Uchaguzi 2020 Ahera ya baada ya uchaguzi 2020

The Dark Father

JF-Expert Member
Oct 9, 2017
1,144
1,399
Nimesahau, nadhani. Hivi lini watanzania tumedai haki zetu?
Lini wahusika tumewahi kupambana?

Watanzania lini tumefungua midomo yetu, tukatoka nje kwetu na kwenda kudai haki zetu?
Au hiyo kazi ya Zitto, Lissu na Fatma Karume watudaie?

Watanzania, inapitishwa kanuni kandamizi, wadau wanalalamika twitter huku wakimsubiri Lissu awasemee. Vyombo vya habari vyote eti vinaogopa hata kufungua class lawsuit ya madai halali ya kulinda uhuru wao. Eti na wao ma-corporation washika industry wanaogopa kusimama kwa ajili ya haki zao.

Wakulima wanatapeliwa hawajiungi kuchukua hatua, bali wanamsikilizia Zitto awalalamikie kwa niaba huku wao wakibaki kufyonza fyonza kwenye vijiwe vya kahawa. Watanzania wanavunjiwa maeneo yao halafu wanabet labda atakuja rais mwingine wa kuwapa haki zao.

Afu tunaitwa wanyonge, basi unakuta tunakenua tuki-find pride in our victimhood. Utakuta, "baba Rais baba, nisaidie baba... Wewe mpenda wanyonge... Nisaidie baba. Ikikupendeza baba, nigaie hata kiduchu ile haki yangu baba... Ileee haki yangu ya mababu zangu, ukijisikia unisaidie baba...."

Ikishindikana, labda one day Sugu na Mdee watatupa hizo haki.

SASA (in Lissu's Voice) mimi ninaona Watanzania tunyooshwe hii miaka mitano (kama itakuwa hivyo kweli, maana...) mpaka tukumbuke hii nchi ni ya nani haswa. Ili tujue namna ya kupambana wenyewe bila ya kuwatia ulemavu watu wengine na kuwaua wakipigania haki ambazo tulipaswa tuzipiganie wenyewe.

Kama sasa hapa tumekaa tunatoa macho tunasubiri mtu mmoja aamue watu milioni 58 aturuhusu tuchati.

Watanzania hatuna haja ya kuhamasishwa tena. Acha tutawaliwe tena na safari hii na mtu mmoja tu! Acha tukajae uwanjani akiapishwa ili tumuombe ikimpendeza atupe ruhusa ya kuishi. Tusisahau kumuombea atuswage maana sisi tu mang'ombe kwa msukuma yule.
Ili siku ifike tupigwe sisi risasi kwa ajili ya nchi yetu badala ya mwanakondoo mmoja tunayemuona ana kiherehere.

Mabibi na Mabwana, tukiwa tunasubiri kupata uhuru kutoka kwa wakoloni weusi, nawasalimu kwa jina lake.
 
Yaani tunasubiri mbuzi mmoja aamue kuturuhusu tu video call wanawake zetu.

Tumetikiswa tumetikisika. Tumewapa ruksa. Tumewazoesha. Tutapata tunachostahili.
 
Back
Top Bottom