Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,921
- 30,265
Nimefika Chuo Kikuu Cha Iowa, Iowa City nyakati za mchana nikitokea Detroit ambako ndiko nilikoingia Marekani nikitokea Amsterdam.
Kutoka Detroit nimepanda ndege ndogo hadi Iowa City na hapo nikachukua taxi hadi University of Iowa.
Nimepewa mwaliko na Prof. James Giblin.
Chuo kina hoteli yake ya kufikia wageni.
Muda si muda simu ya chumbani kwangu inalia.
Prof. Giblin huyo.
Anasema Kiswahili utadhani kazaliwa Kariakoo.
"Mzee wa Tanga nasikia umewasili nitakuja kukuchukua jioni uje nyumbani tule."
Prof. Giblin mkewe Mtanzania.
Dada yangu kafurahi kuniona kwake na yeye pia anasomesha.
Stori zikawa za Dar es Salaam Kariakoo yake na Bi. Kidude na taarab ya Zanzibar.
Wamarekani wanapojifunza somo mfano lugha ya Kiswahili hawaingii nusu nusu utashangaa.
Wanaingia kusoma kila kitu hadi muziki na utamaduni.
Nimepigwa na butwaa nilipokuwa hapo chuoni wale wenye kusema Kiswahili hawazungumzi na mimi ila kwa Kiswahili na kuniuliza mengi ya sehemu wanazozijua Tanzania.
Chuo Kikuu Cha Iowa Idara ya African History imeandaa kongamano kuhusu historia ya Afrika na wataalamu wengi wamealikwa.
Baadhi ya waalikwa tunafahamiana tumeonana Tanzania miaka ya nyuma kama Jonathon Glassman na James Brennan.
Hawa ni mtu na mwanafunzi wake.
James Brennan kapiga goti kwa Jonathon Glassman kusoma shahada ya uzamivu na ndiye aliyemwagiza aje kuzungumza na mimi Tanga wakati wa utafiti wake.
Ilikuwa hapo University of Iowa ndipo nilipokutana na Aili Tripp.
Alinikabili na kunieleza kuwa alikuwa na hamu kubwa ya kuzungumza na mimi kwani yeye baba yake alikuwa akisomesha Chuo Kikuu Cha Dar-es-Salaam na akijuana na Ally Sykes akienda kumtembelea kwake Mbezi Beach.
Akaniambia yeye kasoma Bunge Primary School darasa moja na Mariam Abdul Sykes.
"How's she doing?"
Hili sikulitegemea.
"Mariam passed away many years back."
Leo nilitoka nyumbani.
Niliporudi nikakuta juu ya laptop yangu kitabu hicho hapo chini alichoandika Aili Mali Tripp.
Kitabu hiki kaniletea Zitto Kabwe.
Hakika dunia ni ndogo sana.
Nikiwa University of Iowa nikakutana na Prof. Michael Lofchie mwandishi wa kitabu: "Backgroud to Revolution," (1965).
Prof. Lofchie akaniambia kuwa yeye na Ally Sykes walikuwa marafiki wakubwa sana wakati alipokuwa Chuo Kikuu Cha Dar-es-Salaam.
Akaniambia kuwa alikuwa na hamu ya kukutana na mimi aliposikia kuwa nakuja kwenye kongamano na nitazungumza.
Ndugu yangu chukua tahadhari ukisikia msomi wa Kimarekani ana hamu na wewe jitayarishe kwani hakutafuti mpige soga.
Huyo kakusoma yako anayotaka kuyajua kutoka kwako kwa ushahidi.
Nililijua hili baadae.
Nilimfikishia Ally Sykes salamu zake kutoka kwa rafiki zake Marekani ambao miaka mingi hawajaonana.
Kitabu cha Aili Mari Tripp kimenikumbusha mengi.
Picha hiyo ya watu wengi Aili Tripp kasimama nyuma kushotoni kwangu na picha ya tatu ni Prof. Michael Lofchie.
Picha ya tatu ni James Brennan na ya nne ni James Giblin akiwa ofisini kwake akionyesha kitabu cha Abdul Sykes.
NB:
"Unakumbuka mambo vizuri.
Niliishi karibu na Mariamu Sykes pale Mbezi tukiwa watoto na tulikuwa marafiki.
Nasikitika kusikia kwamba alikufa.
Nitavutiwa kujua maoni yako kuhusu kitabu kuhusu Joan Wicken na Mwalimu Nyerere."
Aili Trip.