Jamani wakati mwingine tuwe wakweli Manula amefanya kazi kubwa sana hasa kwenye mechi ya Namibia. Ni kweli Manula ana madhaifu ya kutoka bila mpangilio na udhaifu wa kucheza krosi na kona. Lakini kwenye mechi dhidi ya Namibia alifanya hayo makosa mara moja au mbili tu. Na Manula ndiye aliyeinua morali ya timu nzima kwa kufanya "saves" za maana. Huu Usimba na Uyanga usitufanye tuwe vipofu hata kwenye mambo yaliyo wazi. Na hongera sana kwa benchi la ufundi kwa kuanza na Farid badala ya Mhilu hapo ndio chachu ya ushindi ilipoanzia.