Ajali mbaya ya BASI, LORI, NOAH, HIACE na PIKIPIKI.

Ajali mbaya ya BASI, LORI, NOAH, HIACE na PIKIPIKI.

poleni sana ndg zetu. Mungu atakuwa pamoja manyi kipindi hiki kigumu.
 
Mkuu hivi ubabe huu hadi kwenye hatari ya kifo?

sidhani kama ni ubabe. nafikiri suala zima linasababishwa na uzembe kwetu sote watanzania. ukianza na jeshi la polisi wanaosimamia sheria za barabarani,wanaufaham uvunjifu wa sheria unaofanywa na madereva wazembe lakn wamesahindwa kuudhibiti. raia ama abiria hushuhudia uzembe unaoweza kufanywa na dereva lakn akijitokeza walau abiria mmoja kumuonya dereva abiria wengine hukaa kimya bila kumuunga mkono na usishangae pia ukiona abiria mwingine akimpinga aliyemuonya dereva. madereva nao wakati mwingine hawafuati vizuri alama za barabarani,wakati mwingine alama za hizo ama hazikuwekwa au pengine zilitoka na akiyepashwa kuzirudishia naye kajisahau au kaacha tu bila sababu ya msingi, almradi tu mambo yanakwenda ndivyo sivyo. jamami tubadilike. tanzania ya leo yenye baadhi ya maeneo kuwa na shule za sekondari karibu kila kijiji doesn't reflect welfare i guess would have been an outcome of educated individuals? hii mimi inanichanganya.
 
Nchi dhaifu, rais dhaifu, wizara dhaifu, waziri dhaifu, dreva dhaifu, konda dhaifu, abiria dhaifu,ajari si dhaifu, vifo si dhaifu.
NB: UDHAIFU HUO NI WA KUFIKIRI
 
Poleni ndugu wa marehemu na ndugu wa NYUMBU a.k.a wahifadhi
 
Poleni sana wahanga wote. Kwa nchi hii watu hawazingatii swala la usalama si kwa madereva hata abiria wenyewe unakuta pikipiki imebeba watu 3-4 unatengemea nini hapo? mwendo kasi bila kuzingatia alama za barabarani na watu wanashangilia Zakaria leo limeingia stand la kwanza dere/suka yule mkali......MAJANGA!
 
Ajali iliyotokea jana na leo hapa Bunda ni katika maeneo yafuatayo. Bulamba hiace na pikipiki jana wanne wamefariki, Lori na nyumbu eneo la Serengeti jana wanne wamefariki na majeruhi 40, Noah na pikipiki eneo la Balili jana afariki mmoja ambaye ni mtendaji, Hiace na pikipiki eneo la daraja mbili karibu na Vilian Ukerewe road leo afariki mmoja, Zakaria express eneo la Serengeti ikitokea Tarime kwenda Mwanza nayo yaua ila uhakika wa waliofariki haijajulikana. Yote haya yametokea wilaya ya Bunda. Hospitali ya BDDH imejaa majeruhi wa ajali hizo.

Wasira keshafika kuwajulia hali?
 
Back
Top Bottom