Aina Hii ya Wizi wa magari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Aina Hii ya Wizi wa magari

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Yona F. Maro, Jan 28, 2010.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Jan 28, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu niko maeneo ya katikati ya jiji la DSM asubuhi hii tulipaki gari yetu Mtaa wa Jamhuri kwa dakika kama 40 hivi , tuliporudi tena tulikuta gari yetu imebadilishwa namba na pembeni yake ilipaki gari inayofanana na hiyo hiyo , Tukaamua kufikisha suala hili katika vyombo vya dola ila iligundulika kwamba kuna kikundi cha watu wezi wa magari wanafanya shuguli hiyo kwa kushirikiana na wenye breakdown maana yake ile gari baada ya muda inakuja kubebwa na breakdown na kupelekwa mafichoni .

  Kwahiyo ndugu zangu muwe makini sana na aina hii mimi naiita mpya kabisa sijawahi kuona namba za gari kubadilishwa kwa muda mfupi hivi kama hili lililotokea asubuhi ya leo ,Imenishangaza sana kwa kweli
   
 2. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #2
  Jan 28, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  pole sana!

  Qn. hilo gari lenu mlilipata?
   
 3. Obi

  Obi JF-Expert Member

  #3
  Jan 28, 2010
  Joined: Jul 6, 2009
  Messages: 376
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Pole sana ndugu kwa masahibu yaliyokupata. Wizi Tanzania umekithiri sana dola na wadau wa ulinzi Tanzania inabidi wawe makini sana kudhibiti hali hii isiendelee
   
 4. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #4
  Jan 28, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,426
  Likes Received: 22,345
  Trophy Points: 280
  Hali ya sasa ni mbaya mno.
  Kila siku wezi wanagundua mbinu mpya wakati jeshi letu la polisi limekaria yare mafunzo ya kigeshi ya mwaka sherashini na mbiri
   
 5. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #5
  Jan 28, 2010
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  pole kwa matatizo ilaumu serikali yako kwa kukumbatia viongozi wasanii.
   
 6. O

  Omumura JF-Expert Member

  #6
  Jan 28, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Walaumu na wadanganyika kwa kuikumbatia CCM.
   
 7. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #7
  Jan 28, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Tatizo geshi la polisi limezidi usanii na kupenda camera, ukiona kwenye taarifa za habari jinsi kikosi maalumu cha Afande (-) anavyoendesha msako wake huko ukerewe, utatamani kucheka!!

  Watu wamevamia kisiwa almost wiki 2 zimepita, leo wanafanya msako na helkopta!! Na wakibahatika kukamata wazururaji na vibaka mjini, basi wanaitisha mkutano na vyombo vya habari kwamba 'geshi la polisi limejidhatiti kukabiliana na majambazi'!!

  Wenye akili wanaona usanii huu. Polisi acheni kuhukumu watu, kabla mahakama haijaamua kama watuhumiwa ni majambazi ama la!!!!!!!
   
 8. Kwetunikwetu

  Kwetunikwetu JF-Expert Member

  #8
  Jan 28, 2010
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 1,544
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  duh bongo balaa...!
   
 9. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #9
  Jan 28, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Jaribu hii,

  [​IMG]

  au hii
  [​IMG]

  wakati mwingine tumia hii:
  [​IMG]

  wasipoelewa fanya hivi:
  [​IMG]
   
 10. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #10
  Jan 28, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 689
  Trophy Points: 280
  Duh! lakini bongo watu wamezidi kula raha kwenye mausafiri ya hatari!--japo kenya nao wamo balaa!!

  Kama una more than 30m car, kwa nn usiweke Car track tu yaishe?
  Au kama vipi vuta corola family ya 1988, imenyooka kama rula. nani ataiba hiyo.
   
 11. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #11
  Jan 28, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,426
  Likes Received: 22,345
  Trophy Points: 280
  Nimezipenda sana hizi mbinu.
  Ziko very much advanced.
   
 12. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #12
  Jan 28, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Tatizo ni kwamba tofauti ya haves na have nots ni kubwa sana, sasa kila mtu anajitahidi kusurvive. Kwa sasa ni kama tuko porini vile yaani simba akiamka anaomba mungu ili awe na mbio na nguvu kuliko nyati ili amkamate amle. Na nyati akiamka asubuhi anasali ili awe na mbio kuliko simba ili asishikwe na kuliwa na simba.

  Na sisi vivi hivi, kila mtu anaamka asubuhi na sala yake, wezi ( ambao ni majority) white collar, black collar, whichever colour wanaomba ili waibe watoto wale na waende shule. Wakati huo huo upande unaoibiwa unajitahidi kusali ili wasiibiwe na wezi.

  Kupunguza adha hii tujaribu kugawana resources zetu angalau fairly sio lazima sawa utaona wizi unapungua, watu wanaiba kwa sababu wanahitaji kula, kusomesha, kujenga, kutunza wazazi wao nakadhalika. Wanaofanya kazi halali ya kuuza maembe na madafu wanapigwa na mgambo wa jiji kuliko wezi wanavyopigwa na askari.

  Unategemea hao watafanyaje????

  Bujubuji, mbombo ngafu fijo.
   
Loading...