Aina sita za mabusu na maana zake

Eddy Tarimo

Member
Nov 27, 2016
27
38
Kiss (Busu) sio kwa mpenzi tu pekeake tumeona wazazi wakiwaaga watoto wao kwa kuwakumbatia na kuwabusu, iwe ni shavuni, kwenye paji la uso au mdomoni kwa baadhi ya wazazi.

Yapo mabusu mengi ila nimechagua aina saba tu ambazo najua kwa namna moja au nyingine ni mabusu maarufu zaidi, na leo nitafafanua kila busu na maana yake, ili hata ukipata busu kutoka kwa mtu ujue alimaanisha nini.

1.Busu katika paji la Uso
Busu hili maana yake nakujali nakupenda, na nakuthamini, ila hutumika kirafiki kindungu au hata kwa wapenzi pia.

2.Busu Shavuni.
Hutumika kwa watu wote, ndugu, marafiki hata wapenzi pia, ni ishara ya upendo kwa mtu wako wa karibu.

3.Busu Mdomoni, (Lip to Lip)
Linaweza kutumika kwa wapenzi, marafiki hata wazazi ni busu kavu lisilo husisha ulimi, ni ishara ya mapenzi mazito na heshima kwa yule mtu.

4.Busu la Mdomo na Ulimi (French Kiss)
Busu hili huusisha ulimi na ulimi baina ya watu wawili hutumika zaidi kwa wapenzi, huitwa deep kiss au wet kiss ni ishara ya mapenzi mazito kwa mtu wako wa karibu.

5.Busu la Shingo
Ni busu la kuomba kitu zaidi, yaani anaekupa busu la shingo ni mtu anaehitaji zaidi ya busu, linapendeza zaidi kama mtu anakupa busu hili awe nyuma ya mgongo wako.

6.Busu la Sikio
Linaweza kuanzia kwenye mdomo, likahamia shingoni hadi sikioni hii pia ni aina ya busu baina ya wapenzi ni ishara pia ya kuwa na mahitaji zaidi ya busu.

6.Busu juu ya Bega
Busu hili halina tofauti sana na busu la shingo, ni ishara ya kuhitaji zaidi kutoka kwa mpenzi wako. Unaweza tumia vitendo katika kuomba unachohitaji na si maneno.

    
 
Watu wamekuuliza sana busu la papuchi ama dushelele linaitwaje? Hautaki kujibia?
Ukifungua darasa kama mwalimu, kubali pia kujibu maswali magumu ambayo sazingine haupendi kuyajibu ama yanakukera.
 
Uzungu huu unipite mbali, siwezi na narudia siwezi na haitakuja kutokea nikutanishe midomo yangu na ndugu yangu au mzazi wangu eti kisa tu naonyesha upendo
 
Mbona umesahau busu la mkononi mkuu!? mnapena mikono halafu mnabusu mikono ile mliyopeana.
Bus la mkononi huashiria furaha aman n upendo, kama umebahatika kuish au kuembelea bibi na babu basi pale unapokua umewasili too kutka safarin mara nying akikuona hua anakubusu mkononi akiashiria ni furaha upendo n aman
 
  • Thanks
Reactions: BAK

Similar Discussions

Back
Top Bottom