Aina nne za malezi na athari zake kwa watoto

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
3,858
2,000
Malezi ya watoto ni elimu muhimu yenye ukurasa unaojitengemea. Tumekuwa na kujifunza darasani maada nyingi na muhimu katika maisha yetu, bahati mbaya ni kuwa suala la malezi ya watoto, ambalo kwa kiasi kikubwa wengi wetu laazima tupitie hatua hii limekuwa likiachwa nyuma, na sasa mtazamo binafsi na uhalisia wa mazingira imebaki kuwa njia pekee tegemewa katika malezi na makuzi ya watoto walio wengi.

Namna unavyomlea au kuwalea watoto wako huweza kuathiri moja kwa moja wanavyochukulia mambo na wanavyojichukulia wao, hivyo ni muhimu kutilia maanani njia bora na sahihi inayomjengea motto msingi bora wa maisha yake ya baadae.
Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali juu ya malezi ya watoto, kuna aina kuu nne za malezi, na leo napenda kukushirikisha aina hizi nne na athari zake;

Malezi ya kimabavu.
Tafakari kidogo juu ya sentensi hizi.
• Unaamini watoto wanahitaji uangalizi tu, na si kusikilizwa.
• Unaamini watoto wafuate sheria zako, na si uhalisia uliopo.
• Hutilii maanani hisia za mtoto.

malezi ya kimabavu

Ikiwa katika sentensi hizo apo juu ni sawa kwako, basi aina yako ya malezi ni ya kimabavu. Wazazi katika aina hii ya malezi huamini watoto lazima wafuate sheria na maelekezo yote wanayopewa bila kupuuza wala kukaidi.

Wazazi wenye malezi ya kimabavu, huwaepusha watoto wao na mazingira au vikwazo vinavyowahitaji kutumia akili, badala yake wazazi huunda sheria na miongozo bila kujali mitazamo ya watoto.

Wazazi wenye malezi ya kimabavu, hupenda kusema “mimi nimesema” na inapotokea mtoto anauliza sababu zinazopelekea kupewa maelekezo husika na mzazi wake, mzazi huwa hayuko tayali kufanya mjadala, husisitiza kuheshimiwa tu, na utekelezaji wa alichokielekeza. Wazazi hutumia adhabu zaidi kuliko kuonya. Hivyo mtoto au watoto hawafundishwi njia za kuepuka makosa, bali wazazi huwafanya watoto wajutie makosa waliyoyafanya.

Athari za malezi ya kimabavu.
Watoto wanaokulia katika malezi ya kimabavu hufuata sheria na maelekezo wakati wote.
Pia watoto hawa hukabiliwa na tatizo la kutokujiamini.
Watoto katika aina hii ya malezi huweza kuwa wakatili na wasiojali hisia za wenzao. Tafiti zinaonesha kuwa watoto hawa huwa ni waongo wazuri, kwani wamekuwa wakiamini kusema uongo ili kuepuka adhabu.

Malezi ya mamlaka (demokrasia)
Tafakari kidogo juu ya sentensi hizi,
• Unatumia nguvu nyingi kujenga mahusiano mazuri na mtoto au watoto wako.
• Unaelezea sababu zinazopelekea sheria au maelekezo yako kwa watoto wako
• Unatilia maanani hisia za mtoto au watoto wako.

Ikiwa katika sentensi hizo apo juu ni sawa kwako, basi aina yako ya malezi ni ya mamlaka. Kama ilivyo kwa wazazi wenye malezi ya kimabavu, wazazi wenye malezi ya mamlaka huweka sheria na miongozo, lakini hutoa nafasi kwa watoto wao kujieleza na kuelezea mitazamo yao.

Wazazi wenye malezi ya mamlaka hutoa nafasi kwa watoto wao kukabiliana na changamoto za maisha, ili kuwajenga.
Pia hutoa maelekezo muhimu kuzuia tabia zisizokuwa nzuri na kusisitiza tabia zenye maadili mema. Hivyo wazazi hupongeza na kusifia tabia nzuri

Athari za malezi ya mamlaka
Watoto wanaokulia katika malezi ya mamlaka au demokrasia huwa wenye furaha na wenye mafanikio.
Pia watoto hawa huwa na uwezo mzuri wa kufanya maamzi sahihi na kutathmini athari ya maamzi yao.
Tafiti zinaonesha kuwa watoto waliolelewa na wazazi wenye malezi ya mamlaka wanapofikia umri wa watu wazima, huwa wawajibikaji na hujisikia huru kujieleza na kuelezea mawazo yao.

Malezi huru
Tafakari kidogo juu ya sentensi hizi,
• Unaweka sheria na maelekezo, lakini hutilii maanani utekelezwaji wake.
• Huwawajibishi watoto mara kwa mara kwa ukiukaji wa maelekezo na sheria.
• Unaamini mtoto atajifunza vizuri, bila ya kumfuatilia sana

Ikiwa katika sentensi hizo apo juu ni sawa kwako, basi una malezi huru. Wazazi wenye malezi huru ni wavumilivu, na hawawafuatilii watoto wao sana. Huingilia na kuonekana pale tu panapojitokeza tatizo kubwa dhidi ya watoto wao.

Wazazi hawa hawawajibishi watoto wao kwa wakati na ikitokea kuwawajibisha hufanya hivyo mara chache zaidi. Hutoa msamaha zaidi na huamini “mtoto ni mtoto tu” , wanapowawajibisha watoto mara nyingi hutoa msamaha pale mtoto anapoomba msamaha na kuahidi kubadili tabia.

Wazazi hawa huchukua nafasi na jukumu la rafiki zaidi kuliko nafasi na jukumu la mzazi. Huwashawishi watoto wazungumze matatizo yao, lakini hawafanyi juhudi kubwa kukemea tabia na maamzi yasiyo sahihi ya watoto wao. Hawakemei tabia nyingi mbovu za watoto wao.

Athari za malezi huru
Watoto wanaokulia katika malezi huru hujituma zaidi kitaaluma, ikiwa wana hulka hiyo.
Watoto hawa hukabiliwa na matatizo mengi ya kinidhamu kwa sababu hawaheshimu utawala wala sheria.
Mara nyingi watoto hawa hawajiamini na muda mwingi huwa ni wenye huzuni.

Watoto hawa huwa na deko lisilo la kawaida, na wazazi hujikuta taratibu wakianza kutumikishwa na watoto wao, bila kujua kuwa tayali wanatumikishwa.

Watoto hawa huwa katika hatari kubwa ya kukubwa na matatizo ya kiafya, hususani meno na tumbo, kwani wazazi hawana muda wa kuwasimamia watoto wao juu ya usafi wa kinywa, chakula na mwili kwa ujumla.

Malezi huria
Tafakari kidogo juu ya sentensi hizi,
• Hufuatilii maendeleo ya watoto wako kitaaluma na kazi zao za shule.
• Mara nyingi hujui wapi mtoto wako yupo na yupo na nani.
• Huna muda wa kukaa na watoto wako.

Ikiwa katika sentensi hizo apo juu ni sawa kwako, basi una malezi huria. Wazazi wenye malezi huria, kimsingi hutarajia watoto wajilee wao wenyewe.

Wazazi hawatumii nguvu nyingi kutafta mahitaji ya watoto wao. Wakati mwingine wazazi hawa, hawafahamu juu ya maendeleo ya watoto wao. Mara nyingi wazazi hawa hujikita kutatua shida nyingine tu kama vile kazi, kodi ya nyumba au pango, bili za umeme, maji, ving’amzi, na mahitaji mengine ya nyumbani.

Wazazi hawana ufahamu wa kutosha juu ya wanachofanya watoto wao. Wazazi huweka sheria na miongozo michache tu. Hakuna msisitizo wa kutosha katika kuwaelekeza watoto wao, kuwaongoza na kuwajali.

Athari za malezi huria
Watoto waliokulia katika malezi huria, huwa hawana ufaulu mzuri darasani, wala hawajiamini.

Watoto hawa hukumbwa na matatizo mengi ya kinidhamu na huwa hawana furaha.

Hitimisho
Wakati mwingine wazazi hawawezi kuwa katika aina moja ya malezi kikamilifu, wengi huchanganya, lakini ni vizuri zaidi kuwa mzazi mwenye malezi ya mamlaka au demokrasia.

Ukiamua kujitoa na kudhamilia kuwa mzazi bora anayefaa, basi ni vizuri kujenga mahusiano mazuri na mtoto au watoto wako, wakati huo huo ujenge mamlaka yako kwa watoto wako kikamilifu kwa njia ambayo ni rafiki katika makuzi na maendeleo yao, ili baadae watoto wavune matunda ya malezi yako katika maisha yao.
 
miles45

JF-Expert Member
Jan 4, 2019
617
1,000
Nyie mbona mmelelewa kwa fimbo nyingi na leo mmekua maprofesa, mainjinia, madoctor nk.

Yaani malezi ya baba kasema moja mbili tatu full stop.

Leo mmekua mmeanza kuhubiri sijui mtoto asikilizwe cha ajabu hao hao watoto wanao sikilizwa leo ni madishi ile mbaya no heshima nk.

Kifupi tuviache vitu viwe vilivyo nature ndio itaamua. But do your best.
 
TheChoji

JF-Expert Member
Apr 14, 2009
3,243
2,000
Nyie mbona mmelelewa kwa fimbo nyingi na leo mmekua maprofesa ,mainjinia,madoctor nk.

Yaani malezi ya baba kasema moja mbili tatu full stop.

Leo mmekua mmeanza kuhubiri sijui mtoto asikilizwe cha ajabu hao hao watoto wanao sikilizwa leo ni madishi ile mbaya no heshima nk.

Kifupi tuviache vitu viwe vilivyo nature ndio itaamua. But do your best.

"Hard times create strong men, strong men create good times, good times create weak men and weak men create hard times.”
 
Ushindi victory

JF-Expert Member
Dec 11, 2018
384
1,000
Hizo demokrasia na uhuru ni mambo ya watu wa magharib na nduguzo wengne white men,,kiafrika,narudia tena kiafrika, mtoto anpaswa kulelewa malezi y half dictatorship, yaan hak kidooogo ubabe mwingi,,moja ya madhara ya ukolon baran afrika ni pamoja na maadir, yaan hawa watu walfanikiwa kutufanya tuige mifumo tao ya malez kwa watoto,jambo lililopelekea kuja kuibuka kwa tabia za ajabu, vizaz vya watot wenye tabia za ajabu,.mfano viburi,uhuni,kukosa heshima,uvivu,lugha mbaya, heshma mbovu kwa mwenza, heshima mbovu kwa wazaz wa mwenza,,mahusiano ya kifamilia kuporomoka, mahusiano ya kimapenz kukosa mvuto na kuarbika mapema,, kuna faida za kuwa na malez ya diplomasia lkn hasara ni nyingi kulko,

Sasa fuatilia hata kwa makjni utofaut wa watoto wa kizaz kile ambao ni babu zetu, na vizaz vya sasa nazan unaona utofaut mkubwa sana,sasa haya ndyo madhara ya uhuru wakipuuz, mtu unazan kumpa Uhuru mtoto ndyo kumpenda kumbe wamwarbu,,,turud kwenye uharisia wa maisha ya kiafrika, uzungu na utandawaz utawapoteza ndugu achen kuiga iga,,mwafrika ana namna yake ya kuish na kushirikiana na jamii tofaut na mataifa mengine,,hivyo bas unapoharbu miiko ya uafrika, lazma tu uzalishe bomu la machoz ambalo ndyo vizaz vya akina jems delicious, ambalulu,ambaruti,.watot wasiosikia wazaz, watot wanaojiamulia maamuz batir bila kuhofia mzaz,.
 
Apollo one spaceship

Senior Member
Jan 28, 2021
102
225
hizo demokrasia na uhuru ni mambo ya watu wa magharib na nduguzo wengne white men,,kiafrika,narudia tena kiafrika, mtoto anpaswa kulelewa malezi y half dictatorship, yaan hak kidooogo ubabe mwingi,,moja ya madhara ya ukolon baran afrika ni pamoja na maadir, yaan hawa watu walfanikiwa kutufanya tuige mifumo tao ya malez kwa watoto,jambo lililopelekea kuja kuibuka kwa tabia za
Kuna shule siku hizi.Watoto walioenda shule huwezi kuwalea kwa njia za kiafrka za zamani.Hii n nature mpya.Lazima kuwe na njia ya kuweka mambo yaende vizuri.
 
Omusolopogasi

JF-Expert Member
Aug 31, 2017
5,514
2,000
Mi ni profesa lkn ukinisimamisha mbele ya watu, tena wanaoongea Kiingereza huwa moyo unadunda sana. Dingi yangu ni kama huyo hapo kwenye picha...
Nyie mbona mmelelewa kwa fimbo nyingi na leo mmekua maprofesa, mainjinia, madoctor nk.

Yaani malezi ya baba kasema moja mbili tatu full stop.

Leo mmekua mmeanza kuhubiri sijui mtoto asikilizwe cha ajabu hao hao watoto wanao sikilizwa leo ni madishi ile mbaya no heshima nk.

Kifupi tuviache vitu viwe vilivyo nature ndio itaamua. But do your best.
 
MUREFU

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
1,328
1,500
Malezi ya watoto ni elimu muhimu yenye ukurasa unaojitengemea. Tumekuwa na kujifunza darasani maada nyingi na muhimu katika maisha yetu, bahati mbaya ni kuwa suala la malezi ya watoto, ambalo kwa kiasi kikubwa wengi wetu laazima tupitie hatua hii limekuwa likiachwa nyuma, na sasa mtazamo binafsi na uhalisia wa mazingira imebaki kuwa njia pekee tegemewa katika malezi na makuzi ya watoto walio wengi.

Namna unavyomlea au kuwalea watoto wako huweza kuathiri moja kwa moja wanavyochukulia mambo na wanavyojichukulia wao, hivyo ni muhimu kutilia maanani njia bora na sahihi inayomjengea motto msingi bora wa maisha yake ya baadae.
Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali juu ya malezi ya watoto, kuna aina kuu nne za malezi, na leo napenda kukushirikisha aina hizi nne na athari zake;

Malezi ya kimabavu.
Tafakari kidogo juu ya sentensi hizi.
• Unaamini watoto wanahitaji uangalizi tu, na si kusikilizwa.
• Unaamini watoto wafuate sheria zako, na si uhalisia uliopo.
• Hutilii maanani hisia za mtoto.

malezi ya kimabavu

Ikiwa katika sentensi hizo apo juu ni sawa kwako, basi aina yako ya malezi ni ya kimabavu. Wazazi katika aina hii ya malezi huamini watoto lazima wafuate sheria na maelekezo yote wanayopewa bila kupuuza wala kukaidi.

Wazazi wenye malezi ya kimabavu, huwaepusha watoto wao na mazingira au vikwazo vinavyowahitaji kutumia akili, badala yake wazazi huunda sheria na miongozo bila kujali mitazamo ya watoto.

Wazazi wenye malezi ya kimabavu, hupenda kusema “mimi nimesema” na inapotokea mtoto anauliza sababu zinazopelekea kupewa maelekezo husika na mzazi wake, mzazi huwa hayuko tayali kufanya mjadala, husisitiza kuheshimiwa tu, na utekelezaji wa alichokielekeza. Wazazi hutumia adhabu zaidi kuliko kuonya. Hivyo mtoto au watoto hawafundishwi njia za kuepuka makosa, bali wazazi huwafanya watoto wajutie makosa waliyoyafanya.

Athari za malezi ya kimabavu.
Watoto wanaokulia katika malezi ya kimabavu hufuata sheria na maelekezo wakati wote.
Pia watoto hawa hukabiliwa na tatizo la kutokujiamini.
Watoto katika aina hii ya malezi huweza kuwa wakatili na wasiojali hisia za wenzao. Tafiti zinaonesha kuwa watoto hawa huwa ni waongo wazuri, kwani wamekuwa wakiamini kusema uongo ili kuepuka adhabu.

Malezi ya mamlaka (demokrasia)
Tafakari kidogo juu ya sentensi hizi,
• Unatumia nguvu nyingi kujenga mahusiano mazuri na mtoto au watoto wako.
• Unaelezea sababu zinazopelekea sheria au maelekezo yako kwa watoto wako
• Unatilia maanani hisia za mtoto au watoto wako.

Ikiwa katika sentensi hizo apo juu ni sawa kwako, basi aina yako ya malezi ni ya mamlaka. Kama ilivyo kwa wazazi wenye malezi ya kimabavu, wazazi wenye malezi ya mamlaka huweka sheria na miongozo, lakini hutoa nafasi kwa watoto wao kujieleza na kuelezea mitazamo yao.

Wazazi wenye malezi ya mamlaka hutoa nafasi kwa watoto wao kukabiliana na changamoto za maisha, ili kuwajenga.
Pia hutoa maelekezo muhimu kuzuia tabia zisizokuwa nzuri na kusisitiza tabia zenye maadili mema. Hivyo wazazi hupongeza na kusifia tabia nzuri

Athari za malezi ya mamlaka
Watoto wanaokulia katika malezi ya mamlaka au demokrasia huwa wenye furaha na wenye mafanikio.
Pia watoto hawa huwa na uwezo mzuri wa kufanya maamzi sahihi na kutathmini athari ya maamzi yao.
Tafiti zinaonesha kuwa watoto waliolelewa na wazazi wenye malezi ya mamlaka wanapofikia umri wa watu wazima, huwa wawajibikaji na hujisikia huru kujieleza na kuelezea mawazo yao.

Malezi huru
Tafakari kidogo juu ya sentensi hizi,
• Unaweka sheria na maelekezo, lakini hutilii maanani utekelezwaji wake.
• Huwawajibishi watoto mara kwa mara kwa ukiukaji wa maelekezo na sheria.
• Unaamini mtoto atajifunza vizuri, bila ya kumfuatilia sana

Ikiwa katika sentensi hizo apo juu ni sawa kwako, basi una malezi huru. Wazazi wenye malezi huru ni wavumilivu, na hawawafuatilii watoto wao sana. Huingilia na kuonekana pale tu panapojitokeza tatizo kubwa dhidi ya watoto wao.

Wazazi hawa hawawajibishi watoto wao kwa wakati na ikitokea kuwawajibisha hufanya hivyo mara chache zaidi. Hutoa msamaha zaidi na huamini “mtoto ni mtoto tu” , wanapowawajibisha watoto mara nyingi hutoa msamaha pale mtoto anapoomba msamaha na kuahidi kubadili tabia.

Wazazi hawa huchukua nafasi na jukumu la rafiki zaidi kuliko nafasi na jukumu la mzazi. Huwashawishi watoto wazungumze matatizo yao, lakini hawafanyi juhudi kubwa kukemea tabia na maamzi yasiyo sahihi ya watoto wao. Hawakemei tabia nyingi mbovu za watoto wao.

Athari za malezi huru
Watoto wanaokulia katika malezi huru hujituma zaidi kitaaluma, ikiwa wana hulka hiyo.
Watoto hawa hukabiliwa na matatizo mengi ya kinidhamu kwa sababu hawaheshimu utawala wala sheria.
Mara nyingi watoto hawa hawajiamini na muda mwingi huwa ni wenye huzuni.

Watoto hawa huwa na deko lisilo la kawaida, na wazazi hujikuta taratibu wakianza kutumikishwa na watoto wao, bila kujua kuwa tayali wanatumikishwa.

Watoto hawa huwa katika hatari kubwa ya kukubwa na matatizo ya kiafya, hususani meno na tumbo, kwani wazazi hawana muda wa kuwasimamia watoto wao juu ya usafi wa kinywa, chakula na mwili kwa ujumla.

Malezi huria
Tafakari kidogo juu ya sentensi hizi,
• Hufuatilii maendeleo ya watoto wako kitaaluma na kazi zao za shule.
• Mara nyingi hujui wapi mtoto wako yupo na yupo na nani.
• Huna muda wa kukaa na watoto wako.

Ikiwa katika sentensi hizo apo juu ni sawa kwako, basi una malezi huria. Wazazi wenye malezi huria, kimsingi hutarajia watoto wajilee wao wenyewe.

Wazazi hawatumii nguvu nyingi kutafta mahitaji ya watoto wao. Wakati mwingine wazazi hawa, hawafahamu juu ya maendeleo ya watoto wao. Mara nyingi wazazi hawa hujikita kutatua shida nyingine tu kama vile kazi, kodi ya nyumba au pango, bili za umeme, maji, ving’amzi, na mahitaji mengine ya nyumbani.

Wazazi hawana ufahamu wa kutosha juu ya wanachofanya watoto wao. Wazazi huweka sheria na miongozo michache tu. Hakuna msisitizo wa kutosha katika kuwaelekeza watoto wao, kuwaongoza na kuwajali.

Athari za malezi huria
Watoto waliokulia katika malezi huria, huwa hawana ufaulu mzuri darasani, wala hawajiamini.

Watoto hawa hukumbwa na matatizo mengi ya kinidhamu na huwa hawana furaha.

Hitimisho
Wakati mwingine wazazi hawawezi kuwa katika aina moja ya malezi kikamilifu, wengi huchanganya, lakini ni vizuri zaidi kuwa mzazi mwenye malezi ya mamlaka au demokrasia.

Ukiamua kujitoa na kudhamilia kuwa mzazi bora anayefaa, basi ni vizuri kujenga mahusiano mazuri na mtoto au watoto wako, wakati huo huo ujenge mamlaka yako kwa watoto wako kikamilifu kwa njia ambayo ni rafiki katika makuzi na maendeleo yao, ili baadae watoto wavune matunda ya malezi yako katika maisha yao.

Aisee nimeelewa sana
 
Fall Army Worm

JF-Expert Member
Jan 8, 2015
13,168

Maisha ni fumbo Sana.Kwa kweli hamna njia moja iliyosahihi ya kumlea mtoto, nadhani itategemea mazingira.

Sent from my Infinix X688C using JamiiForums mobile app
 
cool d

JF-Expert Member
Jan 20, 2015
1,069
2,000
Hizo demokrasia na uhuru ni mambo ya watu wa magharib na nduguzo wengne white men,,kiafrika,narudia tena kiafrika, mtoto anpaswa kulelewa malezi y half dictatorship, yaan hak kidooogo ubabe mwingi,,moja ya madhara ya ukolon baran afrika ni pamoja na maadir, yaan hawa watu walfanikiwa kutufanya tuige mifumo tao ya malez kwa watoto,jambo lililopelekea kuja kuibuka kwa tabia za ajabu, vizaz vya wa
Siyo kama unavyofikiri, hao babu zetu walilelewa na Mama muda mwingi huku wakielekezwa wanapokosea ila sasa watoto wanalelewa na house keepers tena kwa kubadilishwa kila mara na hakuna wakuangalia matendo ya mtoto hivyo watoto ndo tumekuwa hivi, hiyo demokirasia ni mambo ya kisiasa wala familia haiwezi kufanya hivyo.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom