Aina hii ya Riziki kwa sasa imekuwa ngumu kidogo kwa watu wengi

GuDume

JF-Expert Member
Jan 18, 2015
6,652
14,247
Kuna aina tatu za Riziki. Naomba nizielezee kwa kifupi sana nikilinganisha na aina ya maisha tuliyo nayo.

1. Riziki KITAKO
Hii ni Riziki ambayo mpataji anategesha tu michongo yake pesa zinakuja au deals zinakuja. Anapigiwa simu na watu mbalimbali wakimtaka wakapige deals za kupata pesa. Awamu ya Nne hii Riziki ilikuwepo sana. Mtu anaweza toka home asubuh ana mafuta ya kwendea tu town.akaenda kijiweni akafanya michongo akapata mafuta ya week nzima na pesa ya kung'olea mademu wakali. Kwa sasa aina hii ya Riziki imekuwa nadra sana kupatikana.sisemi haipo ila nasema imekuwa na kaugumu flani kwa wengi.

2. Riziki MANTASHALLAH
Hii ni Riziki ambayo wanaipata watu wa ofisini. Inapatikana kwa kuandika andika sana na kusoma. Muda mwingi inatumika akili na maarifa. Hata matapeli pia hutumia hii. Inahitaji ushawishi mkubwa, maarifa na ujuvi. Hii inawahusu sana watu wanaotumia kalamu na maneno kama njia mojawapo ya kupata pesa.

3. Riziki GUJURUBIH
Hii ni Riziki inayopatikana kwa kutumia nguvu sana. Kubeba mizigo, kuponda kokoto, kulima kwa jembe la mkono n.k manual works. Inahitajika sana msuli na kutoa jasho. Na mara nyingi wafanyaji wa kazi hizi huwa wanaenda tumia pesa zao na wadada wanaopata RIZIKI KITAKO. yaani mdada mmoja mzuri anajua tu kuwa ana KITEGA UCHUMI. basi anategeshea na mwanaume huyu anapeleka makusanyo yake ya siku,week au mwezi.

Awamu hii kuna aina ya Riziki zimeshika hatamu na nyingine zimedhoofu kiasi au kabisa.

Imefahamika kuwa hata LAKHI NAYO NI PESA. kwa wadada wengi wamejikuta Riziki KITAKO hailipi sana wanaume waliokuwa wanapata Riziki Kitako wamepungua. Riziki Mantashallah nayo imeingia kwenye ukakasi kiasi flani na hivyo kuwa shida zaidi kwa wahusika kukunjua sana mikono.
 
Riziki mantaadunda= hii riziki lazima udunde dunde ndo uipate kwa mfano madalalli wa vyumba lazima watembee wakidunda kupeleka wateja kwenye vyumba vya kupangisha,na tozo zao kama zifuatavyo
1.nauli ya dalali 5000
2,vocha kuongea na mmilliki wa nyumba 5000
 
Back
Top Bottom