Ajali mbaya ya meli!!!!!

CHAI CHUNGU

JF-Expert Member
Feb 20, 2012
7,113
930
Leo ni miaka 16 imetimia sasa tangu kutokea ajali mbaya ya meli ya MV BUKOBA,ajali hiyo ilimpoteza kaka angu kipenzi aliyekua ndio kwanza ameanza ajira ktk jeshi la jwtz,iliniuma bcoz ndio aliyekua mfadhili wangu wa masomo ya secondary na maisha ya kila siku,hiyo ilipelekea kukatisha masomo yangu bila kupenda ili niitunze family.
Nakuuliza wewe mwana jf mwenzangu hii ajali ilikuathili vipi?ingawa inauma kuikumbuka siku hii!!
 
Mimi iliniathiri sana tena sana coz iiliwazamisha watanzania wenzangu nguvu kazi ya taifa zaidi ya 1200 wakati huo ndo tuu mkapa kaingia madarakani. Mkapa alikuwa na nuksi zake enzi za utawala wake tulipoteza na kupata hasara kadhaa. 1, kuzama kwa meli ya mv bukoba. 2, ajali mbaya ya treni, dodoma,3, kifo cha baba wataifa Julius nyerere. 4 kifo cha dr omary ali juma makamu wa rais. 5, kifo cha jenerali kombe.6, Kuuziwa rada feki kwa bei ghali. .7, kuuziwa ndege ya rais kwa kulifilisi taifa. 8,kifo cha timu ya ushirika moshi. 9, kifo cha timu ya pamba mwanza. 10, kifo cha timu ya majimaji songea. Jamani wekeni muendelezo wa matukio mabaya unayoyakumbuka yaliyotokea enzi za utawala wa mkapa.
 
JK kuingia ikulu!
 
Ajali ya MV Bukoba poleni lakini utawala wa Ben Mkapa kiboko hayo yote 10 ya kijichake nayakubali na aliuza NBC kasoro Magereza
 
Leo ni miaka 16 imetimia sasa tangu kutokea ajari mbaya ya meli ya MV BUKOBA,ajari hiyo ilimpoteza kaka angu kipenzi aliyekua ndio kwanza ameanza ajira ktk jeshi la jwtz,iliniuma bcoz ndio aliyekua mfadhili wangu wa masomo ya secondary na maisha ya kila siku,hiyo ilipelekea kukatisha masomo yangu bila kupenda ili niitunze family.
Nakuuliza wewe mwana jf mwenzangu hii ajari ilikuathili vipi?ingawa inauma kuikumbuka siku hii!!
Spika,
Pole sana na yaliyokusibu.

Cha kusikitisha zaidi ni kutokuwepo kwa utaratibu wa kuwa na makumbusho ya majanga makubwa kama hili ili kuwakumbuka waliotutoka na pia kutukumbusha tuliopo kuwa tusirudie tena makosa yaliyosababisha hilo janga i.e. 'never again'. Kukosekana kwa huu utaratibu nafikiri ndio maana kila leo kunakuwa na ajali na wala hatuonyeshi kujifunza na yaliyopita.
 
MOD badilisha title isomeke kumbukumbu ya ajari mbaya ya MV Bukoba.
 
Mi kinachonigusa ni kutokuwepo kumbukumbu ya haya majanga makubwa Kitaifa.
Mbaya zaidi ajali ile iliwameza sana Nguvu ya Taifa letu!

Tuwakumbuke wahanga wetu,Na MUNGU awalaze mahala pema peponi!

Ameen!!
 
Dah, watz kwa kusahau bana! yaani juzi tu sidhani kama kuna hata chombo cha habari kilichoandika tukio hili...
Ilikuwa ni Huzuni sana nakumbuka nilikuwa kidato cha tano ndo naingia form six huko huko kanda ya ziwa and almost karibu kila nyumba aroud the school and town kulikuwa na vilio...

RIP wote waliofariki kwenye ajali hii.
 
Poleni sana wote na hata mimi kwa msiba mkubwa uliotufika. Nilisononeka sana pale tulipotangaziwa kuwa zoezi la uokoaji "LIMESITISHWA"! Nchi za wenzetu wangeendelea kutafuta mabaki hadi leo!
 
Tatizo la nchi yetu hatujifunzi kutokana na makosa tunayoyafanya; tengejifunza ya MV BUKOBA ya ajali ya meli Ya SPICE ISLAND pengine yangeepukika kule Nungwi!!!
 
Mimi iliniathiri sana tena sana coz iiliwazamisha watanzania wenzangu nguvu kazi ya taifa zaidi ya 1200 wakati huo ndo tuu mkapa kaingia madarakani. Mkapa alikuwa na nuksi zake enzi za utawala wake tulipoteza na kupata hasara kadhaa. 1, kuzama kwa meli ya mv bukoba. 2, ajali mbaya ya treni, dodoma,3, kifo cha baba wataifa Julius nyerere. 4 kifo cha dr omary ali juma makamu wa rais. 5, kifo cha jenerali kombe.6, Kuuziwa rada feki kwa bei ghali. .7, kuuziwa ndege ya rais kwa kulifilisi taifa. 8,kifo cha timu ya ushirika moshi. 9, kifo cha timu ya pamba mwanza. 10, kifo cha timu ya majimaji songea. Jamani wekeni muendelezo wa matukio mabaya unayoyakumbuka yaliyotokea enzi za utawala wa mkapa.

UMESAHAU AJALi YA NO CHALENGE KUTUMBUKIA MTONI TANGA NA KUBADILISHWA JINA KUWA AIR SHENGENA
 
Back
Top Bottom