Ajali barabarani Muro yanusurika

Ajali barabarani Muro yanusurika

mpambanaji

Member
Joined
Apr 5, 2009
Posts
22
Reaction score
1
Katika hali ya kumshukuru Mola, tairi ya mbele kushoto bus la Muro toka Mbeya lapasuka tairi Morogoro wakati likiingia stand kuu ya Morogoro. Mwendo mdogo wa 5km/h umepelekea kulinusuru gari hilo katika janga kubwa ambalo lingeweza kutokea Kama mwendo ungekuwa tuliouzoea
 
Attachments

  • image.jpg
    image.jpg
    553.8 KB · Views: 1,556
Tujadiliane hapa kidogo. Inakuwaje gari liana toka Mbeya kwa safari ndefu ya kilometa zisizopungua 800 bila kuwa hata na tairi la dharura? Gari limeegeshwa Msamvu, yapata saa Moja sasa na hakuna ufumbuzi wowote. Je, utoshelevu wa vifaa vya gari si sehemu ya ukaguzi wa kila siku wa jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani hasa kwa gari za abiria kabla yakuanza safari?
 
baada ta muda wa saa nzima, ya kuhangaika na kupata tairi la kuazima, Polisi Msamvu waibuka, hakuna safari bila spare tyre. Mbeya walikuwa wapi? Ajali ungekuwa mbaya wangejiteteaje? Baada ya kulipa fine gari laruhusiwa. Nini bora, fine au usalama? Sasa limeruhusiwa
 
Katika hali ya kumshukuru Mola, tairi ya mbele kushoto bus la Muro toka Mbeya lapasuka tairi Morogoro wakati likiingia stand kuu ya Morogoro. Mwendo mdogo wa 5km/h umepelekea kulinusuru gari hilo katika janga kubwa ambalo lingeweza kutokea Kama mwendo ungekuwa tuliouzoea

Kama wangekuwa wana kwenda 40 km/h mambo yangekuwa tofauti. Hata 20 km/h ingewatikisa.

Mimi bado nalia na wamiliki wa hili basi jinsi wanavyojiabisha hadharani. Kama lugha huijui, si bora uulize?

Neno "Princes" halipo mahala popote kwenye istilahi ya lugha ya Kiingereza. Unaweza kuwa na maneno "Prince" au "Princess", ambayo maana yake ni "Mwana Mfalme" kwa neno "Prince" na "Binti Mfalme" kwa neno "Princess".

Mimi nina uhakika kwamba kulikuwa na mabishano makali sana kati ya aliyepewa zabuni ya kuchora jina hilo la "Princes Muro" kwenye ubavu wa mabasi hayo na mmiliki wake. Huku kujidhalilisha kwa kutotumia maneno sahihi ya lugha za kigeni, kwa mfano kutumia neno "equipments" badala ya "equipment" kukome! Nina hakika watalii kutoka mabara ya Ulaya na Marekani huwa wanaangua kicheko kila wanapoyaona mabasi haya kwa mara ya kwanza, wakitazamana na kusema "T.I.A. This is Africa!" (Usemi huu unatokana na filamu maarufu "Blood Diamonds" iliyochezwa barani Afrika kwa sehemu kubwa, ikionesha jinsi biashara haramu ya almasi ilivyoshamiri barani hapa. Mmojawapo wa waigizaji wa kizungu alitamka maneno haya akimwambia mwenzake "T.I.A. This is Africa!", akimwelekeza kutoshangazwa sana na mambo ya Afrika.)

T.I.A. This is Africa!
 
Back
Top Bottom