Aishitaki Kampuni ya Pafyumu Kwa Kushindwa Kupata Mchumba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Aishitaki Kampuni ya Pafyumu Kwa Kushindwa Kupata Mchumba

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Dr. Chapa Kiuno, Nov 3, 2009.

 1. Dr. Chapa Kiuno

  Dr. Chapa Kiuno JF-Expert Member

  #1
  Nov 3, 2009
  Joined: Sep 11, 2009
  Messages: 445
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  </SPAN>
  Tuesday, November 03, 2009 7:56 AM
  Mwanaume mmoja nchini India ameifungulia kesi mahakamani kampuni moja ya pafyumu kwa kushindwa kupata mpenzi baada ya kutumia pafyumu za kampuni hiyo kwa miaka saba ingawa tangazo la kampuni hiyo linadai ukitumia pafyumu za kampuni hiyo basi wawanake watakuwa wakijipendeza kwako.


  Mwanaume mmoja nchini India ameifikisha mahakamani kampuni ya pafyumu ya Lynx kwa kushindwa kupata mpenzi ingawa amekuwa akitumia bidhaa za kampuni hiyo kwa miaka saba sasa.

  Vaibhav Bedi, 26, anaidai kampuni ya Unilever fidia ya dola 91,000 kwa matatizo ya kisaikolojia waliyomsaidia baada ya kushindwa kupata mpenzi kama tangazo la kampuni hiyo linavyodai.

  Tangazo la pafyumu ya kampuni kwenye luninga linawaonyesha wanawake warembo wakijipendekeza na kutaka kuwa karibu na wanaume wanaotumia pafyumu za Lynx zinazojulikana kama Axe nchini India.

  "Kampuni hii imenilaghai kwasababu katika tangazo lao wanasema wanawake watavutiwa kwako iwapo utatumia Axe.. nimetumia kwa miaka saba na hajawahi kunifata msichana hata mmoja", alisema Bedi katika jalada la kesi yake lililowasilishwa mahakamani.

  Mahakama mjini New Delhi imekubali chupa zilizotumika za shampoo, sabuni ya kuogea, deodorant na mafuta ya nywele kama ushahidi katika kesi hiyo.

  Mwanasheria wa Bedi, bwana Ram Jethmalani alisema kuwa anatarajia Unilever watataka kulimaliza suala hilo kwa kufanya muafaka nje ya mahakama.

  Kampuni ya Unilever imekataa kusema chochote kuhusiana na kesi hiyo.</SPAN>


  Source: News Agencies
   
 2. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #2
  Nov 3, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Alikuwa domo zege! Kwani alitegemea avuliwe nanihii kwa harufu ya Pafyumu?
   
 3. O

  Omumura JF-Expert Member

  #3
  Nov 4, 2009
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  angetumia cobra aone matokeo, angewakimbia wachumba!
   
Loading...