Ahly Athletic Club vs Dar Yanga Africam | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ahly Athletic Club vs Dar Yanga Africam

Discussion in 'Sports' started by Lucchese DeCavalcante, Mar 14, 2009.

 1. Lucchese DeCavalcante

  Lucchese DeCavalcante JF-Expert Member

  #1
  Mar 14, 2009
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 5,473
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Wana JF na wapenzi wa soka Tanzania na kwingineko duniani kesho ile mechi ya Yanga na El Ahly au National Athletic Club ya Egypt ndio itakuwa inapigwa mida ya saa 1 jioni kwa saa za Afrika mashariki. Kwa mlioko Misri au wenye uwezo wa kuona mechi hii live muwe mnatuupdate hapo kesho mechi itakapoaanza.

  Je wajua;


  1. Mechi itapigwa kwenye dimba la Cairo international Stadium lenye uwezo wa kuchukua watu 74,100. Uwanja huo upo katika kitongoji cha Nasr ndani ya jiji la Cairo na ulifunguliwa mwaka 1960.

   Mafanikio yao katika mashindano mbali mbali ni kama ifuatavyo;
   Egyptian League (31) (Egyptian Record): 1948/49, 1949/50, 1950/51, 1952/53, 1953/54, 1955/56, 1956/57, 1957/58 , 1958/59, 1960/61, 1961/62, 1974/75, 1975/76, 1976/77, 1978/79, 1979/80, 1980/81, 1981/82, 1984/85, 1985/86, 1986/87, 1988/89, 1993/94, 1994/95, 1995/96, 1996/97, 1997/98, 1998/99, 1999/00, 2004/05, 2005/06


   Egyptian Soccer Cup (34) (Egyptian Record): 1923/24, 1924/25, 1926/27, 1927/28, 1929/30, 1930/31, 1936/37, 1939/40, 1941/42, 1942/43, 1944/45, 1945/46, 1946/47, 1948/49, 1949/50, 1950/51, 1952/53, 1955/56, 1957/58, 1960/61, 1965/66, 1977/78, 1980/81, 1982/83, 1983/84, 1984/85, 1988/89, 1990/91, 1991/92, 1992/93, 1995/96, 2000/01, 2002/03, 2005/06

   Egyptian Super Cup (3) (Egyptian Record): 2003, 2005, 2006

   Sultan Hussein Cup (7): 1922/23, 1923/24, 1925/26, 1926/27, 1928/29, 1930/31, 1938/39

   Cairo League (5): 1938/39, 1941/42, 1942/43, 1947/48, 1949/50

   United Arab Republic League (1): 1960/61

   African Championships


   CAF Champions League (5) (Current Champion, African Record):
   1982, 1987, 2001, 2005, 2006

   African Cup Winner's Cup (4) (African Record): 1984,1985,1986, 1993


   CAF Super Cup (2) (Current Champion, African Record):2002, 2006, 2007

   Medalla de bronce en Japón:2006

   Afro-Asian Cup (1):
   1989

   Century Cup (Al-Ahly vs. Real Madrid) (1): 2001

   Arab Champions Cup (1): 1996

   Arab Cup Winners Cup (1):: 1995

   Arab Super Cup (2): 1997, 1998

   Kocha wao ni Manuel José de Jesus ambaye ni raia wa URENO, timu kapteni niEmad Meteeb na raisi wa club ni Hassan Hamdy mbaye yupo madarakani toka Mei 2002.

   Timu yao ya sasa ina wachezaji wafuatao;


   1

   POR
   Essam El-Hadary

   2

   DEF
   Islam El-Shater

   4

   DEF
   Emad El-Nahhas

   5

   DEF
   Ahmad El-Sayed

   6

   DEF
   Ahmad Sedik

   7

   DEF
   Shady Mohamed (capitán)


   8

   MED
   Mohamed Barakat


   9

   DEL
   Emad Moteab

   10

   DEL
   Ahmed Belal

   11

   MED
   Tarek El-Saiid

   12

   DEF
   Sebastiao Gilberto


   14

   MED
   Hassan Mostafa

   15

   DEF
   Abdulilah Galal

   17

   MED
   Anis Boujelbene

   18

   DEL
   Osama Hosny


   No.

   Posición
   Jugador

   19

   DEL
   Akwety Mensah

   20

   MED
   Mohamed Shawky

   21

   MED
   Mohamed Abdullah

   22

   MED
   Mohamed Aboutrika

   23

   DEL
   Flávio Amado


   24

   MED
   Ahmad Hassan Stakoza

   25

   MED
   Hossam Ashour

   26

   DEF
   Wael Gomaa

   27

   POR
   Amir AbdulHamid

   28

   POR
   Nader El-Sayed

   29

   DEF
   Ahmad Shedid Qinawi

   30

   DEF
   Mohamed Sedik

   31

   DEF
   Ahmed Adel

   32

   MED
   Haitham Al Fazani

   33

   DEL
   AbdelHameed Hassan

   Haya wanajangwani na watanzania kwa ujumla kesho kazi tunayo na tunaomba Mungu tuweze kuwaangusha vinara hawa wa soka Afrika na kuweka historia mpya ya soka Tanzania na Afrika.

   Mungu ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika
   
 2. Lucchese DeCavalcante

  Lucchese DeCavalcante JF-Expert Member

  #2
  Mar 14, 2009
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 5,473
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Jamaa wanatugwaya sana cheki hii habari hapo chini,

  Arrival of Tapes about Young Africans

  El-Ahly's technical staff managed to get a set of videotapes of Tanzanian Young Africans in order to identify their strengths and weaknesses before facing them in the round of 32 of the African Champions League.

  El-Ahly Assistant coach, Captain Hossam El-Badri made great efforts in order to obtain these tapes in coordination with the Egyptian ambassador in Tanzania.

  the tapes containing games for the Tanzanian team against the champion of Comoros in the preliminary round of this tournament, as well as some matches in the Tanzanian league.

  On the other hand, the date of arrival of the Tanzanian team to Cairo has not been set yet in order to arrange their accommodation, but it is expected to be known within the next few days as the match will be held at the Cairo Stadium next Sunday, the 15th of March.

  It should be noted that Young Africans had qualified to this round after their win over the champion of Comoros in the preliminary round 14-1 on aggregate!
   
 3. Lucchese DeCavalcante

  Lucchese DeCavalcante JF-Expert Member

  #3
  Mar 14, 2009
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 5,473
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Current Egyptian League Table
  # Team Pts
  1. Al Ahly 45
  2. Ennpi 39
  3. Petrojet 39
  4. Ismaily 38
  5. Hidood 36
   
 4. Lucchese DeCavalcante

  Lucchese DeCavalcante JF-Expert Member

  #4
  Mar 14, 2009
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 5,473
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Last match kwenye ligi yao wamecheza March 10 na matokeo ni Olympi 0-3 Al Ahly

  Kikosi cha Al Ahly kilikuwa;


  Ramzy Saleh GK
  Ahmed Belal (C)
  Ahmed Fathy
  Moataz Eino
  Flavio
  Hussam Ashour
  Wael Gomaa
  Mohamed Samir
  Ahmed El Sayed
  Ahmed Hassan
  Sayed Moawad


  Wafungaji ni;
  21' [1-0] Ahmed Belal
  60' [2-0] Ahmed Hassan
  88' [3-0] Moataz Eino
   
 5. Lucchese DeCavalcante

  Lucchese DeCavalcante JF-Expert Member

  #5
  Mar 14, 2009
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 5,473
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Kikosi cha wapiganaji cha Yanga kilichopo Misri kinajumuisha wachezaji wafuatao;
  Juma Kaseja, Obren Circkovic, Shadrack Nsajigwa, Fred Mbuna, Amir Maftah, Nurdin Bakari, George Owino, Nadir Haroub, Wisdom Ndhlovu, Geoffrey Bonny, Abdi Kassim, Shamte Ally, Athumani Iddi, Mike Baraza, Ben Mwalala, Boniface Ambani, Mrisho Ngassa, Jerry Tegete, Kiggi Makassy na Vincent Barnabas.

  Mechi hii tunaisubiri kwa hamu hapo kesho
   
 6. Lucchese DeCavalcante

  Lucchese DeCavalcante JF-Expert Member

  #6
  Mar 14, 2009
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 5,473
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  YANGA ambayo iliwasili Cairo Alhamisi na kupata mapokezi makubwa kutoka kwa maofisa wa ubalozi na Watanzania waishio nchini humo inakabiliwa na kibarua kigumu leo usiku itakapoikabili, Al Ahly, mabingwa watetezi wa Afrika katika mchezo wa kwanza wa raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa.


  Wawakilishi hao pekee wa Tanzania katika michuano ya klabu Afrika ambao wamefadhiliwa na ubalozi wa Tanzania mjini Cairo kwa chakula na huduma nyingine muhimu wanaingia uwanjani wakiwa na dhamira ya kufuta uteja na rekodi mbaya dhidi ya Waarabu.


  Al Ahly imeanza moja kwa moja raundi ya kwanza kutokana na kuwa ni bingwa mtetezi. Mchezo huo utafanyika kwenye Uwanja wa Cairo.


  Hata hivyo, timu hiyo iliyoiondoa Etoile d'Or Mirontsy ya Comoro kwa mabao 14-1 na inayoundwa na wachezaji wengi wa Taifa Stars iliyokuwa ikishiriki michuano ya Afrika nchini Ivory Coast mwezi huu, wachezaji na viongozi wao wameahidi kupigana kufa au kupona ili kubadili historia ya soka Afrika.


  Nyota wake, Mkenya, Boniface Ambani aliyekuwa China kwa majaribio ya soka la kulipwa ataisaidiwa katika mchezo huo na Mrisho Ngassa, Ben Mwalala, Jerson Tegete na Mike Barasa katika ushambuliaji wakisaka mabao, ingawa wana kibarua kigumu cha kuwapita mabeki na ukuta mgumu wa Ahly.


  Pia, kwa upande wa ulinzi, Shadrack Nsajigwa, Nadir Haroub 'Cannavaro', Nurdin Bakari wana jukumu zito la kumlinda kipa Juma Kaseja au Mserbia Obren Curkovic, ambao mmoja kati yao ndiye atayekuwa katikati ya milingoti mitatu.


  Katika kiungo wanatarajiwa Godfrey Bonny, Athuman Idd 'Chuji', wachezaji wa Stars ambao waliondoka wakiahidi kucheza kwa bidii na maarifa ili kulinda heshima ya nchi yao.


  Tangu kuwasili Cairo, baadhi ya wachezaji wa Yanga, akiwamo Mrisho Ngassa wamekuwa gumzo, wakifuatiliwa pia na vyombo vya habari vya hapa ambavyo vinaisifu timu yao, huku kocha Dusan Kondic akiwajibu wanahabari kuwa wasubiri kuiona uwanjani timu yake ambayo imejiandaa vizuri kwa mchezo huo.


  Kondic ameahidi kuwa vijana wake watacheza kwa bidii na maarifa kama alivyowaelekeza ili kuiondoa Ahly katika michuano ya Afrika mwaka huu
   
 7. Lucchese DeCavalcante

  Lucchese DeCavalcante JF-Expert Member

  #7
  Mar 14, 2009
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 5,473
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  MATOKEO YA MECHI ZA JANA NA LEO CAF Champions League 2009
  Round of 32
  Kampala City Council - Uganda 2 : 1 Supersport United - South Africa

  51' Robert Ssentongo 1-0
  47' Anthony Laffor 1-1
  58' Brian Omony 2-1


  Al-ittihad - Libya 1 : 1 Al Merrikh - Sudan
  47' Mohamed Zubya 1-0
  74' Haitham Tambal 1-1

  Ajax Cape Town - South Africa 3 : 2 Monomotapa United - Zimbabwe
  Primeiro de Agosto - Angola 0 : 1 Canon Yaondi - Cameroon
  ASEC Abidjan - Ivory Coast 2 : 0 Etoile Filante de Ouagadougou - Burkina Faso
  E.S. Sahel - Tunisia 2 : 1 ASO Chlef - Algeria
   
 8. S

  Sahiba JF-Expert Member

  #8
  Mar 14, 2009
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 303
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Lahaula nikiifikiria hiyo aibu ya kesho hadi machozi yananitoka kweli loyality lakini hii ni best team in Africa.Angalau simba wana historia kule kwao lakini yanga,poleni.Mfanyakazi mwenzangu hapa raia wa Misri anasema wametutayarishia TANO tu sio nyingi kwa huruma waliyo nayo na sina sababu ya kutomuamini kwa sababu mpira ni uwezo na uwezo hata wakitaka nane wanao.Sasa tusubiri hiyo kesho.

  SAHIBA.
   
 9. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #9
  Mar 15, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  braza mm nipo Misri hapa lakini si cairo, nipo mji mbali kidogo wa Alexandria, niseme ukweli nawafahamu Ahly na hawa jamaa wanawashabiki wengi sana kuliko timu yoyote hapa Misri, uwezo wanao kweli japo marefa huwabeba wakti fulani, Yanga wana mlima wa kupanda japo mpira unadunda.
   
 10. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #10
  Mar 15, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Hata hivyo udhaifu wa Ahly kwa namna ninavyo waona katika mechi zao hapa, kama yanga wataweza, mchezo wa kukaba mtu na mtu, close marking. Timu zinazoifunga Ahly hapa Misri nimeona sana wanatumia mbinu hii ambayo inawafanya Ahly wapoteze uwezo wa kumiliki mpira na utawaona wana panic na kuchezacheza rafu, sijui kama Yanga wanalijua hilo au ndo hawakuta kutuuliza, mm hofu yangu hawa wapenzi wa Ahly ambao tupo class moja weshaanza kunifanyia tashtiti zao wakininyooshea vidoke vinne,vitatu na wengine viwili. Na inatisha kwa kuwa uwezo huo wanao, timu yao nzuri sapoti yao kubwa sana na wanacheza nyumbani.
   
 11. Lucchese DeCavalcante

  Lucchese DeCavalcante JF-Expert Member

  #11
  Mar 15, 2009
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 5,473
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Mimi natabiri mechi itaisha kwa sie Yanga kushinda 2-1
   
 12. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #12
  Mar 15, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  kama itokea yanga akapata matokeo hayo basi uwezekano wa kusonga mbele upo.....ila mimi ningependa apigwe kama 3-0 au zaidi, maana sipendi kuwa mnafiki siwa pendi yanga kama manu vile...halafu hapa ningependa apate ushindi wa 2-1 au sare yaani hapo nitakuwa nimefurahi kweli kweli....lkn watani yanga mwaka huu ana kikosi kizuri kuliko miaka yote niliyopata kuiona yanga...naomba mfungwe
   
 13. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #13
  Mar 15, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,120
  Likes Received: 615
  Trophy Points: 280
  Al Ahly 3 - 1 Yanga
   
 14. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #14
  Mar 15, 2009
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Tuna msala, ikiwezekana ni kuambiana ukweli jamaa wazuri the only way to beat them is to attack na kudefend, total football tu itatuokoa lkn tukijilinda ni nyingi twapigwa. All the best Yanga
   
 15. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #15
  Mar 15, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  mm nna presha jamani, sjui itakuwaje.....jamaa hapa Misri haweshi kunionyesha vidole kuanzia vinne na kuendelea.
   
 16. Mr Kiroboto

  Mr Kiroboto JF-Expert Member

  #16
  Mar 15, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 321
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  vp game itaoneshwa?kama itaoneshwa,kwa sie tuliopo ughaibuni twaweza ichungulia wapi?
  msaada kwenye tuta!
   
 17. S

  Sahiba JF-Expert Member

  #17
  Mar 15, 2009
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 303
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Al Ahly 5-1 Yanga
   
 18. S

  Sahiba JF-Expert Member

  #18
  Mar 15, 2009
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 303
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wenzetu mpira kazi sio ubishoo.
   
 19. A

  Alpha JF-Expert Member

  #19
  Mar 15, 2009
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 614
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Todays match 1-1


  Return Leg: 2-1 Yanga

  Yanga advance 3-2 on aggregate :)
   
 20. A

  Amwanga JF-Expert Member

  #20
  Mar 15, 2009
  Joined: Jan 11, 2009
  Messages: 294
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Yanga leo wanaua washikaji, kwani hiyo ni taifa star inacheza na katimu ka misiri, labda wapeleke majini uwanjani, manake waarabu kwa ushirikina wapo juu
   
Loading...