Mapema wiki hii nilimsikia Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Eng. Bonaventure Baya, akisema kusababisha kelele kwenye maeneo ya makazi ya watu ni kosa kisheria. Hakika nilikuwa siujui ukweli huu. Binafsi nakerwa sana na kelele kama muziki wa sauti ya juu (siku hizi bodaboda ni kero kubwa zaidi), kwenye makazi ya watu, hasa nyakati za usiku. Nimefurahi kusikia NEMC imeanza kuchukua hatua kali dhidhi ya watu wanaovunja sheria hii. Keep it up NEMC!