Air Tanzania wakusanya BILIONI 9 kwa miezi minne

for life

JF-Expert Member
Sep 22, 2014
3,396
4,437
Shirika la Ndege Tanzania ‘ATCL’ kupitia kwa Mkurugenzi Mkuu, Ladislaus Matindi amesema kuwa wamekusanya kiasi cha Sh. BILIONI 9 kwa kipindi cha miezi minne tangu ndege mbili za Bombardier Q400 zianze kufanya kazi.

Tumejitahidi sana kila tunachokipokea kinaingia katika mfuko wa shirika, mapato yote ambayo tumeyapata yamekuwa yakikusanywa kwa wakati unaotakiwa na kuhakikisha kuwa hakuna upotevu wowote, kumekuwa na nidhamu kubwa katika ukusanyaji wa mapato kwa mfano wa mizigo ya ziada.’ – Ladislaus Matindi.
 
Wanafiki chadema watakuja kupinga hapa

Wanadhani kila mtu ana akili fupi kama wao
 
Mwalimu Wangu Aliniambia Hatoi Heshima Kwa Kampuni Yeyote Kwa Makusanyo au Mapato Sababu Hiyo Siyo Lengo la Biashara.

Lengo la Biashara Yeyote ni Faida Kama Hujataja Faida Unakuwa Hujamweleza Kitu Chochote.

Mwisho wa Kunukuhu
 
Mwalimu Wangu Aliniambia Hatoi Heshima Kwa Kampuni Yeyote Kwa Makusanyo au Mapato Sababu Hiyo Siyo Lengo la Biashara.

Lengo la Biashara Yeyote ni Faida Kama Hujataja Faida Unakuwa Hujamweleza Kitu Chochote.

Mwisho wa Kunukuhu
Haya tutajie faida ya Mboe kuuza ngada
 
Sio kwa uongo huu jamani! Hata wangekuwa wanalipisha mizigo yote inayoingia ndani ya ndege...bado huu muujiza utakuwa haujakamika!
 
Fake reports....airline kibao zinapiga loss mwanzo mwisho! KQ,SA,Air Dubai,Air China,Royal moroc,Rwanda air,Air Namibia,Air Zim,Air Botswana! Nk,waweke Financials zao hapa tuchambue line by line
 
Kama wamepata hizo pesa waanze kulipa madeni. Walipe PPF za wastaafu wao toka wa mwaka 2010 ambao wanadai baadhi ya miaka ambayo michango yao haikupelekwa PPF hali iliyo fanya wapate pension kidogo hapo walikatwa ktk mishahara yao. PPF waliishitaki ATCL mahakamani na kuamriwa kukamata mali ilikulipa madai ya wastaafu wao kitendo ambacho hakijafanyika kwa kuwa ni kampuni ya serikali. Hivyo basi uwongozi wa ATCL uwalipe PPF madai yao ili nao wawalipe wastaafu wa ATCL.
 
Safi, lakini gharama za uendeshaji zikoje? Kama gharama ni bill 20 hapo ni hasara. Watoe full picture.
 
Mnataka kusema kuwa walikuwa wanaingiza 75 milllion tsh kila day,waacheni hizo.....eb mtu aniambie ATCL wana ndege ngapi kwanza!
 
Back
Top Bottom