Ajali mbaya imetokea leo majira ya saa 1: 30 jioni eneo la Endasak wilaya ya Hanang' ikihusisha gari aina ya fuso na power tiler ambapo watu saba kati ya kumi na nne waliokuwepo kwenye power tiler wamepoteza maisha. Chanzo cha habari ni mimi mwenyewe nilikuwepo eneo la tukio.
-----------
Hanang’. Watu saba wamefariki dunia na wengine saba kujeruhiwa kwenye ajali iliyotokea katika Kijiji cha Getasam, Kata ya Endagaw wilayani Hanang’ Mkoa wa Manyara.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Manyara, Christopher Fuime alisema kuwa ajali hiyo iliyohusisha lori la mizigo aina ya Fuso na Power Tiller ilitokea usiku wa kuamkia jana katika Barabara Kuu ya Babati-Singida.
Alisema lori hilo lililokuwa limewabeba wakulima 14 waliotoka kuvuna maharagwe, lilikuwa likitokea Katesh wilayani Hanang.’
Kamanda Fuime aliwataja waliofariki dunia kuwa ni Lazaro Daniel (30), Augustino Marcel (20) Stephano Dahaye (18), Elias Leons (18) na Michael Faustin (25) .
Wengine ambao walifamika kwa jina moja ni Uttu na Innocent (20) wote wakazi wa Kijiji cha Maraa.
Aliwataja majeruhi kuwa ni Isaya Joseph (25), Hemed Darabe (25) Inocenta Ploti (18) Paul Anjelus (16) na Amani Rajab (19).
Wengine ni Daniel Yamee (17) na Godfrey Samweli (17) .
“Chanzo cha ajali hiyo ni mwendo wa kasi wa lori na watu sita walifariki papo hapo, huku mwingine akifariki mara baada ya kufikishwa katika Hospitali ya Dareda Babati,” alisema Kamanda Fuime.
Alisema dereva wa lori alikimbia baada ya ajali hiyo.
Diwani wa Endasak, Daines Peter (Viti Maalum) alisema mtoto wa mmiliki wa lori hilo lililosababisha vifo amenusurika kuuawa na wananchi.
Alisema mtoto huyo alisikika akilisikitikia gari hilo badala ya waliofariki dunia.
“Wananchi wa eneo hilo walichukizwa na kitendo cha mtoto huyo kujali gari lao bila kutanguliza utu ila tunashukuru jamii haikumletea madhara baada ya kutulizwa na wazee,” alisema Peter.
Chanzo: Mwananchi