Jacobus
JF-Expert Member
- Mar 29, 2011
- 4,700
- 1,721
Wakuu,
Leo katika pitapita yangu mitaa fulani nimewakuta jamaa kama wanne hivi wakimmwagia maji machafu mdada huku kicheko kikiendelea. Nilisistuka na kuhoji kulikoni maana nilidhani mdada kawatendea jambo baya hao jamaa hivo wakaamua kumwadhibu kwa kummwagia maji machafu toka barabarani, jibu nililipewa ninilifanya niishiwe mbavu kwa kucheka.
Eti leo ni siku ya kusherehekea kuzaliwa kwa huyo mdada hivo walikuwa wakimrejesha enzi ya utoto kwa kuchafuka kama watoto wanavochafuka kwa michezo yao. Nikatafakari mtindo huu na kuanza kujiuliza labda ni utakata wa kuandaa mambo ya keki na vinywaji ndo kumewafanya kuonesha aina hii ya sherehe (birthday) barabarani.
Dunia ina wabunifu wengi.