AJALI: Gari imezama Kigamboni wakati wa kuvuka katika Pantoni

projectman

JF-Expert Member
Sep 8, 2015
349
486
Watu wawili wamepoteza maisha baada ya gari walilokuwemo kuserereka wakati likiingia katika kivuko na kutumbukia baharini eneo la Kivukoni, Dar es Salaam leo. Gari hiyo aina ya Toyota Hiace ikiwa na 2. Mwili wa dereva wapatikana, na kikosi cha jeshi la zimamoto watafuta wa pili⁠⁠⁠⁠.

===================

KIGGG.jpg


Habari zaidi zinasema wavukaji hao walikuwa ni waombolezaji na wametoka Mkoani Morogoro kwenda msibani eneo la KIGAMBONI na walikuwa hapo tokea saa 9 za usiku na walikuwa wengi kwa idadi ianyokadiriwa kuwa ni 15 na nia yao ikiwa ni kusubiri PANTONI ya alfajiri wawahi kuvuka nayo na walipokuwa hapo (FERRY).

Walishuka katika gari waliyokuja nayo kisha Watu wawili Dereva na Mwanamke mmoja wakakodi gari nyingine aina ya Toyota Hiace ili wakishavuka tu iwasaidie kuwapeleka wote huko Msibani kisha wao ( Dereva na huyo Mwanamke ) wakaingia katika hilo gari aina ya Toyota Hiace huku wale Ndugu wengine wakikaa katika PANTONI.

Safari ilipoanza tu hiyo Saa 10 alfajiri ya kuvuka ndipo GHAFLA ile Hiace ikarudi nyuma na KUZAMA majini wakati huo PANTONI tayari imeshafika katikati ya maji. Baada ya kuona hivyo yule Dereva akafungua mlango haraka na kuruka kutoka katika Gari na kuzama Baharini huku mwanamke aliyekuwepo ndani ya gari akashindwa kufanya lolote na akazama na ile GARI.

Taarifa ziliwafikia WAOKOAJI wa ZIMAMOTO Saa 11 alfajiri ndipo wao wakawahi kufika eneo la tukio kuanza uokoaji huku wakiomba tena MSAADA wa Jeshi la Maji ( Navy ) ambapo walianza kazi ya uokoaji tokea hiyo saa 11 na ilipofika saa 3 asubuhi hii ndiyo wakauona mwili wa yule Dereva ukielea na wakautoa lakini mpaka sasa WAOKOAJI hao wanaendelea kuusaka mwili wa yule Mama

Lakini mpaka sasa hawajafanikiwa na inasemekana kuwa huenda yule mwanamke amezama na lile gari ( Hiace ) na sasa wanafanya utaratibu wa kulitafuta hilo gari chini ya maji ili tu wautoe mwili wa yule Mama ila kipingamizi kikubwa ni hali ya mawimbi kwa sasa, mkondo wa maji yale lakini kubwa zaidi kina kirefu kilichopo pale ambapo ni takribani minazi 7 mpaka 9 ukiipanga kwa kuinyoosha.

Screenshot from 2016-04-20 18:16:43.png

Hatimaye zoezi la kuokoa miili miwili pamoja na gari lililotumbukia kwenye maji Leo alfajiri limekamilika.
 
Haya, tunasubiri taarifa zaidi. Naomba Mungu awasaidie kutoka salama
 
bado hawaon mara vying magar ni kujiachia kwa uzembe wa dereva kutokuweka handbreak na kuminya break wakuta panthon yaondoka gar linarud nyuma na kuza
 
habari mbaya sana...katika sheria za safety ni kosa kuwa katika chombo chochote ukiwa katika pantoni labda gari iwe imebeba hela walinzi ndio wanatakiwa waruhusiwe na wao pia wawe wanepita kozi ya kuzama katika kina kirefu sema Bongo hatufuati sheria za kimataifa za usafirishaji tunafanya tunavyojua kila siku majanga mengine yanaweza kuepukika..
 
Kwanini watu wanakuwa kwenye gari wakati gari ikiwa kwenye pantoni?
 
Nimesikia walikuwa watu 7 katika gari,kumbe dereva hakuweka break.
Akapitiwa na usingizi,gari ikaanza kurudi kinyumenyume,wale watano wakamuamsha dereva lakini alikuwa katika usingizi mzito.

Ikabidi wale watano washuke kwenye gari akabaki mgonjwa na dereva na ndio waliozama na gari.

Lakini nimejiuliza kwanini wale watano badala ya kuweka break au hata kuzima gari wakabaki kumuamsha dereva?

Kama ni kweli basi wale watano nao ni wa kulaumiwa.
 
roho imeumia sana hao tayari rip ... ila watz ni wabishi huwa kuna kuambiwa mshuke abaki dereva ila wakaidi wanabaki wote
 
Back
Top Bottom