Ajali mbaya yaua 11 Mbeya

Ajali mbaya yaua 11 Mbeya

Ruhinda

Member
Joined
Aug 29, 2011
Posts
23
Reaction score
8
Kwa mjibu wa habari ambazo nimezipata,

Inadaiwa watu zaidi ya 11 wamefariki dunia katika ajali ya gari la abiria aina ya Caoster inayofanya safari zake Mbeya Tukuyu hadi Kyela baada ya kugongana uso kwa uso na lori la mizigo lililokuwa likitokea nchini Malawi baada ya kudaiwa kufeli breki na kulivaa basi hilo mudasiyo mrefu.

Taarifa kutoka kwa baadhi ya mashuhuda wamesema hali ni mbaya kutokana na kudaiwa kuna majeruhi wengi ambao wameumia vibaya na hali zao ni mbaya na kwamba kuna uwezekano wakupatikana vifo zaidi.

Majeruhi wanaendelea kukimbizwa katika Hospitali ya rufaa mkoani Mbeya, taarifa zaidi baadaye
cleardot.gif
 
Jamani jamani Watanzania wenzetu poleni sana kwa maumivu mulionayo na kwa wale waliopoteza maisha Mungu azilaze roho za marehemu wote mahala pema peponi amen.
 
Coaster, gari la abiria limegongana uso kwa uso na Lori la Fm Abri wa Iringa eneo la Igawawilo uyole na kuua abiria 12 papo hapo. Source mimi mwenye nilikuwa kwenye tukio.
 
Pole sana kwa wahanga wote wa ajali. Ombi langu kwako, ni vizuri hii habari ingekuwa hoja mchanganyiko maana mambo ya ajali si siasa.
The unseen is illustrated by the seen.
 
Coaster, gari la abiria limegongana uso kwa uso na Lori la Fm Abri wa Iringa eneo la Igawawilo uyole na kuua abiria 12 papo hapo. Source mimi mwenye nilikuwa kwenye tukio.

May the almighty father rest the souls of the departed in eternal glory; Amen
 
Tunasikia juujuu kuwa kunaajali mbaya imetokea maeneo ya igawilo mbona hamtujuzi?
 
Kweli kuna ajali imetokea maeneo ya igawilo barabara ya kwenda kyela. Lori limefeli break na kwenda kuligonga gari ya abiria aina ya coaster,watu 8 wamekufa hapohapo na wengine kujeruhiwa vibaya.
 
Mungu azipumzishe roho za marehemu,tatizo hatupendi kupeleka gari service ndo maana kila siku ajali haziishi,ajali zingine zinaepukika jamani.
 
Back
Top Bottom