Ahmed Ally: Sowah tulimuondoa kambini Dodoma, tukamrejesha Dar

Ahmed Ally: Sowah tulimuondoa kambini Dodoma, tukamrejesha Dar

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,500
Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally, amezungumzia sakata la mshambuliaji wa klabu hiyo, Jonathan Sowah, na kuthibitisha kuwa walimuondoa kambini Dodoma na kumrejesha Dar es Salaam mara baada ya mchezo dhidi ya Tanzania Prisons.

SnapInsta.to_548907356_17942674176049887_3184539964479995696_n.jpg
Ahmed amesema Sowah kwa sasa yupo nje ya kikosi cha Simba, huku akieleza kuwa klabu bado haijawa tayari kutoa taarifa ya kina kuhusu sababu za uamuzi huo.

“Sowah tulimuondoa kambini na kumrejesha Dar es Salaam. Siwezi kueleza ni kwa nini aliondolewa wala nini kitafuata hadi klabu itakapokuwa tayari kutoa taarifa rasmi kuhusu kilichotokea na hatua zitakazochukuliwa,” amesema Ahmed.

Kutokana na hali hiyo, huenda mshambuliaji huyo akaukosa mchezo wa Dabi ya Kariakoo dhidi ya Yanga utakaopigwa Machi 1, 2026 katika dimba la Amaan, Zanzibar.
 
Tunaomba simba wamalize tofauti zao na mchezaji Sowah! ili isiwe chanzo ya kisingizio kuwa fulani hakuwepo. Depu hatacheka na kima siku hiyo.
 
Back
Top Bottom