Ahsante sana mama mkwe

Ahsante sana mama mkwe

Jokajeusi

JF-Expert Member
Joined
Jun 1, 2018
Posts
6,336
Reaction score
10,896
Ewaa!

Nipo na kibinti kimoja kwa sasa kinasoma mwaka wa kwanza Muhimbili. Ni kibinti kizuri chenye akili sana. Tokea nianze nako mahusiano huu ni mwaka wa pili kwani nilikipata tokea kilivyokuwa kidato cha tano.

Katoto kawatu ndio ilikuwa mara yake ya kwanza kudondoka kwenye mapenzi. Kasivyo na bahati sasa kameangukia kwenye penzi la mhuni yaani Joka baya, Joka dhulumati, Joka Lambalamba, Joka jeusi lenye kunyata nyatu! Nyatu! Likimendea mawindo.

Basi dogo akaiva kama kiazi ulaya. Haimbiwi haambiliki. Unaambiwa shule nzima ya Bwiru Girl ilikuwa inanijua japo mnyama nilikuwa DSM kwa Bashite nikiratibu hama hama ya nyumbu kutoka mara national park kuja Serengeti.

Mrembo akahitimu kidato cha sita nikakaitwa kwenye mahafali. Looh! Sikutarajia kama mimi ni mtu mashuhuri shuleni hapo kumbuka sijawahi tia miguu Mwanza hivyo Bwiru Girls sikuwahi kuifahamu. Lakini watoto wakike hasa wa mchepuo wa PCB walikuwa wakiniita shemu Joka. Shem njoo tupige picha. Nilifarijika sana na jambo hilo lilimfanya mpenzi wangu azidi kujivunia kuwa na mimi.

Nilirudi DSM kuendelea kulegeza vyuma. Mtoto akamaliza shule kwa bahati iliyombaya akapangiwa jeshi Oljoro huko Arusha. Dooh! Jinamizi gani hili. Nilikereka sana kwani tulishapanga akimaliza tuu shule angekuja DSM na mimi nijipigie bila tabu. Lakini ndio hivyo tena.

Tokea mwaka jana dogo hakuwa na aibu kuongea na mimi kwa njia ya simu mbele ya mama yake. Kuna wakati alitumia simu ya mama yake kunipigia. Nilishangaa siku moja mama Mkwe akipokea simu ya mrembo wangu na kuniambia mpenzi wangu hayupo kaenda mjini. Huu ulikuwa mwanzo mpya na Mama mzaa chema.

Siku moja mpenzi wangu alipokuwa Jeshini, nilishangaa kuona namba ya Mama mkwe ikinipigia simu. Nilijiuliza kuna nini mbona si kawaida. Hata hivyo nilipokea na kwa kama kawaida ya Joka kijana mwenye uchangamfu ulithibitishwa TBS nikaongea. Mama Mkwe aliniambia anataka nimsaidie kumchagulia mwanae chuo. Nani angekataa jambo hilo ambalo nililihesabu kama pwenti muhimu sana. Alinitumia elfu sitini. Duuh! Nilimpigia simu nikamwambia mbona ni elfu hamsini akacheka sana jambo lililonifanya joka niwe na tahadhari. Kisha akaniambia hiyo nyingine ni ya huduma mwanangu. Basi nikamwambia nisingeweza kumchaji. Akaniambia nisijali.

Nikakamilisha application. Nikampa mrejesho akanishukuru sana. Unajua mpaka muda huo hakuwahi kuniona. Hanijui zaidi ya kwenye picha. Nilishangaa kuona anavyoniamini kiasi kile. Mtoto akachaguliwa Muhimbili. Mama Mkwe alifurahi sana na kunitunuku laki moja iliyoniacha mdomo wazi. Ndio hivyo tena

Looh! Mtoto akatoka ukuruta na kipara kichwani. Usingeamini mtoto katoka Arusha mpaka DSM kwa joka akidai amemiss dushelele la Joka. Mtoto kajaa nyama kilo mia kunako backbearing. Mnyama nilijimaliza kwa siku mbili then siku ya tatu manzi aliruka kupitia Boeng mpaka Mwanza kwani huko ndiko wazazi wake walipo ijapokuwa wote ni watu kutoka ukanda wa mafisadi.

Baada ya wiki mbili nilipigiwa simu na Mama Mkwe akinitaka niende Mwanza. Looh Salale mbona kiroho kinapwita. Kwa nini kisipwite kuitwa ukweni. Niliongea na Manzi akaniambia nisiwe na hofu kila kitu kipo mahali pake. Mnyama nikachukua Fastjet kufumba na kufumbua Nilijikuta Mwanza huku mbele yangu nikipokelewa na Mpenzi wangu akiwa na mdada mmoja wa hirimu ya Jokate.
Tulizama kwenye usafiri na punde gari ilisimama mbele ya Geti kubwa la kifahari. Nilijikausha kama si mimi huku nikataka kujua maana ya mambo yote yale.

Tuliingia ndani ambapo nilimuona mmama mmoja ambaye moja kwa moja nilijua ni mama mkwe kutokana na kufanana na mpenzi wangu. Unaambiwa shepu lake mfano wake niliukosa. Nili-imagine kwamba mpenzi wangu miaka kumi ijayo atakuwa famba kama mama yake. Nilitabasamu kwa kunong'ona.

Mama Mkwe aliniambia maneno yaliyofanya misuli ya uso wangu isinyae na kulegeza ngozi ya uso wangu kwa bumbuwazi. Joka nimekukabishi mwanangu, Naomba umtunze, umheshimu na kumsitiri. Aliongea huku akinitazama usoni kama mtu anayeniamini kuwa sitamuangusha. Nilitingisha kichwa kwa kuashiria nimemuelewa na kukubali.

Alitoa kiboksi kisha akatoa pete mbili akanipa mimi moja na nyingine akamkabidhi mwanae. Tulivalishana huku kila mmoja akila kiapo cha kutomuacha mwenzake.

Ahsante sana Mama mkwe.
 
Back
Top Bottom