Aina mpya ya utapeli

Hahahahaha walai nacheka kama mazuri,
Jamani eeh tukubali tukatae huwezi kutapeliwa kama huna Tamaa, wengi husema Matapeli wanatumia dawa, jibu ni HAPANA, Matapeli wanakutapeli kwa tamaa yako yaan wao hukutia tamaa ukitamani tu wanakuchinjia baharini,

Hao washenzi walishakuja dukani kwangu mara ya mwanzo walimkuta binti, wakamjaza kwa kudai kua rangi nyekundu niliyopaka sio ya biashara, nakosa wateja wanaostahili sababu ya rangi, basi sijui walimwambia na mengine yapi binti ananipigia simu kahamanika anataka nibadili rangi haraka nikamwambia atulize pupa kwanza sina pesa za kuchezea akasema eti nikate kwenye pesa yangu hapo nikahisi binti amechanganyikiwa nikamtuliza akatulia,

Sasa siku hiyo nakumbuka ilikua jumamosi nimekaa zangu dukani na ndugu yangu tunasogoa akaja libaba refu jeusi akajiulizisha kitu nikawa sina akadai alimuagiza binti amuwekee nikamwambia sijapata hiyo order, akaanza, "wewe ndie mmiliki wa hili duka?? Hii rangi unaijua maana yake??? Hiyo ni rangi hutumiwa na waganga na wachawi, hupati wateja unaostahili sababu tu ya rangi, nimeona shetani nani sijui ametawala dukani kwako...." Akaongea blah blah kibaoooooo mwisho wa siku akadai anipe dawa ya kudekia saa 11 alfajiri, nitashangaa wateja watakavyokuja, nikamuuliza bei gani hiyo dawa akasema elfu 2 tu ila majibu yatakavyotokea nitajua mwenyewe nimpongeze kiasi gani,

Tangu mwanzo nilishanusa harufu ya utapeli nikamwambia aache namba nitampigia, akaanza kulazimisha ooh nakusaidia, ooh fikiria nimeacha maduka mangapi hadi nimekuja kwako, mimi nakupa dawa uwe tajiri, hapo nikajiaminisha kua huyu kama sio Tapeli basi Jambazi kabisaaaaaa,

Nikamwambia atoke haraka kabla sijamuitia mwizi, akaondoka ila nikasikia kuna Mmama alifilisiwa na huyo huyo jamaa.
Note: kwenye maisha ukishaona mtu humjui wala hamfamiani anaanza habari za kukupa mchongo jua wewe ndo mchongo mwenyewe.
 
Huyo jamaa yako tamaa ndio imemponza alitakiwa awe na msimamo kwamba hatumii dawa yoyote hivyo asingekubali kuchukua chochote na kwenda kukifanyia kazi sijui kujaribu lakini alivyokubali tu ikawa biashara imeisha.
Angefanikiwa isingeitwa tamaa bali mngesema mafanikio yana siri kubwa.
Leo hii wengi uona nyuma ya utajiri wa matajiri wengi kuna ushirikna au dhuruma.
 
Dah matapeli sio watu poa asee walinifanya aiku moja nijipige makofi ya uso hadi nikavimba, kiufupi hawa jamaa ukitaka uwaweze dhibiti tamaa ya vitu vya bei juu kwa bei rahisi na tamaa ya pesa nyingi za haraka.
 
  • Thanks
Reactions: _ID
Naiandika huku hii mada baada ya kuona huku Kuna watu wengi na elimu itawafikia wengi kuliko kwenye majukwaa mengine.

Ipo hivi Kuna jirani yangu anabiashara yake inayo muweka mjini na kumfanya avimbe hapa mjini.

Basi Kuna siku akiwa officin kwake akaja mtu na kumuomba waongee huyu bro hakua na hiyana wakatoka nje ya office , yule mtu akamuambia kitu chenyewe ni Cha Siri kidogo tunaweza toka hapa na kwenda sehemu yoyote uipendayo tuongee vizuri.....? Huyu bro kwakua alipewa chance ya kuchagua sehem aipendayo Basi hakua na hofu na huyo jamaa.

Basi wakaenda sehemu wakakaaa na kunza mazungumzo.....yule jamaa akanza na kumuomba msamaha kwa kumpotezea muda wake na kujitambulisha kuwa yeye ni mganga na anadawa ya kuongeza wateja kwenye duka lake ......huyu bro akastuka kidogo na kumuambia kuwa mbona Mimi situmii hayo Mambo ...? Jamaa akamjibu usijari ni mambo ya kawaida kabisa na Wala hayahitaji mambo mengi.... Akatoa kipande Cha mzizi chenye urefu Kama futi moja na nusi ila kimegawika kimapingili kama vile mua.

Akamuambia dawa yenyewe ni hii hapa Wala haiitaji mambo mengi .... Unachukua tu hiki kipande unaloweka kwenye maji ya kudekia tu Kisha unadeki duka lako na kukirudisha sehemu salama na Yale maji ulio Delia pia unamwaga nje mbele ya duka lako Basi hivyo tu wateja utajionea mwenyewe.......na kuambiwa ile mzizi wote unauzwa million nne ila kwa Leo anammegea kipande tu Cha kwenda kufanyia majaribio akipata majibu amtafute kwa namba hizi. Basi akampa kile kipande na kuagana na kila mtu kuendelea na mishe zake .

Bro kwa kua hakupigwa pesa zozote aliamini kuwa huyu mtu anaweza akawa mkweli .

Basi siku ya pili yake bro akafanya Kama alivyo agizwa huku akiwahi ofisini kwake mapema zaidi ya wafanyakazi na wake na kudeki Kama alivyo agizwa... Siku ya kwanza wafanyakazi walishangaa Sana na kuhusi watafukuzwa kazi....

Basi kumbe yule jamaa anagenge lake huku nyuma kumbe Kuna mtu spesho kwa ajili ya kuangalia Kama wamedekea ile dawa kwa kuangalia unyevu wa maji mlangoni.

Basi walivyo ona ameanza kudekia wale matapeli wakaanza kwenda kununua vitu kwa fujo dukani kwa bro kiufupi ni watu wenye mitaji mikubwa Hawa mbwa wakikuundia tume huchomoki. Siku ya kwanza bro alikusanya mauzo Mara tatu ya mauzo ya kawaida, siku ya pili akipata mauzu Mara tano , siku ya nne yakawa Mara tano na kidogo ..........Hadi siku ya Saba ambayo aliambiwa muda wa majaribio hapa yalikua mauzo Mara 11 .....bro akadata na kuona kile kitu ni ukweli kumbe Basi akaenda kukopa bank ili achukue mzigo mkubwa zaidi akafanikiwa kwenda kuchukua mzigo huo na kuuweka standby dukani na kuwatafuta wale matapeli akawapigia simu na wakakutana Kama kawaida ....ila Cha ajabu wakamuambia kuwa ile dawa ya milioni nne imeisha imebaki ya milioni nane na hairuhusiwi kumegwa vipande inatakiwa yote ikatumike sehemu moja Kama duka moja tu . Kama Hana hela asubiri Hadi watakapo enda kuchukua nyingine hizo za milioni nne.

Bro akapiga hesabu na kuona Hadi waende wakachukue nyingine muda utakua mrefu zaidi ...Basi akaenda akachukua milioni 8 na kueakabidhi na kupewa hilo limzizi kwa ajiri ya kwenda kupigia pesa

Akaenda akadekia Kama kawaida ila Cha ajabu wale wateja wanunua kwa vurugu hawakutokea wakabaki wateja wa kawaida tu siku ya kwanza .....siku ya pili.....wiki......mwezi .....miezi......holaaa....na mzigo hautoki dukani na benki Kama kawaida ila anaendelea kusubiri Chao

NB
Ndugu zanguni usione watu benk zinauza nyumba zao ukazani wote ni wazembe ,au walikopa pesa wakala au walihonga ....hii dunia iacheni tu ....Muda wowote unaweza ukawa masikini wa kutupwa au tajiri wa kufa mtu.

Tusichoke kumuomba Mwwnyezi Mungu kutuepusha na majaribu.
iko hivi ukisika mganga anataka million jua uyo mwizi mganga wa kweli bei zao ni km mafundi saa 2000 au 5000 basi
 
huyo naye mshamba kama washamba wengine.

Kama mtu ana huo ujanja kwanini asifungue biashara yake apige pesa hadi akuletee wewe. Hujiulizi ni kwa huruma gani.

Lakini huo utapeli niliusikia kwa mara ya kwanza mwaka 1984. Ulifanywa kwa mafanikio kiasi cha mwenye duka kupata kichaa.

So hakuna jipya chini ya jua.
 
Huyu jamaa atakuwa alikuwa na biashara ndogo kiasi kwamba jamaa walimmudu kununua na kuongeza mauzo.
 
Back
Top Bottom