Naunga mkono hoja.Najua wengi itakua ngumu kunielewa.
Huyu jamaa amewekwa pale Ili kuwapumbaza wanasimba na wanasimba bila kuwa na uelewa wanamuona kama ni Mtu wa maana sana. Hivi hamjiulizi kila siku anaropoka vitu nje ya uwanja ila ndani ya uwanja timu inachofanya nadhani mnakijua halafu baada ya mchezo analeta maneno mengine ya uongo uongo na wanasimba mnaridhika kabisa.
Huyu jamaa ni chawa wa Mo na anafanya hivi Ili kuwapoteza maboya halafu wengi mnamsema Mangungu wakati Mangungu pale yupo kama picha tu. Nina ushahidi 100% anafurahia kinachoendelea Simba huku anaingiza pesa.
Ahmed Ally ni Yanga damu na mtateseka sana sababu hamtapata mbadala, Ahmed anajua kuzima maneno ya mashabiki.
Ni mental case hio.Anavyozungumza kama mwanamke huwa ninahisi aibu sana.
Jamaa anaonekana kichwani ni mweupe sana.
Ally Kamwe anajua sana kujieleza kwa utulivu.
Hawa vijana awali walikuwa wachambuzi wazuri wa michezo pale Azam Media, ila sijui ni kitu gani kikemkuta Ahmed Ally maana anazungumza kama kachanganyikiwa hivi.
Sio kama kachanganyikiwa ila kachanganyikiwa kabisa yule.Anavyozungumza kama mwanamke huwa ninahisi aibu sana.
Jamaa anaonekana kichwani ni mweupe sana.
Ally Kamwe anajua sana kujieleza kwa utulivu.
Hawa vijana awali walikuwa wachambuzi wazuri wa michezo pale Azam Media, ila sijui ni kitu gani kikemkuta Ahmed Ally maana anazungumza kama kachanganyikiwa hivi.
Mangungu mnamtishia kumtoa meno unataka aje kufanya nini kwani yeye hajipendi?Ahmed Ally si tatizo Simba. Jamaa ni mfano wa kuigwa kwa wanaojifunza kazi ya usemaji wa timu. Anajua haswa kuhamasisha mashabiki kujaa uwanjani.
Tatizo la Simba ni wachezaji kukosa philosophy , morali na kushindwa kucheza kwa fomesheni hivyo kupata matokeo mabovu.
benchi la ufundi Simba halina uwezo wa kimbinu kufundisha wachezaji .
Rais wa Yanga Eng Hersi kila mechi yuko uwanjani, kwa Simba ni tofauti , kiongozi wao hatumuoni uwanjani kila mechi.
Simba imeporomoka si sahihi kumuangushia jumba bovu Ahmed Ally.
[emoji23][emoji23][emoji23]Huyo jamaa mwanzoni alikuwa yupo vozuri sana lakini siku hizi sijui kakumbwa na kitu gani. Jamaa kawa kituko sana. Mwambieni aangalie clip zake za mwanzo wakati anaanza kazi Simba na hata akiwa anafanya kazi Azam halafu alinganishe na hizi za hivi karibuni halafu ajirekebishe. Na kikubwa ajue mipaka ya kazi yake. Vinginevyo huko anakoelekea atakuwa kituko zaidi.