Glasnost
JF-Expert Member
- May 18, 2017
- 266
- 259
Nimeshangazwa na hali niliyoiona na kuikuta kwenye tovuti ya shirikisho la soka Tanzania (TFF). Kilichonisukuma kuingia kwenye tovuti hii ni jambo ambalo kila mwanamichezo,mpenda soka au mtafiti anaweza kufanya katika kutaka kupata habari zilizojiri, zitakazojiri na hata pia kutaka kufahamu mambo mbalimbali kuhusu soka la Tanzania. Mimi nilikuwa nataka kufahamu majina ya walioshinda, katika uchaguzi uliomalizika wa TFF, katika ngazi mbalimbali hapa Tanzania, lakini nilichokuta na kuona huko nilifadhaika sana, nilisikitika na kujiuliza maswali mengi mno.
Hii ni mara ya pili sasa, baada ya ile ya mara ya kwanza ya kutaka kufahamu waliopitishwa kugombea nafasi mbalimbali za TFF. Takriban wiki sasa tangu uongozi mpya uingie, hakuna mabadiliko yoyote ya kiutendaji. Mazoea yanaendelea kufanyika na hakuna wa kushangaa au kuuliza ni kwanini tovuti ya chama cha soka Tanzania haifanyi kazi. Najiuliza sipati majibu, je ni pesa za kuendesha ndo tatizo au haina wataalamu katika kitengo cha habari na mawasiliano?
Historia ya TFF imeandikwa katika mpangilio mbovu,haina maelezo ya kutosha na kuridhisha kwa msomaji, kamati mbalimbali za michezo,bodi ya wakurugenzi na wafanyazi wa ngazi za juu hakuna maelezo wala wasifu wao. Maswali mengi mtu unajiuliza hivi idara ya habari,teknolojia na mawasiliano inafanya kazi gani? Tovuti hii imetumia lugha ya kiingereza kama lugha kuu lakini cha kushangaza na kutia aibu kwa taifa ni mchanganyiko wa lugha mbili yaani Kiswahili na kiingereza kwa wakati mmoja. Unakuta kichwa cha habari kimeandikwa kwa lugha ya kiingereza alafu habari kamili kwa lugha ya Kiswahili.
Uboreshaji na mwendelezo wa habari mpya ni mdogo sana wa tovuti hii, tangu Novemba 2016 (miezi tisa na ushee sasa) hakuna habari mpya mpaka sasa. “Mkwasa ataja Taifa stars itakayoivaa Zimbabwe November 13”, ndio Ilikuwa habari mwisho kuandikwa katika tovuti yao. Sasa mtu unaweza jiuliza ina maana hawajui umuhimu wa habari za soka kwa wadau na wanachi wa Tanzania leo hii? Kweli wameshindwa kuiendesha tovuti hii?
Hii tabia ya kutozingatia au ya “kuchukulia poa”, kutofanya kazi kwa ufanisi na kupuuzia mambo muhimu iliyojengeka miongoni mwa mashirika ya umma na taasisi binafsi ni ya hatari na yakupigwa vita kila sehemu. Katika dunia ya karne ya 21 sitegemei mambo haya kuendekezwa hata kidogo. Kupata habari ni jambo muhimu na ni maendeleo pia kwa hivyo ni jukumu la kila kiongozi wa ngazi yoyote ile kulipa kipaumbele. Unapoona vitu kama hivi inatia hasira na kuuzunisha, ni wapi tunakwenda kama baadhi ya watu waliopewa dhamana hiyo hawafanyi kazi kwa ufanisi.
Afisa habari wa TFF Bwn. Afred Lucas ni mtu ambaye lazima anafahamu umuhimu wa habari kwa mwananchi. Kumnyima mwananchi fursa ya kupata habari ni kosa kikatiba na pia kiofisi ni kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi na kwa ujuzi ulioaminiwa kuwa unaweza hiyo kazi.
Ni wakati sasa shirikisho la soka Tanzania (TFF) kufanya masuala ya soka kwa kufuata misingi ya utawala bora,kuacha kufanya kazi kwa mazoea, pia kuajiri watu wenye weledi wa kazi hizo. Yapo baadhi ya makampuni yanaajiri watu pale tu shida inapotokea ya kiufundi kwa sababu hawana wajuzi ndani ya makampuni yao,lakini unaweza kuta katika mikataba yao na wawezeshaji wa pesa za miradi na kuendesha hizo taasisi wanajua kuwa wana watu wa teknolojia na mawasiliano wakati ni uongo mtupu.
Kuna watu wana ujuzi wa lugha za kigeni, ujuzi katika teknolojia ya habari na mawasiliano, watumieni ipasavyo, toeni ajira kwa sifa na sio kwa kujuana au kutoajiri kabisa, maana mwisho wa siku tunaaibika sote na sio TFF peke yake. Fikiria kwa sekunde kadhaa mtu anataka kufanya utafiti kuhusu masuala ya soka Tanzania alafu anakutana na vitu vya ajabu au “upuuzi” kama niliokutana nao mimi. Hivi kweli unakuwa na tovuti iliyojipambanua kutumia lugha ya kigeni au ya kibiashara(Kiingereza) kujitangaza alafu maelezo yake yanakuwa vingine tena sio kwa ueledi na ufanisi wa kitaalamu na kulikoroga zaidi Kiswahili kinatumika kueleza habari iliyotakiwa kuwa katika lugha ya Kiingereza ?.
Kwakuwa uchaguzi umemalizika na kupatikana raisi na makamo mpya basi ni wakati sahihi kabisa kwa raisi mpya wa TFF kuwa timu ya watu waliotukuka kimaadili,ueledi na wenye kujua nini maana ya utawala bora. Hatuwezi kuendesha soka la Tanzania kizembezembe na kutokwenda na wakati katika dunia ya leo. Maendeleo hayapatikani kwa porojo, uvivu na ukosefu wa fikra endelevu.