Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,375
Kiukweli kabisa na kwa dhati ya moyo wangu, natoa pongezi za dhati kwa Wazanzibari wote. Kwanza wametimiza haki yao ya kikatiba katika uchaguzi wa Marudio uliofanyika jana. Uchaguzi umefanyika kwa njia ya amani na mpaka sasa utulivu unatamalaki.
Pili natoa pongezi kwa Amir Jeshi Mkuu kwa kuviweka sawa vyombo vya Ulinzi na Usalama ili uchaguzi huo ufanyike kwa amani. Hakika Amir Jeshi Mkuu umetimiza ahadi yako ya kuhakikisha kuwa uchaguzi huo unafanyika kwa njia ya amani na Utulivu.
Kumalizika kwa uchaguzi huu ni kwanzo wa uchaguzi wa 2020. Niwape tu pole wale waliodanganywa na wakadanganyika na sasa wanajuta kwa maamuzi waliyochukua. Ndo hivyo tena. Maji yamemwagika kwenye mchanga. Hakuna jeuri ya kuyazoa tena. Tujipange kwa ajili ya 2020 vinginevyo Bye Bye kwenye ulimwengu wa siasa Tanzania.