AIBU: Kikwete aingizwa mkenge Mbozi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

AIBU: Kikwete aingizwa mkenge Mbozi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Jul 8, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jul 8, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,614
  Trophy Points: 280
  Mussa Juma, Dodoma

  [​IMG]Rais Jakaya Kikwete

  MRADI wa Utunzwaji wa Kumbukumbu za Usajili wa Hati za Miliki za Kimila kwa mfumo wa kompyuta umemwingiza tena Rais Jakaya Kikwete katika mtego wa kudanganywa na watendaji wake na kusababisha azindue ofisi hewa za mradi huo ambazo ziliyeyuka siku chache baada ya uzinduzi.

  Hii ni mara ya pili kwa Rais Kikwete kuripotiwa kushiriki kwa kuzindua, au kuhudhuria hafla za miradi yenye utata katika kipindi kisichozidi mwezi mmoja.

  Juni 22, mwaka huu Mbunge wa Kyela, Dk Harrison Mwakyembe alilieleza Bunge kuwa rais alidanganywa kwa kushikishwa bango la hundi ya mkopo hewa na benki ya NMB mkoani Mbeya na Julai 2, mwaka huu alizindua mradi wenye mgogoro wa kisheria wa Bwawa maji la Manchira lililoko wilayani Serengeti, Mara.

  Juzi Mbunge wa Mbozi Mashariki, Godfrey Zambi (CCM) alilieleza Bunge kuwa Rais Kikwete alidanganywa katika mradi wa utunzaji kumbukumbu za usajili wa hati za miliki za kimila kwa mfumo wa kompyuta aliouzindua Oktoba mwaka jana.

  Alisema mradi huo uliozinduliwa na Rais wilayani Mbozi, haujafanya kazi na kompyuta zote alizoonyeshwa kuwa zipo kwa ajili ya kazi hiyo, zilitoweka mara tu baada ya uzinduzi huo.

  Mbunge huyo alisema hayo wakati Bunge likiwa limekaa Kamati kwa ajili ya kupitisha bajeti ya Wizara wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

  Katika hoja hiyo Zambi alitaka Waziri mwenye dhamana atolee ufafanuzi suala hilo kabla bajeti yake haijapitishwa.

  Alisema Rais Kikwete alizindua mradi huo Oktoba 31, mwaka jana katika Kata ya Harungu ambayo ilikuwa kata ya mfano nchini kwa kutekeleza mradi wa utolewaji hati miliki za ardhi za kimila nchini.

  Alieleza kuwa baada ya uzinduzi huo wataalamu wa ardhi, walimwonyesha Rais Kikwete jinsi watakavyotunza kumbukumbu za hati miliki za kimila, jambo ambalo lifurahiwa na rais na wananchi waliohudhuria hafla hiyo.

  Zambi alilieleza Bunge kuwa tangu mradi huo uzinduliwe na baada ya rais kuondoka, jengo la mradi limefungwa, kompyuta zote hazipo na hata wataalamu ambao waliahidi wangefanya kazi hiyo mbele ya rais hawapo tena.

  Akifafanua hoja hiyo nje ya Ukumbi wa Bunge, Zambi alisema mradi huo upo takriban kilometa 25 kutoka makao makuu ya wilaya ya Mbozi na wataalamu ambao walikuwa wakisimamia mradi huo walipata mafunzo kutoka wizara hiyo ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi.

  "Wananchi wa eneo hilo wameshangazwa na kutofanya kazi kwa kituo hicho cha masjala na wamekuwa na maswali mengi yasiyokuwa na majibu," alisema Zambi.

  Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, John Chiligati aliahidi kuwa kompyuta zote zilizokuwapo kwenye kituo hicho zitarejeshwa mapema ili mradi uendelee.

  Katika tukio la Rais kudanganywa na NMB, Mwakyembe alilieleza Bunge kuwa benki hiyo ilimbebesha rais bango kubwa la mkopo wa Sh20 milioni ya Chama Cha Kuweka na Kukopa cha Kimbalu kilichoko wilayani Kyela.

  Dk Mwakyembe alitoa tuhuma hizo alipokuwa akichangia makadirio ya bajeti ya Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika.

  Alisema Oktoba 11, 2008, Rais Kikwete alitembelea wilaya ya Kyela ambako alizindua maktaba na jengo la kisasa la Saccos ya Kimbalu.

  “Kabla ya ujio huo wa rais, Saccos hiyo ilikuwa imeanza kuprocess mkopo kutoka benki ya NMB lakini, ulikuwa bado haujaiva,” alisema Dk Mwakyembe na kuongeza:

  “Lakini siku ambayo rais alifika, ikaletwa ‘cheki’ (hundi) kuubwa ya Sh20 milioni na kumkabidhi rais na kusema fedha hizo zimepatikana, kilichobaki ni kuchukuliwa tu.

  “Rais aliuliza hii fedha ni mkopo au msaada? Wakajibu ni Mkopo. Akaishika hundi hiyo na kuinyanyua juu kuwaonyesha wanaSaccos hao.

  “Cha ajabu, tangu tarehe hiyo (Oktoba 11, 2008 hadi ninavyozungumza hapa, ile fedha hizo hasijapatikana na kila wakienda benki wanaambiwa masharti ambayo hayatekelezeki”.

  Julai 2, mwaka huu Rais Kikwete pia alizindua mradi wa Bwawa la Manchira lililoko wilayani Serengeti wakati wananchi wamekwishafungua kesi Mahakama Kuu ya Mwanza wakidai fidia.

  Kesi hiyo iliyofunguliwa ni matokeo ya viongozi wa serikali wilayani Serengeti kudaiwa kuhsiriki kuwalipa fidia watu wasiohusika na kuwaacha walengwa waliofanyiwa tathmini.

  Kesi hiyo ya madai namba 21/2009 iliyofunguliwa katika Mahakama Kuu ya Mwanza, Kitengo cha Ardhi chini ya Jaji Nyangarika inahusisha wananchi 77 ambao wanadai kiasi cha Sh2 bilioni.

  Mmoja wa wawakilishi wa wananchi hao, Jackson Mwita aliwaambia waandishi wa habari wakati wakimsubiri Rais Kikwete katika bwawa hilo kwamba, fedha walizotakiwa kuwalipa waathirika wa mradi huo walilipwa watu wasistahili na viongozi wa wilaya wawapuuza walalamikaji.

  Alisema wanashangaa mradi huo kuzinduliwa kwa mbwembwe wakati halmashauri ya wilaya imefikishwa mahakamani na wameitwa mara tatu bila kuhudhuria.

  “Tulipanga kumfikishia Rais ujumbe kwa njia ya mabango, ajue kuwa kadanganywa maana eneo lina mgogoro ili baada ya kuzindua asije akasikia taarifa nyingine mbaya kwa kuwa wasaisizi wake si wakweli, lakini tumetishwa,” alisema Mwita.

  Hata hivyo, wananchi hao baada ya kutishwa kupitia wenyeviti wa vitongoji ambao inadaiwa kuwa Mkuu wa Wilaya hiyo, Edward Ole Lenga alikutana nao usiku na kuwataka wahakikishe wananchi hawatoi mabango.
  Kikwete aingizwa mkenge Mbozi

  Hawa washauri wa Mzee J.Kikwete mbona wanamfanya Mzee J.Kikwete kama Babu yao? kila mara wanamdanganya?Watamdanganya mpaka lini Rais wa Nchi?
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Jul 8, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Mnawaonea tu wasaidizi wa Rais...
   
 3. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #3
  Jul 8, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Inaelekea ata alipokuwa shule akipewa sumu I mean majibu ya uongo does not querry anareproduce tuu!
  Wasaidizi hawatakiwi kulaumiwa bse ata akifaamu kuwa kadanganywa hachukuaji hatua.
   
 4. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #4
  Jul 8, 2010
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  [​IMG]
   
 5. Bramo

  Bramo JF Bronze Member

  #5
  Jul 8, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 9,454
  Likes Received: 2,504
  Trophy Points: 280
  MRADI wa Utunzwaji wa Kumbukumbu za Usajili wa Hati za Miliki za Kimila kwa mfumo wa kompyuta umemwingiza tena Rais Jakaya Kikwete katika mtego wa kudanganywa na watendaji wake na kusababisha azindue ofisi hewa za mradi huo ambazo ziliyeyuka siku chache baada ya uzinduzi.

  Hii ni mara ya pili kwa Rais Kikwete kuripotiwa kushiriki kwa kuzindua, au kuhudhuria hafla za miradi yenye utata katika kipindi kisichozidi mwezi mmoja.

  Juni 22, mwaka huu Mbunge wa Kyela, Dk Harrison Mwakyembe alilieleza Bunge kuwa rais alidanganywa kwa kushikishwa bango la hundi ya mkopo hewa na benki ya NMB mkoani Mbeya na Julai 2, mwaka huu alizindua mradi wenye mgogoro wa kisheria wa Bwawa maji la Manchira lililoko wilayani Serengeti, Mara.

  Juzi Mbunge wa Mbozi Mashariki, Godfrey Zambi (CCM) alilieleza Bunge kuwa Rais Kikwete alidanganywa katika mradi wa utunzaji kumbukumbu za usajili wa hati za miliki za kimila kwa mfumo wa kompyuta aliouzindua Oktoba mwaka jana.

  Alisema mradi huo uliozinduliwa na Rais wilayani Mbozi, haujafanya kazi na kompyuta zote alizoonyeshwa kuwa zipo kwa ajili ya kazi hiyo, zilitoweka mara tu baada ya uzinduzi huo.

  Mbunge huyo alisema hayo wakati Bunge likiwa limekaa Kamati kwa ajili ya kupitisha bajeti ya Wizara wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

  Katika hoja hiyo Zambi alitaka Waziri mwenye dhamana atolee ufafanuzi suala hilo kabla bajeti yake haijapitishwa.

  Alisema Rais Kikwete alizindua mradi huo Oktoba 31, mwaka jana katika Kata ya Harungu ambayo ilikuwa kata ya mfano nchini kwa kutekeleza mradi wa utolewaji hati miliki za ardhi za kimila nchini.

  Alieleza kuwa baada ya uzinduzi huo wataalamu wa ardhi, walimwonyesha Rais Kikwete jinsi watakavyotunza kumbukumbu za hati miliki za kimila, jambo ambalo lifurahiwa na rais na wananchi waliohudhuria hafla hiyo.

  Zambi alilieleza Bunge kuwa tangu mradi huo uzinduliwe na baada ya rais kuondoka, jengo la mradi limefungwa, kompyuta zote hazipo na hata wataalamu ambao waliahidi wangefanya kazi hiyo mbele ya rais hawapo tena.

  Akifafanua hoja hiyo nje ya Ukumbi wa Bunge, Zambi alisema mradi huo upo takriban kilometa 25 kutoka makao makuu ya wilaya ya Mbozi na wataalamu ambao walikuwa wakisimamia mradi huo walipata mafunzo kutoka wizara hiyo ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi.

  "Wananchi wa eneo hilo wameshangazwa na kutofanya kazi kwa kituo hicho cha masjala na wamekuwa na maswali mengi yasiyokuwa na majibu," alisema Zambi.

  Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, John Chiligati aliahidi kuwa kompyuta zote zilizokuwapo kwenye kituo hicho zitarejeshwa mapema ili mradi uendelee.

  Katika tukio la Rais kudanganywa na NMB, Mwakyembe alilieleza Bunge kuwa benki hiyo ilimbebesha rais bango kubwa la mkopo wa Sh20 milioni ya Chama Cha Kuweka na Kukopa cha Kimbalu kilichoko wilayani Kyela.

  Dk Mwakyembe alitoa tuhuma hizo alipokuwa akichangia makadirio ya bajeti ya Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika.

  Alisema Oktoba 11, 2008, Rais Kikwete alitembelea wilaya ya Kyela ambako alizindua maktaba na jengo la kisasa la Saccos ya Kimbalu.

  “Kabla ya ujio huo wa rais, Saccos hiyo ilikuwa imeanza kuprocess mkopo kutoka benki ya NMB lakini, ulikuwa bado haujaiva,” alisema Dk Mwakyembe na kuongeza:

  “Lakini siku ambayo rais alifika, ikaletwa ‘cheki’ (hundi) kuubwa ya Sh20 milioni na kumkabidhi rais na kusema fedha hizo zimepatikana, kilichobaki ni kuchukuliwa tu.

  “Rais aliuliza hii fedha ni mkopo au msaada? Wakajibu ni Mkopo. Akaishika hundi hiyo na kuinyanyua juu kuwaonyesha wanaSaccos hao.

  “Cha ajabu, tangu tarehe hiyo (Oktoba 11, 2008 hadi ninavyozungumza hapa, ile fedha hizo hasijapatikana na kila wakienda benki wanaambiwa masharti ambayo hayatekelezeki”.

  Julai 2, mwaka huu Rais Kikwete pia alizindua mradi wa Bwawa la Manchira lililoko wilayani Serengeti wakati wananchi wamekwishafungua kesi Mahakama Kuu ya Mwanza wakidai fidia.

  Kesi hiyo iliyofunguliwa ni matokeo ya viongozi wa serikali wilayani Serengeti kudaiwa kuhsiriki kuwalipa fidia watu wasiohusika na kuwaacha walengwa waliofanyiwa tathmini.

  Kesi hiyo ya madai namba 21/2009 iliyofunguliwa katika Mahakama Kuu ya Mwanza, Kitengo cha Ardhi chini ya Jaji Nyangarika inahusisha wananchi 77 ambao wanadai kiasi cha Sh2 bilioni.

  Mmoja wa wawakilishi wa wananchi hao, Jackson Mwita aliwaambia waandishi wa habari wakati wakimsubiri Rais Kikwete katika bwawa hilo kwamba, fedha walizotakiwa kuwalipa waathirika wa mradi huo walilipwa watu wasistahili na viongozi wa wilaya wawapuuza walalamikaji.

  Alisema wanashangaa mradi huo kuzinduliwa kwa mbwembwe wakati halmashauri ya wilaya imefikishwa mahakamani na wameitwa mara tatu bila kuhudhuria.

  “Tulipanga kumfikishia Rais ujumbe kwa njia ya mabango, ajue kuwa kadanganywa maana eneo lina mgogoro ili baada ya kuzindua asije akasikia taarifa nyingine mbaya kwa kuwa wasaisizi wake si wakweli, lakini tumetishwa,” alisema Mwita.

  Hata hivyo, wananchi hao baada ya kutishwa kupitia wenyeviti wa vitongoji ambao inadaiwa kuwa Mkuu wa Wilaya hiyo, Edward Ole Lenga alikutana nao usiku na kuwataka wahakikishe wananchi hawatoi mabango.

  Source: Mwananchi
   
 6. W

  WAMURUBHERE JF-Expert Member

  #6
  Jul 8, 2010
  Joined: Apr 21, 2010
  Messages: 337
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  bado anajifunza uongozi si keshasema jamani!
   
 7. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #7
  Jul 8, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  ha ha ha wanamuona kiongozi mzugaji kwahio wanajitesea tu kwa kumfanyia usanii.
   
Loading...