Ajali mbaya kwa mbonde kibaha

Ajali mbaya kwa mbonde kibaha

mtangazaji wa habari hii radio one alisema 'mabasi mawili ya abiria yaliweza kugongana uso kwa uso' huwa nakereka sana na watangazaji wa aina hii, kuweza kugongana maana yake nini!!!!

kauli zingine za watangazaji wa redio ambazo hunikera ni kama na ifuatavyo:

hali ya sintofahamu
mimi kama mimi
lisaa limoja nk.
samahanikwa kutoka nje ya mada na poleni wahanga wote.
Ongezea na hizi 'sio kihivo', 'si kivile'
 
Imenishtua sana kwa kuwa mkate wangu nautafutaga maeneo hayo. MUNGU awarehemu marehemu tena awatie nguvu na imani wafiwa.
MUNGU tusaidie suala hili linatushinda
 
Pole zao sana waliopatwa na msiba huo na majeruhi pia. TZ ajali imekuwani kama kawaida kutokea kila siku, Ni vile sijui hatujifunzi kila ajali zinapotokea au ni vipi!!. Imefika wakati sasa yani mtu unasubiri zamu yako tu, hujui lini na wakati gani. kwanini mtu usishangae kwani imewatokea hao, kwanini isiwe wewe!!. Lakini mi nadhani haya yote yanachangiwa sana na ugumu wa masiha ambao tunao.

Mungu tuepushe na hili janga la Taifa
 
Mungu azilaze Roho za Marehemu mahali pema peponi.
Hivi Tanzania watu watazidi kufa barabarani mpaka lini. Hivi tunachukua takwimu kuzichambua na kuangalia kama kuna kitu tunaweza kufanya kurekebisha hali hii. Tukiangalia week hii tu ni watu wangapi wamekufa barabarani. Hivi Tanzania tunajua msamihati wa Health and Safety First? Leseni za kupewa na Wajomba wakiongozwa na Mwema zinatufikisha pabaya. Kwa wenzetu kupata leseni ya kuendesha gari unaifanyia kazi kweli kweli, kwetu unapata leseni hata kama hujawahi kushika usukani wa gari. Matokeo yake ni haya kila siku kuna mtu anakufa barabarani. Does the government care? No.
 
Back
Top Bottom