Ajali Basi la mohamed Trans lapinduka

Zuia Sayayi

JF-Expert Member
Mar 28, 2011
841
133
Basi La MTL lilikuwa likitoka Mwanza kwenda Dar Limepinduka
kuna majeruhi na hakuna taarifa za vifo
source R.f.a
 
poleni sana wahanga. usishangae kuwa chanzo ni mwendo kasi sasa jiulize kipindi cha UBU kinawasaidia watu??????????????
 
Limepinduka leo asubuhi na chanzo wanasema ni mwendo kasi uliopitiliza kiasi kwamba ikitoke likagongana na basi jingine (uso kwa uso) mabasi hayo yatavaana na kuwa basi moja.!
 
Ajali zimeshakuwa janga la taifa kwa sasa... Mpaka 2015 asilimia 50% ya wasafiri Tanzania watakuwa either vilema. Au wemapatwa na mauti

Na hakuna kiongozi anayeongelea swala la ajali barabarani... Viongozi wote wako bize kula vya mwisho mwisho, mpaka ukoko.

Swala la ajali wamemuachia Mungu.
Utawasikia eti "Tumshukuru Mungu, kwa ajali, na watu kufa".haha

Sasa sijui wana_maanishaga Mungu au shetaniii..... Maana hamna Mungu anayependa tuwe vilema, au watu wafe....

Ni hayo tu...
 
Pole kwa majeruhi!

Hizi pole hazisaidii jamani. Kila siku poleee...

Tutafute chanzo cha hizi ajali. Ajali kwa kiasi kikubwa zinaepukika, na wala sio swala la bahati mbaya..

Kila siku watu wanakufa, wengine wanapatwa na vilema.. Afu mnasema "POLE"
 
Kweli ligongane na gari lingine bila kuua, hio sijaielewa bado, na imetokea wapi?
 
Haya mabasi ya Mohamed trans yana nuksi naona wameanza kutoa kafara ya mwaka huu, maana mwaka jana ilikuwa kimbembe, mara limeungua mara limepasuka tairi na kupinduka mara limegongana na roli mmmmh watu waache kupanda haya mabasi ya Mohamed trans kwa kweli
 
Hizi pole hazisaidii jamani. Kila siku poleee...

Tutafute chanzo cha hizi ajali. Ajali kwa kiasi kikubwa zinaepukika, na wala sio swala la bahati mbaya..

Kila siku watu wanakufa, wengine wanapatwa na vilema.. Afu mnasema "POLE"

Chanzo ni mwendokasi. Haya, majeruhi bado hawastahili kupewa Pole?
 
Hawa madereva wanatumaliza ..

Sio madereva tu. Hata magari yenyewe ni mabovu... Magari mengi siku hizi ni mchina.. Mbali na hapo hamna regulatory authority yoyote Tanzania kuhusu ubora wa magari (hasa yanayosafirisha abiria)..

Kuna mtu alipost hapa JF, mwanafunzi mmoja ali_kanyagwa na tairi. Baada ya kiti alichokuwa amekalia kwenye school basi kutumbukia (nchi zingine hii ni skendo kubwa, ingepelekea afisa usalama barabarani kujiuuzuru)....

Hii inaonyesha jinsi magari yetu yalivyo mabovu. Na hakuna mtu wa kusimamia sheria za usafirishaji. Wamiliki wa mabasi wanafanya wanavyotaka.

Mimi naomba waTanzania tupiganie sheria inayom_bana mmiliki wa mabasi kulipa fidia kubwa, kwa abiria pindi anapopata ajali (kama ilivyo ULAYA na kwingineko). Hii itasaidia wamiliki kuwa makini na mabasi yao...

Tukisubiri serikali, isamamie na kutunga sheria za usalama barabarani, kwa ajili ya maisha yetu. Hatutaweza,...
 
Haya mabasi ya Mohamed trans yana nuksi naona wameanza kutoa kafara ya mwaka huu, maana mwaka jana ilikuwa kimbembe, mara limeungua mara limepasuka tairi na kupinduka mara limegongana na roli mmmmh watu waache kupanda haya mabasi ya Mohamed trans kwa kweli

na hayafungiwi
 
Chanzo ni mwendokasi. Haya, majeruhi bado hawastahili kupewa Pole?

Why do you confirm kuwa ni mwendo kasi??? Umeenda kupima kwenye tukio.
Marekani magari yanakimbia kuliko bongo mbona hawapati ajali za kila siku kama bongo.

Naomba download "seconds from disater" uone ajali zinavyotokea, na jinsi viongozi walio_serious na maisha ya raia wao Wanavyowajibika.

Asilimia kubwa ya ajali ni uzembe.
 
Hii ni Ligi sasa.
 
Limepinduka leo asubuhi na chanzo wanasema ni mwendo kasi uliopitiliza kiasi kwamba ikitoke likagongana na basi jingine (uso kwa uso) mabasi hayo yatavaana na kuwa basi moja.!

maskini nilijua kuwa hilo ndio tatizo sasa unajiuliza hivi alikuwa anakimbilia wapi? sasaameishia bugando badala ya kufika dar.
 
Hii sijui itakua mpaka lini, viongozi wetu sijui wana fanya nini au tuamini usemi ulioenea mtaa kua viongozi wetu wanapenda zaid kutuma salamu za rambirambi kuliko kuokoa maisha.
 
Back
Top Bottom