Aina 10 za wanandoa

Aina 10 za wanandoa

The redemeer

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2025
Posts
4,780
Reaction score
8,155
1. KUMBIKUMBI
Hawa huongozana kila mahali. Yaani wanapendana hadi mahasidi wanatamani wanywe maji ya betri.

2. WAPAMBANAO
Hawa muda wote hupambana , hubishana na kurushiana maneno na kukosoana utasema wanaachana kesho ila huwa wanapendana , hawaachani ng'o.

3.WAZAZI WENZA
Hawa kwa asilimia kubwa huwa wapo kwa ajili ya watoto au wapo kufurahisha ndugu na wazazi. Moyoni walishaachana ila nje wanaonekana pamoja kusogeza siku watoto wakue.

4. WASITAO
Hawa ni kama hawana uhakika na ndoa yao na hawapendi kabisa kujulikana kama ni mke na mume labda ikilazimu sana. Wanaweza kuwa na miaka mingi kwenye ndoa ila wanaishi kama bado wanachunguzana.

5.VING'ANG'ANIZI
Wanajijua kabisa hawapendani ila wanatumia nguvu nyingi kuhakikisha wanaendelea kuwa pamoja kwani kila mmoja yupo kwenye ndoa kimkakati na kimaslahi. Hawa huwa hawaamini kama kuna upendo wa kweli na kama watu wanaweza kuishi kama marafiki. Wakiona watu wanapendana wanahisi kuna limbwata limetumika na wao wenyewe wanakuwaga washirikina.

6. WAIGIZAJI
Hawa huwa maadui wakubwa wawapo nyumbani lakini wakiwa mbele za watu hujifanya wanapendana.

7. UPANDE MMOJA
Hawa unakuta mmoja ndiye anaendesha ndoa kwa kila kila jambo yeye ndiye anaamua kila kitu na mwenzake hukaa tu kama msukule na kukubaliana na kila lisemwalo ili kuepusha shari japo moyoni huwa hampendi wala kumkubali mwenzi wake.

8.WANAHURIA
Yaani kila mtu anaishi kivyake ni kupeana tu taarifa leo nasafiri au jana nimenunua kiwanja yaani ni taarifa tu . Kila mtu ana mapato yake na matumizi yake na hakuna mipango ya pamoja.

9. WACHAMUNGU
Hawa wana hofu ya Mungu. Wanaishi kwa malengo na wanamtegemea Mungu na kufanya maombi pamoja na maamuzi yote yanatokana na imani yao.

10. WADAU
Hawa huishi kama wadau wa kibiashara na ndoa huendeshwa kama taasisi au mradi fulani. Mambo yanaenda kwa mpangilio, heshima ipo, maendeleo yapo ila ndoa haina mashamsham wala upendo kila mtu ana siri zake moyoni na mambo yake ya kisirisiri.
 
Kusema kweli ndoa zina mambo ya ajabu wajuba. Zipo ndoa wanaishi pamoja kwa amani na upendo hakuna magomvi ila kila mwanandoa ruksa kufanya majamboz nje ya ndoa bila kuoneana wivu, mpaka huzaa nje ya ndoa lakini hawatengani na kuachana
 
Wanahuria nimeshuhudia kwa jirani mke ana mpa taarifa mume mimi naenda bar toka umekula uko na mume nae ivyo ivyo
 
Back
Top Bottom