Airtel Imesharudishwa kwenye umiliki wa Serikali?

Kinyungu

Platinum Member
Joined
Apr 6, 2008
Posts
22,811
Reaction score
46,015
Wadau mtakumbuka mwishoni mwa Disemba 2017, Mtukufu raisi wetu kipenzi Mheshimiwa Dr. (PhD) Magufuli alitutangazi kuwa kulikuwa na ukiukwaji wa sheria katika uuzwaji wa kampuni ya mawasiliano ya Airtel, kwanza kwenda Celltel, baadaye Zain na hatimaye hii ya sasa Airtel, na kwa kimsingi kampuni hiyo inapaswa kurudishwa chini ya umiliki wa serikali.

Katika kuonesha anamanisha alichokuwa akikisema aliamuru Waziri wa fedha Mheshimiwa Mpango kufanya uchunguzi na kumpa ripoti ndani ya wiki mbili.(Hili lilishafanyika)

Sasa mimi naomba kufahamu kama hii kampuni ya mawasiliano imesharudishwa kwenye umiliki wa serikali na hatua walizochukuliwa wale waliolihujumu taifa kwa uuzwaji wake ambao haukuzingatia maslahi ya nchi.
 
Taratibu Zipo Mwisho Yaani Serikali Ya Viwanda Ichukue Airtel Yake Maana Majizi Hayana Nafasi
 
Wadau mtakumbuka mwishoni mwa Disemba 2017, Mtukufu raisi wetu kipenzi Mheshimiwa Dr. (PhD) Magufuli alitutangazi kuwa kulikuwa na ukiukwaji wa sheria katika uuzwaji wa kampuni ya mawasiliano ya Airtel, kwanza kwenda Celltel, baadaye Zain na hatimaye hii ya sasa Airtel, na kwa kimsingi kampuni hiyo inapaswa kurudishwa chini ya umiliki wa serikali.

Katika kuonesha anamanisha alichokuwa akikisema aliamuru Waziri wa fedha Mheshimiwa Mpango kufanya uchunguzi na kumpa ripoti ndani ya wiki mbili.(Hili lilishafanyika)

Sasa mimi naomba kufahamu kama hii kampuni ya mawasiliano imesharudishwa kwenye umiliki wa serikali na hatua walizochukuliwa wale waliolihujumu taifa kwa uuzwaji wake ambao haukuzingatia maslahi ya nchi.
kuna kitu inaitwa "siasa", ni kitu cha ajabu sana. hiyo imeshapita, kwani barrick/accasia walitulipa mzee? bei gani?
 
Hahaha TTCL hata hawajui ni kampuni ya nini, waichukue airtel waipeleke wapi ikulu?! ATCL inawafia huko jasho linawatoka hata hawajui wafanye nini wewe unaulizia airtel?! Siku wakiichukua inakufa hapohapo na kuhakikishia.
 
Airtel itarudishwa siku tukilipwa zile hela zetu za Noah. Teh teh teh
Tujifunze kutofautisha kiki na vitu halisi.
 
Mkuu Mtukufu raisi alikuwa anaongea kwa kujiamini sana. Nilijua baada ya zile wiki mbili alizopewa Mh. Mpango Airtel itakuwa kwenye mikono salama ya Serikali lakini inaonekana kama wanataka hili nalo lipite tu kimya kimya kama Makinikia
 
Ni mwendo wa kiki tu. Kitu gani kimefanikiwa hadi sasa?
Miaka kumi ya utawala wake, Tanzania Itakuwa imerudi nyuma sana.
Kwanza itafika miaka kumi?
 
Back
Top Bottom