Pole nyingi kwa ndugu na jamaa wote wa marehemu, kwa vyovyote vile hawa ni ndugu zetu waliokuwa wana wahi shughuli za ujenzi wa taifa letu changa. Kwa bahati mbaya wakati wenza wao kikazi wakiwasubiri janga hili linawatokea.
Mungu wasamehe dhambi zao kwa kifo hiki cha ghafla, japo imeandikwa hatujui siku wala saa.
Ni majonzi ya kutisha kabisa. Yaani mtu unaogopa hata kuendesha gari yako, unajitahidi kuchukua tahadhari zote ila dereva mzembe anakuchukulia maisha yako. So sad. Picha zimenipa hofu kubwa sana. Naomba nisizikumbuke wakati nikiwa njiani naendesha kwani ukiona lori au daladal unaweza kupaki pembeni kabisa. Kwa hakika nikiwa naendesha nakuwa makini sana na malori, daladala na siku hizi pikipiki (ikiwemo vya miguu mitatu a.k.a vichenge).