Ajali Mbaya TAZARA Bakhresa

Ajali Mbaya TAZARA Bakhresa

inasikitisha sana, huyo konda kafanya ukatili, huwezi msukuma mtu gari likiwa linatembea, pole kwa waliopoteza ndugu yao.
 
Duh,Konda anabahati sana,ingekuwa mitaa mingine lazima wangemmaliza.
Hii tabia wanayo sana,kuna siku alimsukuma jamaa mmoja basi alimkamata shati wakaenda wote chini,alichezea ngumi za haraka haraka akawa mpole.
 
Mimi nazani kama kuna abiria alikuwepo kwwnye hiyo daladala na anasoma Uzi huu na aliona hilo tukio muwakamate haraka sana hao wahusika kondakta na dereva wapelekwe polisi. Pia hata hilo Lori naamini kwa foleni ya Mandela road hata Ubungo halijafika kama kuna washuhuda wanalikumbuka Lori walifukuzie na bodaboda watalikamata.

Hapo kwenye red ndo huwa nachoka kabisa na kupoteza hamu ya kushi Dar! Watu tumekosa ubinadam kabisa, tukio linaweza kufanyika hapa na watu wanaangalia tu wala hawatoi msaada! Inakuwaje mtu amekanyaga mtu halafu anakimbia tu bila kusimama au watu kumzuia asiondoke? Inakuwaje konda anasukuma mtoto bila watu wengine kutoa msaada?

Dar jifunzeni ubinadam aisee!! Matukio mengi tu hapo Dar yanatokea akina mama wanakwapuliwa mikoba na vibaka huku watu wanaangalia tu bila kutoa msaada wowote!!
 
pale pananikera wale wavukaji wasivyoogopa magari...
 
kampumzike kwa amani huko mbinguni,nchi yetu haijali sana sheria za usalama barabarani na sehemu nyingine,raiti zingekuwa zinazingatiwa hakika wahusika wangefikishwa mbele ya pilato mapemaaa ,poleni sana wafiwa
 
Habari wapendwa katika Bwana

Kuna ajali imetokea Tazara karibia na mataa ya Tazara Bakhresa kuna binti amegongwa na Lori la mizigo. Kichwa chote kimesagika kwakuwa tairi zimepita kichwani hivyo kichwa kimetoka kabisa hivyo hajulikani. Polisi wamezuia kuchukua picha lakini alikuwa amevaa simpo nyeusi. Nguo hazitambuliki. Anaonekana kwa kukisia ni kama binti wa miaka 12-17 hivi.

Chanzo cha ajali alikuwa anajaribu kupanda daladala iliojaa kupita kiasi konda akamshusha kwalengo lakunguza abiria bahati mbaya akadondoka ndipo Lori likamkanyaga.

RIP sana dada yetu mpendwa.
 
Hapo kwenye red ndo huwa nachoka kabisa na kupoteza hamu ya kushi Dar! Watu tumekosa ubinadam kabisa, tukio linaweza kufanyika hapa na watu wanaangalia tu wala hawatoi msaada! Inakuwaje mtu amekanyaga mtu halafu anakimbia tu bila kusimama au watu kumzuia asiondoke? Inakuwaje konda anasukuma mtoto bila watu wengine kutoa msaada?

Dar jifunzeni ubinadam aisee!! Matukio mengi tu hapo Dar yanatokea akina mama wanakwapuliwa mikoba na vibaka huku watu wanaangalia tu bila kutoa msaada wowote!!

Sawa kabisa Mkuu. Kwa wale wanaofahamu maeneo yale pana wauza mitumba wengi miaka nenda rudi. Chakushangaza nolipouwaliza kulikoni wakanionesha mwili wa marehemu ukiwa umefunikwa kanga katikati ya barabara (kwenye tuta la katikati linalotenganisha barabara mbili) wanajibu kirahisi utazani aliekufa ni paka tu, watu hawaoneshi kusikitika, traffic anajitahidi kuzuia magari ilo kuepusha ajali nyingine kwakuwa watu walikuwa wanakimbia ovyo barabarani kwenda kuona kuutambua mwili wa marehemu. Sasa kwa hali ile wanachukulia kama vile Dada marehemu hakuwa makini wengi wanalaumu yaani vurugu tupu.
 
Mwanga wa milele...umuangazie...mwanga wa milele umwangazeee
 
Yaani ilitakiwa muda huu huyo konda awe mochwari na gari limeteketea kwa kuchomwa na watu wenye hasira kali
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom