Ahadi za magufuli

Naface

Member
May 27, 2015
66
65
Ahadi Muhimu za Dr J.P.M kwa Watanzania wote :

1.Elimu bure kuanzia Darasa la kwanza hadi kidato cha 4.

2.Wanawake kuwezeshwa mikopo kwa ajili ya Miradi ya maendeleo.

3.Vijana kuwezeshwa mikopo kwa ajili ya Miradi mbalimbali ya maendeleo.

4.Unafuu wa bei kwa Vifaa vya Ujenzi kama Cement, ambapo kiwanda kipya cha cement kilichopo MTWARA kufunguliwa karibuni.

5.Viwanda mbalimbali vya kisasa kujengwa,hivo Kuongeza Ajira kwa Watanzania..

6.Upatikanaji wa dawa zote kwa hospitali za serikali.

7.Kuondoa Ushuru kwa wafanyabiashara wadogowadogo kama Mama Ntilie,Bodaboda.

8.Kuanzishwa Mahakama Maalumu kuwashughulikia wabadhilifu wa pesa za Umma (Mafisadi).

9.Wakulima kupewa kipaumbele wakati wa kuuza mazao na pia Wafugaji kuzingatiwa haki zao.

10.Wanafunzi wa vyuo kupata mikopo katika muda muafaka.

11.Barabara na Madaraja ya kisasa kujengwa.

Hayo yote kwa asilimia mia Ataweza mana hua ni Mtekelezaji kwa Ahadi Zake.
Tanzania Mpya ya Magufuli,
Zinatekelezeka,tutakuchagua
#HAPAKAZITU!
 
Back
Top Bottom