Aina za watu tunaobishana nao mitandaoni

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,111
115,902
Rostam Aziz: mahakama zetu sio huru ni sahihi Kwa Dp world kuweka kipengele cha mahakama ya South Africa.

Kwanini mahakama zisimchukulie hatua kali iwe fundisho. Anafikiri ukiwa na pesa unaweza iletea mahakama dharau? Mahakama zisikubali kuchafuliwa zimshughulikie haraka Sana iwe fundisho. Mahakama zetu ni huru na ziachwe zifanye kazi yake bila kuingiliwa...

Few day latter..
Mahakama: Mkataba wa DP World hauna shida, zipo kasoro ndogo zinaweza kurekebishika kwenye mkataba unaofata wa HGA. uwekezaji uendelee.

Wadau wakasema Rostam alikuwa sahihi kabisa mahakama zetu sio huru...

Kikwete: watu wakikosoa waachwe wakosoe unarekebisha kama wanacho ongea ni kweli.

Ma great thinkers wa JF: Samia anapaswa kumsikiliza Mzee wetu Kikwete...Rais mstaafu ana busara sana...

Few days latter..
Kikwete: Viongozi wa dini wasichanganye dini na siasa....

Wadau: Huyu Mzee anatakiwa afunge mdomo wake asitupangie kila mtu ana Uhuru wa kutoa maoni yake.

Very interesting
 
Mambo hayaendi namna hiyo The Boss , nakubaliana na wewe kabisa kwamba Kuna watu Wana ushabiki usio na tija hapa JF.

Nnachopinga ni kwamba, kama Leo The Monk kaongea kuhusu jambo na kutoa maoni yake haimaanishi hawezi kutoa maoni ya kitu kingine Kwa mtizamo tofauti, inabaki kuwa hayo ni mawazo na maoni yake.

Tatizo linakuja hapa, mtu anataka kumfanya binadamu kama rejea ya kipimo na Yuko sahihi siku zote, hakuna binadamu wa aina hiyo na ni hatari sana kuweka tumaini au Imani Kwa binadamu badala ya hoja zake.

Unakuta mtu anasema namkubali sana flani, hiyo ni tatizo, yeye ana misimamo yake, maslahi yake binafsi na mitazamo tofauti kuhusu Kila jambo, lazima atabadilika kulingana na Hilo jambo linalojadiliwa.

Tusiweke nguvu kubwa sana kuunga mkono au kushabikia watu, tujikite kwenye hoja, hapo ndio itakua tumepunguza hizi sarakasi zinaziendelea.
 
Kwenye maisha ukifanya vyema unasifiwa, ukikosea unaambiwa, hiyo ndio kawaida ya binadamu, au wewe ulitaka hao GT uliowakebehi hapa wafanyeje, tukubali tu kwamba UWEKEZAJI NI MZURI, ILA MKATABA NI MBOVU, nendeni mkabadilishe mje na kitu chenye manufaa na faida kwa UMMA.
 
Rostam Aziz: mahakama zetu sio huru ni sahihi Kwa Dp world kuweka kipengele cha mahakama ya South Africa...

"Ma great thinkers wa JF:mshenzi Sana huyu mwarabu koko...analeta dharau Kwa mahakama zetu...?...kwanza kwanini mahakama zisimchukulie hatua Kali iwe fundisho..... anafikiri ukiwa na pesa unaweza iletea mahakama dharau ?...
Hivi kuwa Great Thinker maana yake ni kuwa na msimamo kuhusu mtu au hoja?

NB: Msingi wa hoja haubadiliki hasa kama ni wa kisayansi. Mtu anayetoa hoja anaweza akabadilika hasa kama ni mwanasiasa
 
Back
Top Bottom