Uncle Jei Jei
JF-Expert Member
- Jan 7, 2011
- 1,683
- 2,157
Kumetokea ajali ya basi la majinja lililokuwa linatoka Mbeya kwenda Dar. Sababu ya ajali ni mwendo kasi wa basi la majinja ambalo lilitaka kulipita gari lingine ambapo walikutana na lori upande wa pili na kumlazimisha dereva kulipeleka gari porini kuepusha kugongana uso kwa uso na hivyo, basi kupinduka vibaya sana. Hakuna vifo mpaka sasa ila majeruhi zaidi ya 28 wamepelekwa hospitali ya Morogoro. Majeruhi zaid wanaendelea kupokelewa. Dereva wa basi amekimbia. Ajali imetokea morogoro mjini eneo la nane nane.
Chanzo. Radio one stereo breaking news.
Ajali imetokea maeneo ya FRANSALIAN barabara kuu ya dsm, ajali imetokea baada ya basi hilo kugongana na lori lililokuwa likitokea dsm. Kwa mujibu wa majeruhi wa ajali hiyo, ajali imetokea pale dereva wa basi alipotaka kulipita gari la mbele huku akiwa mwendo kasi. Kwa mujibu wa majeruhi na mashuhuda wengine hakuna aliyepoteza maisha na dereva wa basi hilo amekimbia.