Air Zara International Yasimamisha Safari Zake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Air Zara International Yasimamisha Safari Zake

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Ilulu, Nov 23, 2009.

 1. Ilulu

  Ilulu Senior Member

  #1
  Nov 23, 2009
  Joined: Mar 22, 2008
  Messages: 161
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hatimaye leo muda si mrefu nikiwa nawasiliana na wakala wa Usafiri wa Ndege, ameniarifu kuwa Kampuni ya Air Zara International imesitisha huduma zake until further notice. Niliulizia usafiri wa Dar-Mwanza-Dar.
  Nakumbuka kumekuwa na vitimbi kadha wa kadha Air Zara wamekuwa wakifanyiwa hivi siku za karibuni, na wapo walioandika juu ya hali hiyo hapa jamvini... siikumbuki ile nyuzi (thread).

  Matukio kama haya yaliikuta Kampuni ya Community Air na hatimaye kutoweka kabisa katika anga ya Tanzania.

  Ninachojiuliza, kwanini makampuni ya bei nafuu katika huduma hasa hii ya usafiri wa anga hupata misukosuko mingi hapa Tanzania?

  Bei ya return Ticket ya Air Zara, Dar-Mwanza-Dar ni Tshs 262,000 ambayo ni cheap mara dufu ulikilinganisha na Makapuni mengine.

  Wenye taarifa ya kina tafadhali tufahamishane
   
 2. Tripo9

  Tripo9 JF-Expert Member

  #2
  Nov 23, 2009
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 2,168
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Haya sasa
   
 3. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #3
  Nov 23, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,867
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Air Zara ni mali ya nani? Kwa nini wafulie mapema hivyo?
   
 4. B

  ByaseL JF-Expert Member

  #4
  Nov 23, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 2,223
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Jibu lake ni rahisi sana. Biashara ya ndege inahitaji mtaji mkubwa sana. Kwanza ni biashara ambayo gharama zake ziko juu na pili ni biashara ambayo wateja wake ni sensitive sana. Kuna mambo mengi ambayo abiria uyatilia maanani kabla ya kuamua kupanda ndege hususan usalama (safety) wa ndege, uhakika wa ratiba (schedule reliabililty), convinience ya ratiba ya ndege (unatoka au kufika saa ngapi), huduma ndani ya ndege, na bei ya tiketi ingawa hiki sio lazima sana maana inategemea na uwezo wa mteja, n.k

  Ukianzisha huduma za ndege lazima uwe na mtaji mkubwa ( working capital) maana inachukua muda mrefu kuweza kupata abiria wakutosha kuweza kuanza kupata angalau pesa za kujiendesha na faida. Wawekezaji wengi ufanya very optimistic forecasts wakifikiri wakiweka ndege abiria watakuja tu ili mradi nauli ziko chini kumbe sivyo. Baada ya safari kadhaa bila abiria wakutosha mashrka kama Community na Zahra ujikuta wameishiwa na hivyo kusimamisha huduma. Kwa kifupi the airline business is a cashflow business. Period.
   
 5. s

  shabanimzungu Senior Member

  #5
  Nov 23, 2009
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 182
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  bwana the business rivalry is what is suffocating the airline business..old players do not want Air Zahra to come in so sabotage may be the issue here........
   
Loading...