Airtel na Airtel Money, Badilikeni

Jamaa liongo, pesa ikirudi kwa mteja hawezi kuitumia hadi wakala apigiwe athibitishe. ukiona hivyo kapigiwa wiki nzima hapokei huyo
Mimi Tigo walinirudishia muda huohuo nikaituma Airtel na ikafika.

Cha msingi na secondary hawa jamaa Mawakala wao inatakiwa wapewe vipaumbe na sio kuwaona wasumbufu wakati wametaka wenyewe kutoa huhuma ya jamii.
 
Jamaa liongo, pesa ikirudi kwa mteja hawezi kuitumia hadi wakala apigiwe athibitishe. ukiona hivyo kapigiwa wiki nzima hapokei huyo
Kweli Mkuu Muamala Wa Wakala na Mteja Uliotolewa Ombi la Kuzuiliwa Huwaga Haurudishwi Bila Kufanya Mawasiliano na Wakala Ndipo Hiyo Fedha Hurudishwa.
 
... kurudisha kutoka namba ya kawaida shortly after transaction haina tatizo sana. Tatizo ni kurudisha kutoka kwa wakala (ambaye tayari alishakukabidhi cash) au namba za "lipa hapa kwa ..." (umeshakabidhiwa mali/huduma hapo ndipo walichemka.
Unajua dudus,,kuna changamoto moja bado ina nipa maswali sana kichwani juu ya kurudisha muamala na kuwa na access ya kuitumia tena mda huo huo...hii sehem inabdi waizingatie sana,mfano mimi nakuja kwenye duka lako kununua bidhaa,,nikasema sina cash naweza kukurushia kwenye simu yako ya kawaida let's say ni mpesa au tigopesa au airtelmoney...mi ikarusha muamala na ukanikabidhi bidhaa nikaingia chocho la pili nikarudisha muamala fasta nikatoa pesa kwa wakal nikatupa pain...hili jambo hawajakaa kujiuliza mianya hii ya kitapeli kwamba inaweza kufanyika..yani bado nadhani,waweze kuishikilia hela mpk kuwe na uthibitisho wa kweli kwa aliyepokea...kusiwe rahisi rahisi tu mtu anarudisha muamala...upumbavu huu naukataa kabisa...wakae chini warekebishe hilo...pia huduma ya lipa km nao wanaruhusu ujinga huu nawaomba pia warekebishe,ivi unapobuni huduma kwann usiwaze nje ya box juu ya mianya ya kitapeli.
Ova
 
Unajua dudus,,kuna changamoto moja bado ina nipa maswali sana kichwani juu ya kurudisha muamala na kuwa na access ya kuitumia tena mda huo huo...hii sehem inabdi waizingatie sana,mfano mimi nakuja kwenye duka lako kununua bidhaa,,nikasema sina cash naweza kukurushia kwenye simu yako ya kawaida let's say ni mpesa au tigopesa au airtelmoney...mi ikarusha muamala na ukanikabidhi bidhaa nikaingia chocho la pili nikarudisha muamala fasta nikatoa pesa kwa wakal nikatupa pain...hili jambo hawajakaa kujiuliza mianya hii ya kitapeli kwamba inaweza kufanyika..yani bado nadhani,waweze kuishikilia hela mpk kuwe na uthibitisho wa kweli kwa aliyepokea...kusiwe rahisi rahisi tu mtu anarudisha muamala...upumbavu huu naukataa kabisa...wakae chini warekebishe hilo...
Ova
... wananchi waelimishwe kutolipia bidhaa au huduma kwa namba za kawaida. Malipo yawe kwa namba maalum za "Lipia hapa kwa ...". Case closed.
 
mimi huwa nasema aitel ndio mtandao wa ajabu ajabu kuli yote nchini.

zamani ulikiwa ukichukua line,ukabonyeza menu ya airtel money,ukiingiza namba ya siri mata 3 ikiwa sio yenyewe wanakutumia namba mpya ya kiazio.

sasa fikiria sio aliushika simu sio mhusika,nini kinafuata hapo!!!
 
Hiyo huduma ya kufanya confirmation Kama hii pesa inatakiwa iwe reversed au la Airtel wanayo, muhudumu kabla ya kurudisha pesa anapiga simu kwa aliyewekewa pesa kimakosa kuhakiki...na sio Airtel tu nadhani Ni mitandao yote wanafanya hvyo

Hapo ipo namna Kati ya huyo tapeli na muhudumu wa kampuni....pumbavu zao,ndo tatizo la kutumia requirement agency,kwa ajili ya kukutafutia wafanyakazi,wao hawaangalii quality as long as una basic ya computer Basi kazi umepata...

Na asilimia kubwa wanaofanya hzo kazi Ni vijana waliomaliza elimu bado michongo ya kazi haijaa kaa sawa,wapo nyumbani au kwa ndugu na wengine ndo wametoka mikoani

Mishahara midogo Sana,na vijana wanadream kubwa(za kwenye movie)wanataka wapige pesa kwa haraka
 
Kama ni kweli Airtel wanarudisha muamala bila kuwasiliana na wakala au mtu yeyote yule toka kwenye akaunti, basi huo ni wizi na utapeli, unatoaje pesa kwenye akaunti ya mtu bila kuwasiliana nae???!!!! Maaana wengine tunaliowa kwa njia ya simu, sasa mtu nishampa mzigo halafu akarudisha muamala, unafikiri nitawaelewa?!!!
 
Hii iliishaje??


Mkuuu Kijana wangu amepigwa Laki Tano na Ishirini yaani.


wiki kadhaa nyuma Jamaa wa pemben, amepigwa 1.2M

Alafu hawa wajinga nawapigia wananipa uswahili mwingi
 
Sasa uzi wa nyodo unahusika vipi?
 
Ingekuwa ni rahisi hivyo watu wengi wangefanya na hizo cases zingekuwa nyingi sana, hata mimi nimeenda kutoa halafu nirudisha fasta na line nitupe huko.
Nadhani huyo alipigiwa hakupokea au na yeye amehusika kucheza dili kijanza(amemzunguka boss wake)
 
Kama ni kweli Airtel wanarudisha muamala bila kuwasiliana na wakala au mtu yeyote yule toka kwenye akaunti, basi huo ni wizi na utapeli, unatoaje pesa kwenye akaunti ya mtu bila kuwasiliana nae???!!!! Maaana wengine tunaliowa kwa njia ya simu, sasa mtu nishampa mzigo halafu akarudisha muamala, unafikiri nitawaelewa?!!!
Mkuu ,nahisi shida niivi vijamaa wanavyoviajiri nakuvilipa laki mbili nanusu , kazi kwao ni mazoea, "Usikate simu tatizo lako tunalishugulikia".
 
Mara baada ya kufatilia ili swala


Ilikua hivi... Mteja alotoa Hela alikua kashirikiana na mwizi.

Na mteja alokuja, yeye hakutoa Hela

Badala yake , YULE MWIZI MWENZIE ALIYEKO SINGIDA, NDIYE ALIYETOA HELA ...

HUYI MWIZI ALOKUJA KWA OFISI YANGU YEYE ALIKUA ANAJIFANYA KUTOA KUMBE NDO ALIKUA ANATUMA NAMBA YA WAKALA KWA MWIZI WA SINGIDA.


MWIZI WA SINGIDA AKATOA HELA... NA MUAMALA KIJANA WANGU AKAUONA KAMA KAWAIDA NA KUMPA PESA.



ALIVYOONDOKA, MWIZI WA SINGIDA, AKAPIGA AIRTEL MONEY WALIVYOONA ENEO ALIPO, WAKARIDHIKA NAYE NAKUMRUDISHIA PESA.
 
Back
Top Bottom