Ajali Arusha: Basi la Saibaba lagongana uso kwa uso na Lori, watatu wapoteza maisha

chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
20,819
26,180
Watu watatu wapoteza maisha katika ajali iliyohusisha basi la Saibaba

Watu watatu wamefariki dunia na wengine sita kujeruhiwa vibaya katika eneo la sakina jijini Arusha, baada ya basi linalo milikiwa na kampuni ya Saibaba lililokuwa katika majaribio kugongana uso kwa uso na lori ambalo lilikuwa likitokea eneo la Oldonyosambu wilayani Arumeru mkoani Arusha.

Basi hilo lenye usajili namba T 720 ADE lililigonga na lori hilo lenye usajili namba T742 CRS ambapo kwa mujibu wa Mashuhuda wa ajari hiyo ,wanadai ajali hiyo ilitokea majira ya saa tisa alfajiri wakati basi la Saibaba lilipokuwa likifanyiwa majaribio na fundi aliyejulikana kwa jina la Athuman sadiki naghafla lilizimika taa zote za mbele na kupoteza mwelekeo na ndipo lilipo ligonga lori hilo lillilokuwa limebeba shehena ya karoti.

Hata hivyo inadaiwa kuwa marehemu na majeruhi wote walikuwa abiria wa lori.

Channel ten inafanya jitihada za kufika katika hospital ya mkoa wa Arusha mount meru ambapo uongozi wa haspitali hiyo unashindwa kutoa ushirikiano wa aina yoyote licha ya majeruhi na miili ya marehemu kuripotiwa kufikishwa katika hospital hiyo huku kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Arusha Liberatus Sabasi akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na tayari dereva wa basi anashikiliwa na jeshi hilo.

Kwa mujibu wa kamanda Sabasi majina ya marehemu hao ni Nouvel Joseph ambaye ndiye alikuwa dereva wa lori hilo wengine ni ,James Kaaya na Paschal Peter wote wakiwa abiria katika lori hilo.

uploadfromtaptalk1457931957464.jpg
 
Hayo mabasi niliachaga kupanda siku nyingi sana, madereva wake huwa hawaheshimu sheria za barabarani
 
Kwanini hospital ya Mount Meru imeshindwa kutoa ushirikiano?
R.I.P anyway
 
Haya majaribio yameleta umauti kwa wapendwa wetu, wapumzike kwa Amani.
 
Sasa fundi atafanyaje majaribio saa tisa za usiku??? Uumhhh
 
Huyo dereva mchawi? Anafanyaje majaribio saa tisa usiku?

Mara nyingi mabasi vimeo yanayotoka ya kwanza Arusha hufanyiwa majaribio muda huo mkuu, wala hakuna uchawi.
Fikiria gari lilifika jioni jana yake huku likiwa na tatizo, kwa vyovyote litatengezwa usiku na kujaribiwa muda huo.
Shida iliyopo mabasi ya Saibaba ni mabovu kupita kiasi na mara nyingi husimama sana njiani. Yazuiwe tu kusafiri safari ndefu kama serikali ilivyofanya kwa baadhi ya mabasi ya Dar Express.

Ova
 
Back
Top Bottom