AINA YA MARAFIKI WANAOKUZUNGUKA

AINA YA MARAFIKI WANAOKUZUNGUKA

Konzo Ikweta

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2013
Posts
745
Reaction score
1,504
Kwa Mujibu wa Adam Grant mwandishi wa kitabu cha “Give and Take” kuna aina kuu tatu za marafiki katika maisha yetu.Na wewe pia unaangukia katika aina mojawapo ya kundi hili kama rafiki wa wengine:

1)TAKERS (Wanaotaka kupokea tu)

Hawa huwa kila siku wamekaa mkao wa kupokea tu na sio kutoa.Wanataka wakipata shida wewe ndio uwe wa kwanza kuwasaidia ila wewe ukiwa na shida hawaonekani.Msipowasiliana hawafanyi bidii kukutafuta bali wanaanza kulaumu kuwa hauwatafuti.Kifupi WAMEJIHESABIA HAKI kuwa wewe ndio una wajibu wa KUFANYA KITU kwao kila siku na sio wao.Ukiwasaidia mambo 100 ila ukashindwa kuwasaida katika moja WANAGEUZA hilo moja kuwa ni UBAYA wako wa KUUTANGAZA kila KONA na wanasahu mema yote uliyowafanyia.

2) MATCHERS (Nipe Nikupe)

Hawa wanaishi kwa mbadilishano,hata kama hawajakuambia.Ukiwafanyia kitu na wenyewe wanakufanyia usipofanya,na wao hawafanyi.Ukisahau birthday yao na wao watajisahaulisha ya kwako.Watu hawa wanahamasishwa zaidi pale unaporudisha wema waliokufanyia.

2) GIVERS (Wanatoa tu kila siku)

Hawa huwa wamejikita katika kusaidia na kuwakumbuka wengine tu.Changamoto yao ni kuwa mambo yao mengi binafsi huwa yanaishia kuharibika.Wana muda wa kufanya ya kila mtu isipokuwa kufanya ya kwao.Huwa wanapendwa na wengi ingawa mwisho wa siku huwa wanalaumiwa na wengi kwa kutokumbuka kufanya mambo yao ya msingi.

Je,umeshawahi kukutana na rafiki yoyote kati ya hawa?

#Nanauka
Great%20Thinkers%2020190614_085046.jpeg
 
#NanaukaView attachment 1150349
Upo vizuri mkuu
 
Mara ya mwisho kuwa na rafiki wa kuaminiana ilikuwa 2005 nikiwa sekondari.

hata kazini nashindwa kuweka urafiki wa karibu kwa sababu sijui kuchagua rafiki.

Nina tatizo gani?
 
Futa marafiki wote anza upya
 
Ukiwa rafiki yangu basi nakuwa rafiki namba 1. Oooh yeeeah!!
 
Back
Top Bottom