AI na ushahidi wa picha

AI na ushahidi wa picha

Kupitia AI,

Picha zinaelekea kutokua ushahidi wa kutosha mahakamani hata kutoka kwa mtu mwingine tu.

Kipindi cha nyuma ukisema ulikuwepo sehemu fulani au ulishuhudia tukio fulani, halafu ukaonyesha na picha bhasi utaaminika mia kwa mia.

Ila kwasasa, picha ambazo zingeweza kutumika kama ushahidi wa kweli kwa watu wengine zinaweza kubuniwa tu kwa AI kwa ufanisi sana.

Siku za usoni:

Makosa ya kisheria, Kesi za jinai au kesi za kiraia zina hatari kubwa ya kushawishiwa na picha za uongo.

Itakuwa ngumu kuwaaminisha watu kama ulitembelea sehemu fulani hata kama una picha au video fupi.

Mtu akikutumia picha hutaweza tena kuamini muonekano wake mpaka ukutane naye.

Huko mbeleni hata ukitumiwa picha ya lijamaa linamgegeda mke wako, haitakuwa rahisi kuamini.

Hata wataalamu wa picha bado wanaweza kuchanganyiwa.

AI inachanganya uhalisia na uongo,
Nyuso, matukio, au mazingira yanaweza kuundwa na programu za AI kwa usahihi mkubwa kwasasa.

Inahitajika teknolojia ya kugundua picha bandia na uthibitisho kutoka kwa vyanzo vingi.

Hebu niambie wewe unalionaje hili suala la AI na ushahidi wa kipicha linakoelekea...!?
Hilo la 'lijamaa kumgegeda mkeo' umebonyeza sana mpaka umetutoa kwenye reli bhana.
 
AI Ina makosa mengi na bado itakuwa nayo kwa muda mrefu sana.
Kwa mfano Kuna documentary ya jinsi Saddam Hussein alivyo salitiwa na kukamatwa kwenye maficho yake.
Ile video graphics nzuri karibu kila kitu kipo kiwango cha uhalisia kumbe AI generated.
Kosa moja Saddam anaonekana akiandika kwenye karatasi toka kushoto kwenda kulia wakati yeye muarabu alikuwa akiandika kiarabu toka kulia kwenda kushoto. Hilo kosa limekuja kuonesha ni AI siyo video halisia.
 
AI Ina makosa mengi na bado itakuwa nayo kwa muda mrefu sana.
Kwa mfano Kuna documentary ya jinsi Saddam Hussein alivyo salitiwa na kukamatwa kwenye maficho yake.
Ile video graphics nzuri karibu kila kitu kilo kiwango cha uhalisia kumbe AI generated.
Kosa moja Saddam anaonekana akiandika kwenye karatasi toka kushoto kwenda Julia wakati yeye muarabu alikuwa akiandika kiarabu toka kulia kwenda kushoto. Hilo kosa limekuja kuonesha ni AI siyo video halisia.
Hatari mkuu.
Inahitajika akili nyingi sana aisee!
 
Back
Top Bottom