Aibu yako umasikini wako

TechTino

Member
Oct 16, 2016
71
25
AIBU YAKO UMASKINI WAKO

Aibu na Umaskini, Vijana wengi tumekumbwa na changamoto ya aibu na kutupa wakati mgumu tutaanzaje kukabiliana na maisha hasa kwa wale walio jaliwa kupata elimu na kuhitimu katika vyuo mbalimbali ndani na nje ya nchi , msongo wa mawazo umewakumba wengi hasa pale unapotafuta kazi na bado hukufanikiwa kwa mara myingi zaidi ,pia unapo amuakuingia kujiajiri bado unakutana na changamoto nyingi ikiwemo kuogopa na kufikiria jamii itakuchukuliaje kuanza biashara yenye mtaji mdogo pamoja na kuvaa uhusika wa moja kwa moja. Mimi ni mmoja wa wahitimu wa chuo kikuu nimeshajaribu biashara nyingi mpaka sasa na ninajua baadhi ya changamoto, kosa moja kubwa la jamii pamoja na wahitimu ni kuamini kuwa watakapo hitimu tuu basi watapata kazi isopokuwa hivyo basi jamii huanza kuwazarau hufikia hata wao pia kujizarau na kufikia kuogopa kufanya jambo lolote wakiofia kuwa jamii itawachukuliaje kutokana na hadhi ya elimu walio nayo. Sisi kama vijana tunawezaje kujikwamua na kujitoa kwenye janga la umaskini na tegemezi , acha nikwambie jambo nililojifunza katika maisha ya utafutaji na wengi wamekuwa wakifanikiwa kupitia hilo , kama unahofu nahujiamini kuanzisha jambo mahari ulipo zaliwa au unapojulikana sana hama mahari hapo na nenda kaanze maisha mahari ambo utaonekana mgeni mara nyingi hii imekuwa ikiwasaidia vijana wengi kwani huondoa aibu na kuwapa ujasili.

MAMBO YA KUZINGATIA ILI KUJIKWAMUA KIUCHUMI SISI KAMA VIJANA NA JAMII
Mtu yeyote, anaweza kujijengea mafanikio makubwa kabisa kwa kuanzia pale alipo sasa. Hii ina maana kwamba kama huna pakuanzia kabisa, basi unaweza kuanzia chini kabisa, ukawekaa juhudi na maarifa, ukawa mvumilivu na king’ang’anizi na ukaweka muda na hatimaye ukafikia mafanikio makubwa. Ni kitu ambacho kinawezekana, lakini siyo rahisi.Ni ukweli usiopingika kuwa kila kitu katika maisha ya mwanadamu kina njia zake,mfano ukitaka kwenda mbinguni lazima upitie njia ya wokovu.Kadhalika Mafanikio yana njia zake. Kwani mafanikio hayana tabia ya kuja tuu na kutoka kusikojulikana ,badala yake yana namna yanavyoweza kupatikana, Jambo moja la muhimu kijana zingatia kuwa kila nchi ina taratibu zake zabkuhalalisha mali na upatikanaji wake basi fuata njia halali katika harakati zako za kutafuta mali usikimbilie urahisi na wepesi vya haraka havidumu nakukumbusha tuu. Basi sasa tuangalie baadhi ya jia ambazo kijana anaweza kuzitumia na kufikia mafanikio nakusisitiza tuu kuwa sipo njia nyingi za halali na halamu, Njia zetu halali za kufikia mafanikio ni kama ifuatavyo…..,

Fanya ibada, Vijana wengi wanahau kuwa katika mafanikio kuna Mungu na imani ,kwanini nasema kijana afanye ibada ,kwasababu huku kwa Mungu ndiko kuna usalama zaidi wa maisha yetu na mali tunazozitafuta kifupi mimi naweza kumwambia kijana kuwa kitabu cha mafanikio cha kwanza ni Biblia au Quran Tukufu kutegemea na imani yako huku ndiko tunapata vijana wavumilivu, wenye kusubiri wenye hekima na busara ,pia vitabu hivi vimemaliza kila kitu kwa kijana kufanikiwa , jitahidi kusoma vitabu hivi vya kiimani kama utaweza soma vyote viwili naamini kuna kitu utajifunza achana na dhumuni jingine ila soma ujue Mungu ananjia gani nyingi za kutufanya wanadam tufanikiwe. AMINI MUNGU YUPO NA ANATENDA achana na njia za kishirikina wengi tunasikia wanavyoteseka kwa upande huo huku wengi wakitoa shuhuda za upande huo.

Acha kutalajia kila jambo ulilopanga liende kama ulivyopanga, Nimeanza na Mungu kwanza ili kijana mwenzagu utambue kuwa tunapambana na maisha lakini hatuwezi kupambana na kumbadilisha Mungu juu ya anayotuwazia kwahiyo pambana na usikate tamaa lakini kaa ukijua mambo hupangwa na Mungu. Mtu anaefanya jambo lake kwa uvivu hawezi fanikiwa kamwe mwisho atamlaum kila mtu sasa ilikuepuka kuwalaum watu fanya mipango yako kwa umakini, juhudi na maarifa.

Acha hofu ya kushindwa , Vijana wengi wamwkuwa wahanga wa mambo yatalajiwayo ,jambo hilo limetesa na kuwaumiza wengi iwe kwenye harakati za kutafuta kazi au kuanza biashara wengi wamekuwa wakiwaza kushindwa , acha nikwambie jambo kijana na ndugu yangu wote sisi tunatafuta mafanikio lakini kitendo cha kuona kuwa utashindwa tuu kinaharibu ubongo wako na kuufanya uwe mtu wa kushindwa kila jambo maana utaingia na mkono legelege, akili iliyochoka na maarifa finyu. Pambana kijana mambo sio mepesi kwa mtazamo ila kusha anza utapata nafasi nyingi na njia tofauti tofauti za kukabili hofu yako.
Acha mawzo hasi, nikukumbushe kijana kuwa imani inafanya kazi muda wote kitendo cha kuufanya ubongo wako kuamini mambo yasio kuwa natija kwenye harakati zako yatakukwamisha , kila mtu anajua kuwa ushirikina umekuwa mwingi kila mahali kunamabango "mgaganga toka ….. anatoa pete ya mali, anatoa chumaulete analeta mvuto" vijana wengi wamekuwa wakimbilia huko na kuamini kuwa kunawatu wanawakwamisha lakini katika uhalisia vijana wengi huanza kukwama kwenye mawazo yao na mitazamo yao juu ya kile wanenda kukianzisha mwisho wa siku tunakuwa watumwa wa watu wengine jambo likishindikana tuu basi umeshawaza kuwa kuna mtu anakukwamisha, Wahanga wengine ni vijana wanaoamini kuwa kila jambo Mungu atawafanyia ,Mungu mwewenye anataka tufanye kazi kwa bidii ili tupate mafanikio tumtolee dhaka na sadaka , amka kijana naamini mahali ulipo bado hujashindwa na kama umefanikiwa basi bado kunachangamoto zitakuja binadamu aisiyekuwa na changamoto basi huyo hajafanya jambo lolote katika maisha yake bado.

Zingatia malengo yako, Hakikisha unakuwa mbishi kushikamana na malengo yako ilimradi unajua unakokwwnda usiwe mtu wa kuyumbishwa na kila kinachokukatisha tamaa ,sio vibaya kubadili jambo ambalo unaona haliendi sawa lakini ni vyema unapolianzisha jambo basi lifanikiwe kabla hujaingia kwenye jambo lingine ,kuna usemi unasema kuwa "mshika mawili moja humponyoka" huu usemi una maana kubwa sana hasa kwasisi wanaharakati wa kutafuta mafanikio kwasababu mafanikio hayaji kirahi basi pambana wewe wala mimi si wa kwanza kwenye njia ya mafanikio amini kuwa lengo lako ndio bora zaidi ila usiache kujifunza na kupokea ushauri kutoka kwa wengine.

Usijilinganishe na wengine, Kujilinganisha na watu wengine kunaleta kukata tamaa kwasababu tunajipa mzigo ambao bado hatujaufikia , amini kuwa wewe ndio mtu sahihi wa kujilinganisha na wewe , sio vibaya kuangalia watu waliofanikiwa na kuwatazama wao na namna walivyo fikia mafanikio waliyo nayo , ukijilinganisha sana na wengine inaweza kukuletea msongo wa mawazo na kulazima kufikia mahali fulani kwa muda mfupi wakati unajilinganisha nae alipambana zaidi ya miaka mingi hadi kufikia hapo alipo katika mafanikio yake.

Acha wivu na tamaa, Kijana ukisha jiona kuwa unawivu mpaka unaumia na unatamani mtu aliyekuzdi au unaeshindana nae kibiashara mambo yake yayumbe basi ujue bado hujakomaa kuingia kwenye biashara waswahili wanasema wivu ni kidonda ukiushiriki utakonda na wivu ndio unafanya vijana wanakuwa na tamaa ya mali na kutaka kuipata kwa haraka kumbe harakaharaka haina baraka mwisho wanashindwa kufikia malengo na kuwa watu wanaopiga hatua mbili mbele mbili nyuma. Tamaa imewafanya vijana waishie magerezani wengine kuingia kwenye biashara na makundi halamu.

Acha matumizi yasiyo ya lazima yatakayotumia faida yako yote,Vijana tumekumbwa na janga anasa na starehe za kupitiliza yani mtu anatumia pesa hata zaidi ya anavyozalisha , nikukumbushe kuwa pesa unayoipata haiwezi kuzalisha pesa nyingine pasipokuwa na nidhamu katika matumizi yake heshimu nguvu na jasho lako usitumie ovyo na wala usiingie kwenye starehee ambazo zitakuletea urahibu (chronic) mfano matumizi ya sigara , pombe na badhi ya michezo ya kubahatisha vijana wanacheza kupita kiasi nakujikuta wanapoteza zaidi kuliko kupata ,sisemi watu wasicheze ila chunguza faida unayopata inalingana na muda na pesa unayoitumia ,pia katika hili nikukumbushe lejea vitabu vya dini vitakufunza juu ya michezo hii jee inamanufaa na jee watu wote waliofanikiwa walipitia huko, usiifanye akili yako iamini kuwa huna jianyingine ya kupata mtaji.

Usiwe na wachumba wengi, Hapa vijana wengi ni wahanga unakuta kijana anawachumba zaidi ya mmoja nawengine si wachumba lakini ni uhuni , kuto linda matumizi ya pesa unapokuwa na pesa inawaghalimu vijana wengi sana "mahali unapowekeza pesa yako zaidi huko ndiko moyo wako uliko" kwahiyo kijana chunga sana matumizi ya pesa unapanza biashara yako wengine wapo sio kuambatana na wewe katika changamoto zako ila wapo kuambatana na wewe katika mafanikio yako , asilimia kubwa vijana wamekuwa wahanga wa mahusiano hasa pale wanapotenga kwahiyo ili kuepukana na jambo hili tuliza akili chagua mmoja ambae mtafikia malengo yetu hata kama mmoja wenu ataishia njia basi kuna jambo moja nimekwisha kwambia AMINI KUWA MUNGU YUPO NA MAMBO UPANGWA NA YEYE, acha kulazimisha mapenzi unawezakujikuta unaacha harakati zako za utafutaji na kuwa mtumwa wa mapenzi.

Muda unaopata unathamani kuliko pesa , Watu wengi wako bize kutafuta pesa lakini muda ndio kila kitu ,kama hupati nafasi ya kufanya jambo basi jua huwezi fanikiwa na kama lengo lako kupata pesa kama huna muda basi huna pesa , nikupe mfano wa watu walio gerezani hawana muda wa kutafuta pesa na hawana pesa , kwahiyo muda ndio kila kitu usipoteze muda wako kwenye mambo yasiokuwa ya msingi na kukujenga kwenye harakati za mafanikio , watu husema kuanguka si kushindwa ila kushindwa kuinuka ndio kushindwa kukubwa hivyo kwanye kuinuka kuna muda ukishindwa kuinika jua huna muda , Kijana acha kujikadilia muda wa mafanikio maisha yetu ni leo hakuna anejua kesho yake hivyo pambana leo kesho itakuja tuu usijipe kazi ya kutaka kulazimisha kuijua kesho mwisho utajikuta unakata tamaa kwa kuogopa kifo , na mambo mengine .
Waepuke marafiki wavivu na wasio kuwa na tija katika mapambano yako ya mafanikio bila hivyo watakuangusha tuu kwakuwa mmetofautiana mitazamo mmoja mafanikio tuu na mmoja matumizi tuu bila kufanya kazi.

ZINGATIA MUDA UNAWEZA KURUDISHA PESA ILA PESA HAIWEZI KURUDISHA PESA PAMBANA SASA KESHO ITAKUJA NA MAMBO YAKE
 
AIBU YAKO UMASKINI WAKO

Aibu na Umaskini, Vijana wengi tumekumbwa na changamoto ya aibu na kutupa wakati mgumu tutaanzaje kukabiliana na maisha hasa kwa wale walio jaliwa kupata elimu na kuhitimu katika vyuo mbalimbali ndani na nje ya nchi , msongo wa mawazo umewakumba wengi hasa pale unapotafuta kazi na bado hukufanikiwa kwa mara myingi zaidi ,pia unapo amuakuingia kujiajiri bado unakutana na changamoto nyingi ikiwemo kuogopa na kufikiria jamii i
ANDIKO zuri sanaaa..

Ila zingatia paragraph.

Weka paragraph fupifupi ili usaidie wazee wa Scanning and fast peruzing..!!!

Other wise....

HONGERA KWA KUWA NA MAWAZO HAYA.

#YNWA
 
Degree ya Toursm ipo kabatini tu na sidhani kama nitakuja kuomba kazi tena.
Nilianza kama dalali wa Viwnja na mashamba baada ya kuona ajira imekuwa ngumu kupatikana lakini nilikuwa nikaimini ipo siku nitafanikiwa.

Nilikutana na Kijana mwenzangu anaitwa Jeff yeye ana experience na biashara ya ardhi kwa muda mrefu alinifundisha biashara challenges zake na namna ya kutengeneza faida.

Wakati naanza udalali hata baadhi ya ndugu zangu walisema yani unaacha kutafuta kazi msomi unakuwa Dalali?
Nilikutana na maneno mengi ya kukatisha tamaa ila niliamini fikra na maono yangu.
Mpaka sasa nimesha sajili kampuni @Leven Land and Property Ltd baada ya kununua mashamba Kigamboni na Vikindu.

Pengine ni jambo gumu kwa kijana kubadi mtazamo juu namna ya kujishusha ili upate ridhiki yako ukweli ni kwamba njia pekee wakati mwingine ni kujishusha tu na kukubali uhalisia wako ili siku moja uje kufanikiwa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom