Ndwanga
Member
- Dec 9, 2011
- 23
- 2
Katika hali isiyo ya kawaida nikiwa katika pitapita zangu za kujitaftia riziki nilijikuta katika hali ya mshangao pale nilipo kumbana na vijana wabunifu wa ajira zisizo rasimi ambapo vijana walikua wakifanya kazi ya kutoa magari yaliokua yakikwama katika shimo la maji machafu na kutoza fedha madereva wa magari hayo. Shimo ilo lipo maeneo ya Posta pembeni mwajengo la HIDERY PLAZA. Kwakifupi barabara hii imekua kero kubwa kwa madereva wa magari kwani inamashimo yasio ya kawaida yani utafikiri sio barabara ya lami na hata kama ni lami haipo katikati ya mji. swali ni kwamba je wahusika hawajaona kero hio? na je fedha zinazotengwa kwa ajili ya ukarabati wa barabara (road maintenance) hazitoshi. na wahusika wa idara husika wafanya kazi gani?