Aidha Magufuli au Lowassa, mabadiliko katika uhalisia

queenkami

JF-Expert Member
Feb 8, 2010
1,599
1,025
Ndugu zangu watanzania,naomba nitumie nafasi hii na mimi niseme langu la moyoni.Kwa sasa mimi sio mfuasi wa chama chochote cha kisiasa na siko upande wowote.

Mimi ni mmoja wa watanzania mwenye kiu ya mabadiliko na hata siwez kuelezea ni kiasi gani ninavyoyatamani mabadiliko kutokana na kuchoshwa na kero za nchi hii.Watanzania tunateseka sana bila sababu ilhali nchi yetu imebarikiwa utajiri wa ajabu.Kuna mateso tunayoyapata mimi huwa najiuliza hivi kweli serikali yetu ikiamua kwa dhati inashindwa kweli kutuondolea haya mateso??

Upande wa afya hali ni mbaya inasikitisha ukija kwenye elimu ndo utachoka lakini kila siku tunasikia mahela yakiibiwa na wezi wa pesa hizo hakuna wanachofanywa.Kero ni nyingi mno kila upande unanuka hakuna penye afadhali.Wenye kufaidi nchi hii ni matajiri na vigogo wa serikali na familia zao.Wake zao wanaenda kujifungulia ulaya na marekani sisi walalahoi tunajifungua kwa mateso huku tukichapwa makofi na manesi na ukibahatika ukajifungua salama bqsi mtalala Wanne kitanda kimoja na vichanga vyenu au mtalala chini.Kwa kweli haya mateso yamenifanya niwe na chuki kali sana dhidi ya CCm na viongozi Wake wote.Hawana huruma na mtanzania wanajijali wao na familia zao.NAICHUKIA CCM HADI NDANI YA MIFUPA YANGU.Kwangu mimi ccm ni genge la wanyonyaji.

Mimi nilikuaga Chadema damu ila nilijitoa siku LOWASSA alipokatwa na mafisadi wenzie wa CCM akakimbilia ukawa na akapokelewa. Yes, lOWASSA ni mmoja wa mafisadi aliyechangia watanzania kuishi maisha ya tabu bila sababu. CCM tunawalaumu kwa kutotufanyia la maana kwa miaka hamsini waliyotuongoza ila ikumbukwe katika hiyo miaka hamsin Lowasa amekua nao kwa miaka zaid ya 30 na hakuona ubaya wa ccm wala haja ya kutuletea mabadiliko ila baada ya mafisadi wenzie kumchezea rafu ghafla amekua mtakatifu mwenye kuuchukia umasikini.

Kwa miaka 30 aliyokua ccm hakuona kama watanzania wanahitaji mabadiliko,aliutumia ujana Wake wwoote kufanya mabadiliko kwenye salio lake la benki leo ghafla bin vuu roho wa Mtakatifu kamshukie uzeeni baada yakuchezewa rafu na na ndugu zake wa ccm eti anataka kulikomboa taifa hili.

Ndugu mtanzania kubali kataa nitukane upendavyo ila uchaguzi wa mwaka huu tumeingia choo cha walemavu, si Lowasa si Magufuli hakuna wakutuletea mabadiliko tunayoyataka. Magufuli yuko vizuri tatizo ccm, ukija kwa Lowasa ni FISADI PAPA tena ni Fisadi mgonjwa mroho macho yote kayakodoa kwenye gesi yetu.

Hivi mtanzania kwa akili yako kabisaa unaamini kuwa Lowassa na maswahiba zake wanatumia mabilion yote hayo ya pesa kuingia ikulu ili wewe kajambanani uje kuwa na maisha mazuri kama ya mwanae Freddy?? (hahaaaaa SMH).

Mtanzania wakati wa ukombozi bado haujafika. Ili tupate ukombozi tunahitaji mkombozi na kati ya hao mnaowashabikia hakuna hata mmoja wa kutukomboa.

Watanzania wote tumechoka na tunataka mabadilko ila inabidi tutumie hekima, busara na uvumilivu. Hasira zetu dhidi ya Maccm na kiu ya kuwatoa ili tupate mabadiliko isitufanye tuwe kama mwanamke aliyepitisha umri mkubwa bila kuolewa na hivyo kuamua kuolewa na hata mvuta bangi ilimradi na yeye avae pete ya ndoa kidoleni.

Watanzania mnaposema mko tayari kupigia kura hata jiwe au kivuli nakuwa siwaelewi kuwa mtakapoikabidhi nchi yetu tukufu ktk mikono isiyofaa sijui mnafikiri mnamkomoa nani.

Ili tupate mabadiliko inabidi tuchukue maamuzi magumu.Maamuzi magumu wakati mwingine inamaanisha kufanya vitu usivyopenda ili upate unachokitaka.

Mimi binafsi najua Lowasa ni hatari kwa taifa hili sababu ni FISADI na MGONJWA.
Kama huamni kuwa ni fisadi hiyo ni wewe na uwezo wako wakufikiri.

Hivi kwani huko ukawa hakuna mtu mwingine mwnye nguvu na afya anayeweza kusimama kama mgombea mpaka mtake kuikabidhi nchi yetu kwa mtu yuko mahututi hata kuongea hawezi jukwaan hadi apandishwe?Hata kama mnataka kuingoa ccm lkn sio ndio kwa kuchagua mgojwa hajiwezi,tuwen makin tutajuta badae Lowasa yule wazir mkuu sio Lowasa huyu wa leo.Lowasa hafai achilia mbali ufisadi ni mgonjwa jamani.

Kwa vile mnampenda Lowasa wenu chaguo la Mungu muombeni basi kwa faida ya nchi hii ateuwe mtu mwingine mwenye afya na nguvu agombee badala yake, yeye abaki kuwa mshauri mkuu.Kwanin anangangania kuingia ikulu wakati anajua fika hawez !!??,kwani ana nia gani hasa na Taifa hili..??

Mnasema mnamtaka hivyo hivyo sbb ikulu hakubebwi zege,fine ,ila ili alete mabadiliko anahitaji kutumia akili sana na wazungu wanasema mwili ukiumwa na ubongo unaumwa,ubongo ukiumwa na mwili lazima uumwe.Healthy body healthy mind.

Don't grant this beautiful Country to a dying Fisadi.He is not worthy it.
 
queenkami

Yani hatukuelewi kabisa,ATA MSEMAJE IKULU NI YA UKAWA AWAMU HII...NA HILI LIPO WAZI BILA UBISHI..

IMG-20150916-WA0002.jpg .
 
Last edited by a moderator:
Yani hatukuelewi kabisa,ATA MSEMAJE IKULU NI YA UKAWA AWAMU HII...NA HILI LIPO WAZI BILA UBISHI..

View attachment 288090.

Kwani kama UKAWA lazima iende ikulu huko ukawa nzima hakuna watu wengine wenye nguvu na afya mnaoweza kuwapigia kura?why must it be Lowasa.?Au Lowasa ndio ukawa na ukawa ni Lowasa?Ikitokea amekufa leo na ndoto zenu zinakufa au?Kwani kwa mfano akaona kuwa akastep down kutokana na hali yake halafu akateua mtu mwenye nguvu agombee kutoka huko huko ukawa kitaharibika nini?Kwanini anatumia mahela mengi na kila mbinu kutaka urais wakati hata kujifuta maudenda yake hawezi?Ana nia gani huyu mbabu na nchi hii?Ukiangalia uso wake tu unaona kabisa the old man is sick ila anataka kuwa rais.Why?Sijasema mchague Ccm ila ninachouliza kwanini mnataka kupeleka the walking dead kwenye ikulu yetu wakati huko huko UKAWA kuna watu wenye nguvu na afya?Kwani akibakia kama mshauri mkuu kitaharibika nini?
 
Queen ondoa shaka, Lowassa haingii ikulu...

Honestly najua sisi kama Taifa kuna vitu tunafanya vinamchukiza Mungu na sio ajabu akatuadhibu.Lowasa akifanikiwa kuwa rais wa nchi hii basi nitajua kabisa kuwa Mungu ameamua kutuadhibu bila huruma.Ila sometimes nataman Lowasa awe rais ili hawa wanaoimba MABADILIKO LOWASA LOWASA MABADILIKO niwaone watakavyolia kwa majuto then tuwaambie 'we told you guys' ila hapana tutaumia wengi so naombea kwa Mungu atuepushe na balaa hili.
 
queenkami

unaweza kunihakikishia kuwa magufuli hatakufa ndani ya miaka kumi ijayo?au wewe mwenyewe utakuwepo 2020?cpt komba si alitangaza kuingia msituni kumpinga warioba?leo yuko wapi wakati warioba bado anadunda?hebu tuambie wazazi wako wameshakufa?au unajua watakufa lini kwa sababu ni wazee?mbona huswemi wazazi wako wamezeeka wanaumwa kisukari,mapresha etc hawafai kuongoza familia?

sorry miss,tumeshafanya maamuzi,hata tukute mavi kwenye karatasi la kura,tutalipigia kura na siyo mgombea wa ccm
 
Last edited by a moderator:
hakuna mabadiliko ya kweli ndani ya ccm kamwe. ni ndoto...

Nyie watu mnatia huruma.Hata sio makosa yenu,ni makosa ya Ccm kushindwa kugaia wananchi wake elimu zaidi ya ile ya kusoma na kuandika.
Nakutakia kila lq kheri katika kuyapata mabadiliko.
 
unaweza kunihakikishia kuwa magufuli hatakufa ndani ya miaka kumi ijayo?au wewe mwenyewe utakuwepo 2020?cpt komba si alitangaza kuingia msituni kumpinga warioba?leo yuko wapi wakati warioba bado anadunda?hebu tuambie wazazi wako wameshakufa?au unajua watakufa lini kwa sababu ni wazee?mbona huswemi wazazi wako wamezeeka wanaumwa kisukari,mapresha etc hawafai kuongoza familia?

sorry miss,tumeshafanya maamuzi,hata tukute mavi kwenye karatasi la kura,tutalipigia kura na siyo mgombea wa ccm

Nyie watu jaribuni kutumia japo muda kidogo kutumia ubongo kusoma jambo na kulielewa,ukishaelewa litafakari na kulichekecha.
Sio kila anayewaambia Lowasa ni Fisadi au hatawapa hayo mabadiliko ni mwwna Ccm.Wewe hata ukitaka kunywa uharo wa Lowasa ukiamin utakuletea mabadiliko kunywa nin kupigia karatasi yenye mavi.Unadhan unamkomoa nani?Mnakurupuka sana nyie watu hlf wengi wenu Iq ndogo.Kama unabisha nioneshe sehemu nimesema upigie kura Ccm.
 
Unaanzisha uzi mwenyewe halafu una comment mwenyewe kweli fisiem mmekwisha, tuambie na wewe utakufa lini manake una Iq kubwa
 
Unaanzisha uzi mwenyewe halafu una comment mwenyewe kweli fisiem mmekwisha, tuambie na wewe utakufa lini manake una Iq kubwa

Roho imeniuma sana aisee ulivoniita ccm.Mm leo hii niwe ccm!!.Daah !!Akutukanae hakuchagulii tusi.
Jamani sio kila asiyemkubali fisadi lowasa ni ccm.
Wengine tunaoweza kuwa spot mafisadi walioko ndani na nje ya ccm.
Poleni nyie mnaodhani balaa liko ccm peke yake.Mna macho ila hamuoni.
 
Haya sasa nenda kachukue buku 5 zako naona jasho linakutoka sana fisiem.
Mbona unakwepa kutuambia wewe na wazazi wako mtakufa lini??

Roho imeniuma sana aisee ulivoniita ccm.Mm leo hii niwe ccm!!.Daah !!Akutukanae hakuchagulii tusi.
Jamani sio kila asiyemkubali fisadi lowasa ni ccm.
Wengine tunaoweza kuwa spot mafisadi walioko ndani na nje ya ccm.
Poleni nyie mnaodhani balaa liko ccm peke yake.Mna macho ila hamuoni.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom