calculate uzito.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…