Mshikaji kajikuta katika hali ya taharuki baada ya kutumbukia pasipo kujua katika shimo la maji taka lililopo pembezoni mwa jengo la HIDERY PLAZA posta
Hatari sanaa ilo ni eneo korofi na kibaya zaid halina alama yeyote ya oyo ila lakufuraisha ni kwamba kuna vijana wameweka kijiwe kwaajili ya magari madogo yanayo kwama
Eneo lote la katikati ya jiji liko hivyo. Mifuniko ya majitaka imeibwa almost kila kona. Hali ni hiyo hiyo hapo barabara ya Samora, ilipo wizara ya Ujenzi. Na penyewe na shimo wazi la majitaka
Mkuu kila mwaka ndio wembo huwo huwo tu na siyo hapo ni kila sehemu ya kitumbini mnazi mmoja uhuru lakini wamekaa kimya kama vipofu lakini subiri ukaribei uchaguzi basi hapo tena vishindo vya ukarabati na ufisadi na sisi tena wavimba macho huwa zile hasira za mateso tunakuwa tushazisahau tunachekelia sasa safi kumbe washashiba sana wao wausika na hiyo kazi ya kubo bota bobota na si ya kudumu ni ufisadi tuu
Usiombe ukutwe na janga alafu watu walio jirani na wewe wawe wateja wa FB,IG au ana Blog dadadadekiiiii utaomba ardhi ipasuke mpaka wakuokoe lazima 360 zimekuphotoa sana.