Aibu: Bunge la awamu ya 5 laua utalii wa filamu na ndoto ya Kikwete

nzagambadume

JF-Expert Member
Apr 9, 2018
2,430
5,769
Amini usiamini ila hili ndilo bunge la hovyo kuwahi kutokea katika historia ya nchi hii likiendeshwa na speaker dhaifu kabisa,nafikiri hata nchi za kifalme zina mabunge yenye nafuu kuliko hili,sitaongelea udhaifu wa wabunge haswa wa CCM katika kuchambua mambo mambo ufahamu wa IQ zao na jinsi hata wasivyojua dunia inaendaje,leo nazungumzia sheria ya marekebisho ya filamu waliyopitisha.Lord have mercy on us,were these dudes high on cocaine au nini?

Wakati wa awamu ya nne Rais kikwete alikwenda marekani akakutana na producer/actor/director aitwaye William zahne maarufu kama Bill zahne katika moja ya issues walizoongelea ni jamaa na wenzake kuja kujenga movie studio ya kisasa maeneo ya Bagamoyo iwe katika level ya ile ya cape town au zilizopo Morocco nafikiri hiyo process bado ilikuwepo ila kwa miaka mingi producers wa Hollywood na bollywood wamekuwa wakiikwepa Tanzania ingawa ina maendeo mazuri sana ya ku shoot na yaliyopo unique badala yake wamekuwa wakienda Kenya,Morocco,South Africa,Madagascar,Namibia,Sychelles na Mauritius.

Kuna movie nimeisahau jina ilitoka 2010 inaonyesha hadi mount kilimanjaro jamaa waliifanyia studio huko namibia.

Mauritius,shelisheli na madagascar wanaingiza hela nyingi sana na ajira kupitia films za hollywood na bollywood zinazofanyika huko.

Kuna movie iitwayo BUCKET LIST starring ni Morgan freeman serengeti imetajwa na walishoot pale ilisaidia sana kutangaza jina na income,movie ya majuzi tu kuhusu lead singer wa kundi la Queens la UK the late Freddie mercury(BOHEMIAN RHAPSODY) iliongeza watalii waliokuja zanzibar kushangaa nyumba aliyozaliwa Freddie a.k.a Farouk pale Unguja

Hivi hawa wabunge wa CCM hawajui hata america katika utalii wa ndani watu huenda sehemu fulani na kushangaa kwamba nyumba hii au gari hili lilitumika katika filamu fulani?

Jamani miaka yote kushuti Tanzania ni gharama kubwa sasa kama haitoshi bungeni wamepitisha kituko.Masharti ya ajabu kabisa ni mengi mno,naambatanisha waraka wa James Gayo ujisomee mwenyewe,embu imagine eti geographic channel waje washuti bongo halafu wapeleke materials yao bodi ya filamu ambayo itayatumia itakavyo
Hii Serikali ya awamu ya tano inatumia mabavu mengi akili kisoda mambo yakiwachachia wanalialia na kudai mabeberu yanawaharibia na kuishia kuitisha makongamano ya kujikosha unafiki

Muswada wa marekebisho ya sheria, kaburi la utalii wa filamu.
Hapa Tanzania ukitamka neno "utalii", harakaharaka akili za watu hukimbilia kwenye mbuga za wanyama, mlima Kilimanjaro labda na fukwe za Zanzibar: Basi!

Hata Serikali inaelekea kufikiria hivyo, ndio maana mkazo kuhusu utalii uko kwenye aina hiyo tu ya utalii. Namna finyu namna hii ya kuuangalia utalii ndiyo inayosababisha tuwe na watalii wachache sana mbali na kuwa na vivutio vingi nadra na vyenye hadhi ya tuzo bora duniani.

Kwa mtazamo wetu finyu namna hii haitushangazi kwa nini mnara mmoja tu huko ufaransa (Eiffel tower) utembelewa na watalii milioni 7 kwa mwaka wakati Tanzania na ujumla wa mamia ya vivutio vyake ipokee watalii milioni 1 tu kwa mwaka!; au kwanini watalii milioni 11 watembelee mapiramidi ya Misri mwaka jana ilihali Tanzania yenye Serengeti, ngorongoro na mlima Kilimanjaro ipokee wageni milioni moja tu.

Nyakati zanabadilika na utalii ni zaidi ya vivutio vya macho!
Nimesoma, pamoja na mapendekezo mengine, mabadiliko ya sheria ya filamu na maigizo kwenye muswada unaosemekana kupelekwa kwa hati ya dharula na kubaki kinywa wazi.

Kwanza kwa nini mswaada wa sheria nane zilizosheheni mambo makubwa yanayohitaji uamuzi wenye hadhari kubwa unapelekwa bungeni kwa hati ya dharula ni swala linalobaki kuwa siri ya waliouandika.
Pamoja na nia njema baadhi ya vipengele vinatuumiza wenyewe.

Sheria hii ikipita kama ilivyo inaenda kuondoa kabisa uwezekano wa mtu au kampuni yoyote ya nje kurekodi filamu hapa nchini.

Utalii wa filamu ni sekta mpya inayoinukia duniani kote na kwa kutambua hilo nchi jirani zimetunga sheria rafiki ili kuvutia makampuni ya nje kuja kutengeneza filamu kwenye nchi zao.

Wakati makampuni makubwa ya sinema yanaendelea kutafuta mandhari mpya za kuvutia, mtindo wa watazamaji wa sinema kutembelea maeneo zilikotengenezwa sinema walizozipenda unashamiri pia.

Imekuwaje basi katika ushindani wa namna hii sisi tunafikiria kufanya mambo yawe magumu kwa mtu yoyote kuja kwetu?

Fikiria kwa mfano (Ntataja vipengelevyenye utata)

(1) Kwamba, kampuni yoyote ya kigeni itakayotumia ardhi ya Tanzania kutengeneza filamu, nzima au kipande, italazimika kukabidhi “Raw Footage” (Picha ghafi moja kwa moja kutoka kwenye kamera kabla haijahaririwa) kwa bodi ya filamu Tanzania.
Hili haliwezekani: Maaslahi ya sinema pote duniani yanahitaji kulindwa na unyeti wa hali ya juu (Hasa kabla ya sinema kuanza kusambazwa)
Kwa filamu zinazotengenezwa kwa kutumia camera za mikanda (film cameras) ndio haiwezekani kabisa maana ili kuona kilichorekodiwa sharti film zipelekwe maabara maalumu kwa usafishaji. Tanzania haina film Lab hata moja, sharti hili litatekelezwaje?

(2) Kwamba, mara baada ya kazi yake ngumu ya kurekodi filamu, mtengenezaji atasaini waraka na kuukabidhi kwa bodi ya filamu ya Tanzania akitoa idhini kwa Serikali ya Tanzania kuitumia filamu yake ipendavyo kwa ajili ya kutangaza vivutio vyake. National Geographic wakisikia sharti hili watacheka tu!

(3) Kwamba bodi ya filamu ndiyo itakayopanga na kuamua idadi ya wataalamu na waigizaji wa kigeni watakaoruhusiwa kuingia nchini. Sijui mantiki ya kipengele hiki, idadi ya wataalamu au waigizaji huamuliwa na watengenezaji kulingana na mahitaji ya filamu, kwa vipi bodi itaamua nani aje na nani asije?
Vipengele hivi vinaletwa wakati Tayari Tanzania inalalamikiwa kuwa na masharti magumu kuliko wenzetu wa Afrika mashariki. Mfano, wakati tozo la kupiga picha nchini Rwanda ni USD 30 na silingi 15,000 nchini Kenya, Tanzania inatoza (Bila kujali kama ni mtu binafsi au Warner Bros) USD 1,000 ndani ya mwezi mmoja na 3,000 kwa wale wanaohitaji kibali ndani ya siku 7! Nimepata kukutana na watu wa nje waliolalamikia kutuma maomba kwa mujibu wa fomu ya kuomba kibali na bado hawakupata majibu yoyote. Taratibu za wageni kuingia na vifaa vya kupigia picha pia ni ngumu kuliko nchi jirani.
Haishangazi basi, kwamba kila wakati, sehemu fulani katika mbuga ya Kenya kuna kampuni, kubwa au ndogo, inatengeneza sinema huku sisi tukiridhika na tuzo inayoitambua Serengeti kama mbuga bora kuliko zote Afrika!
Kuna kampeni inayoendeendelea mitandaoni ikikusanya sahihi ili kuwashinikiza wabunge kutopitisha mapendekezo ya mswada wa sheria nane (8) pasipo majadiliano na tafakuri ya kutosha. Wahamasishaji wanatahadharisha kuwa muswada huo, pamoja na kuathiri utalii wa filamu, utaziathiri azaki zote hata zile za kidini na hata uanzishaji wa kampuni ya kibiashara.
Yeyote anayeguswa na mustakabali wa nchi yetu anakaribishwa kuusoma na hata kuweka sahihi katika kampeni hii:
http://www.changetanzania.org/petitions/ombi-kwa-bunge-na-serikali-kuongeza-muda-kwa-mchakato-wa-muswada-wa-mabadiliko-ya-sheria-mbali-mbali-8-zilizopo-bunge-kwa-hati-ya-dharura?fbclid=IwAR2fL3A-KHX6aO4oEHcuBdfqGDuY19mzhIxmmXhYnBwX3fmkMyPhMgzaxqI
JE ULIJUA... Kwamba sinema hizi zilirekodiwa nchini Kenya?
1. Gun Runners
2. Nowhere in Africa
3. The Constant Gardener
4. Cry Freedom
5. The First Grader
6. Tom Raider
7. Sense 8
8. Born to be Wild
9. The rise and fall of Idi Amin
10. The Ghost and the Darkness
11. Inception
Imeandikwa na James Gayo
 
ndio maana filamu nyingi mtu akiongea kiswahili unajua tu huyu sio mbongo anyway pia lugha inaangazia kwa filamu naop ni utalii
ndipo utajua kwa nini wabunge wenye IQ kubwa hawapendwi na mr dhaifu,ukisikiliza kiswahili cha movie nyingi kinakosewa kabisa hata kipindi kina diamond wanaenda ku shoot south africa walisema masharti kule ni mepesi kupata vibali ni rahisi na accessories hapa ni kizungumkuti sasa rwanda wanachaji dollar 30 hapa dollar 3000 uwe producer mdogo au mkubwa utajiju,yanawaza kodi tu ili ionekane wamevunja rekodi kumbe they cant see the bigger picture
 
Kabla ya yote je lengo lao ni nini?
baba wanawaza mapato ya TRA ionekane wanavunja rekodi ya kikwete...na labda wanataka geographic channel wasije tena kushoot ili tbc 3 aka safari channel ichukue nafasi sijui wanaweza kufanya documentary za wanyama level ya geographic channel? eti aje slyvester stallone kushuti ngorongoro akimaliza akabidhi materials yake bodi ya filamu.hivi yale mabunge ya ccm ukitoa bashe huwaga yanasoma kilichoandikwa kweli au yanasubiri muda uishe yakale nyama na kufukuzia vibinti vya cbe na u dom?
 
Back
Top Bottom