Ajali: Basi la Happy Nation, Abood bus na Lori, yapata ajali Milima Kitonga,

Satuuuu

JF-Expert Member
Dec 3, 2015
1,849
1,993
16939398_1143754535733361_8069999251089772412_n.jpg

Wakuu kuna habari nimepewa na mmoja wa wasafiri yakuwa Leo majira ya saa tano kuna ajali imetokea eneo la mlima Kitonga ambapo bus la Aboud,Hpy Nation na fuso yasemekana yameporomokea shimoni,sasa mliopo ktk eneo la tukio tafadhali naomba mtujuze zaidi.
17022000_1143800852395396_7055574325318216194_n.jpg
17155177_1143800922395389_1494184959410715532_n.jpg
16939503_1143800905728724_8173141113391633377_n.jpg
17155883_1143800845728730_3847666219554855169_n.jpg
17098415_1143800849062063_3665194859517256645_n.jpg

Ajali mlima kitonga mchana huu kati ya basi la Happy Nation, Abood bus na roli. Ajali imesababishwa na bus la abood baada ya break zake kugoma likiwa linashuka mlimani..
17155764_10211130434710095_1496899062248581028_n.jpg

AJALI KITONGA: Watu 12 wajeruhiwa baada ya mabasi ya Happy Nation na Abood yakitoka Iringa kwenda Dar kugongana na lori huko Kitonga Iringa, polisi yathibitisha.
 
Hmmm! Mungu awanusuru wasafiri. Pale mahali panatisha sana.
 
Tetesi ni za kweli, ila sina taarifa kamili, nitawajuza kadri nitakavyopata taarifa
7a02329b6843b95d70d8176b93990ef8.jpg

=========
Hii ni baada ya abood kukosa brek na kuligonga fm ambalo halikuanguka,likaigonga fuso iliyokuwa imebeba ndizi na kutumbukia korongoni baadae likaigonga happy national na zote kutumbukia korongoni
==
 
Duuuuuuuu, tulia mkuu uje na repot kamili
Mkuu mie nipo mbali sana issue ni kweli na chakushangaza ni tokea majira hayo ya asbh so tusubirie tupate picha na uhakika kwa wadau
 
Wakuu kuna habari nimepewa na mmoja wa wasafiri yakuwa Leo majira ya saa tano kuna ajali imetokea eneo la mlima Kitonga ambapo bus la Aboud,Hpy Nation na fuso yasemekana yameporomokea shimoni,sasa mliopo ktk eneo la tukio tafadhali naomba mtujuze zaidi.

Mungu nusuru waja wako
 
Tetesi ni za kweli, ila sina taarifa kamili, nitawajuza kadri nitakavyopata taarifa
7a02329b6843b95d70d8176b93990ef8.jpg

=========
Hii ni baada ya abood kukosa brek na kuligonga fm ambalo halikuanguka,likaigonga fuso iliyokuwa imebeba ndizi na kutumbukia korongoni baadae likaigonga happy national na zote kutumbukia korongoni
==
Pole kwa wote waliopata ajali hizo.
 
Mpinga alisema kikosi cha usalama barabarani kitaweka utaratibu wa ukaguzi maalumu wa magari katika maeneo ambayo ajali zimekuwa zikitokea mara kwa mara ikiwa ni pamoja na katika mlima huo

..........................
 
View attachment 477072
Wakuu kuna habari nimepewa na mmoja wa wasafiri yakuwa Leo majira ya saa tano kuna ajali imetokea eneo la mlima Kitonga ambapo bus la Aboud,Hpy Nation na fuso yasemekana yameporomokea shimoni,sasa mliopo ktk eneo la tukio tafadhali naomba mtujuze zaidi.
View attachment 477052 View attachment 477053 View attachment 477054 View attachment 477055 View attachment 477056
Ajali mlima kitonga mchana huu kati ya basi la Happy Nation, Abood bus na roli. Ajali imesababishwa na bus la abood baada ya break zake kugoma likiwa linashuka mlimani..
View attachment 477068 View attachment 477067 View attachment 477066
View attachment 477071 View attachment 477070
WATU wanne wamekufa papo hapo na mmoja kujeruhiwa vibaya baada ya malori mawili kugongana na kutumbukia bondeni katika mteremko wa mlima kitonga wilayani Kilolo katika barabara kuu ya Iringa - Dar es Salaam.

Maroli hayo moja lenye shehena kubwa ya madini aina ya shaba na lingine lenye bidhaa mbalimbali za dukani yanalindwa vikali na askari Polisi wa wilaya hiyo, ili kunusuru mali hizo zisiibiwe.

Akizungumza katika eneo la ajali Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Taifa, Mohamed Mpinga alisema kwa masikitiko kwamba ajali nyingi zinazoendelea kutokea nchini zimekuwa zikisababishwa na uzembe wa madereva.

Tarifa kutoka kwa mashuhuda waliokuwepo katika eneo la tukio zimedai kwamba, ajali hiyo ilitokea usiku wa kuamkia jana na kuwa chanzo cha ajali hiyo ni lori lenye namba za usajili T587 BGP aina la Scania.

Mashaka Abdala alisema roli hilo lenye mali mbali mbali za dukani lilikuwa limeharibika na kuegeshwa kando ya barabara hiyo na liligongwa na lori lingine lenye namba za usajili T T319 BDG aina ya Scania pia ambalo breki zake zilikataa wakati likitelemka katika mlima huo.

Akithibitisha vifo vya watu waliokuwemo kwenye maroli hayo, Mpinga alisema taarifa za Polisi zimethibitisha watu wanne kati ya sita waliokuwemo katika maroli hayo kufa hapo huku mmoja akijeruhiwa vibaya na kukimbizwa katika hospitali ya mkoa wa Iringa.

Mbali na majina yao kutofahamika mara moja, mpaka tunakwenda mitamboni maiti moja ilikuwa bado haijatolewa kutoka kwenye kibini ya moja ya maroli hayo kilichopondwa na kufunikwa na kontena za maroli hayo, katika bonde la mlima huo.

Taarifa za kipolisi zimedai kwamba katika ajali hiyo kibini ya roli lilolokuwa limepakia shaba lilifunikwa na kontena za maroli hayo baada ya kwa pamoja maroli hayo kutumbukia katika korongo la mlima huo.

Ajali hiyo ni moja kati ya ajali nyingi zinazoendelea kutokea mkoani Iringa huku ukiwa katika maandalizi ya kitaifa ya kuadhimisha Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani.

Kamanda Mpinga aliwakumbusha madereva kuzingatia sheria za barabarani na akahidi kwamba msako mkali wa wale wanaokiuka sheria hizo utaanza kufanywa.

Mpinga alisema kikosi cha usalama barabarani kitaweka utaratibu wa ukaguzi maalumu wa magari katika maeneo ambayo ajali zimekuwa zikitokea mara kwa mara ikiwa ni pamoja na katika mlima huo.

Credit: Frank Leonard

Habari haijazungumzia mabasi yaliyotajwa kwenye heading
 
Back
Top Bottom