Kusherehekea siku ya kuzaliwa hali ya kuwa wananchi wanateseka na umasikini

Abraham Lincolnn

JF-Expert Member
Apr 12, 2018
2,510
4,217
Wakuu nisipende kuwachosha
Ila inasikitisha sana kuona ikulu ambapo Nyerere aliwahi kusema kuwa ni mahala patakatifu imebadilika na kuwa pango la walanguzi.

Leo ikulu hapafanyiki tena mikutano ya kujadili mikataba ya madini,utiaji saini miradi ya maendeleo n.k Bali imekuwa sehemu ya kufanya karamu kuonana na viongozi wastaafu kupongezana n.k

Kiongozi mkuu wa nchi amekuwa mwepesi kuhudhuri shughuli nyepesi nyepesi zisizokuwa na tija kubwa kwa taifa huku akiacha hoja za msingi na miradi ya msingi ya kimaendeleo hususan kwa nchi yetu masikini ambayo bado hali ya uchumi si nzuri na changamoto ni nyingi mno kwa wananchi ambao wamepigwa na maisha hata hawakumbuki siku zao za kuzaliwa.

Kiongozi mkuu wa nchi amebaki kufanya makongamano,teuzi,birthday party n.k huku akisahau kuna miradi ya kimkakati kama JNHP, SGR pia anapaswa kubrainnstorm kuja na miradi mingi ili uchumi ukue watanzania waondokane na umasikini unaowatesa miaka nenda rudi.Sijakataa mtu kusherehekea siku yake ya kuzaliwa siku moja kati ya 365 lakini vipi masikini wanaoteseka siku zote 365 huku yule waliyemtuma wakitegemea atawaondolea umasikini akiponda raha (kiujumla maisha ya Rais kwa mshahara wake ni bonus tosha kwa siku zote 365 ukilinganisha na watanzania wengi ) lakini bado pia kabla hajatimiza azma za waliomtuma tayari anafanya karamu tena hali ya kuwa wale waliomtuma hawakumbuki hata siku zao za kuzaliwa kwa tabu na masumbuko ya umasikini wanaoupitia!

Wakuu nina mengi moyoni ila hasira zimenikaba kwenye koo mpaka nashindwa kuendelea. Naomba niishie hapa kwa Leo .
wasafifm~p~CZOrWONsefq~1.jpg
wasafifm~p~CZOrWONsefq~2.jpg
 
Hii inaitwa roho ya kwanini, sio kitu kizuri!. Mtu amelitumikia taifa kwa siku 364, hiyo siku moja tuu ya 365 ndio inakuuma?.

Tena sisi Tanzania tuna bahati, siku ya birthday ya mkuu wa nchi ni siku ya kawaida, wenzetu ikiwemo Uingereza, Birthday ya Queen ni public holiday!. Na sio UK pekee, ni Great Britain yote, na kwenye dominion zake site, Canada, Australia na Newsland.

Siku hiyo balozi zote za Uingereza dunia nzima zinaiadhimisha kwa tafrija mchapalo.

Nami nijiunge na Watanzania wenzangu kumtakia Happy Birthday President Mama Samia Suluhu Hassan.
P
 
Hii inaitwa roho ya kwanini, sio kitu kizuri!. Mtu amelitumikia taifa kwa siku 364, hiyo siku moja tuu ya 365 ndio inakuuma?.

Tena sisi Tanzania tuna bahati, siku ya birthday ya mkuu wa nchi ni siku ya kawaida...
Mkuu so unaonaje ingefanywa pubic holiday ili wote tufurahie?ongeza l panapostahili.Pili Hii picha ya shule gofu si ya kutengeneza kweli maana tulishamaliza ujenzi wa madarasa
 
Nilikuwa nakuheshim Sana kama,Kwa hili nimekudharau Sana, samahani.
Kama ulikuwa unaniheshimu, then ulikuwa na sababu. Kama heshima hiyo sasa umeiondoa tuu kwasababu tuu mimi nimeunga mkono birthday ya Mama Samia!, then asante sana kwa heshima yako, nasikitika sana, nitamiss heshima yako nitaathirika sana kuikosa heshima yako. Sina jinsi asante.
P
 
Back
Top Bottom