Ahadi za diwani na mbunge wangu vipi?

Mbugi

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
1,488
257
Naomba kupitia jukwa (jf ) kumbusha mbunge na diwani wangu juu ya ahadi zao ukuachana na ahadi za mh Rais (jk) kwa kuzingatia kuwa zilikuwa za kitaifa zaidi na za jumla jumla.

Mimi ni mkazi wa kata ya Iganzo, mtaa wa Iganzo, Jiji la Mbeya, Mh. diwani wangu anaitwa F. Uswege na mbunge wangu ni mh. SUGU, NAPENDA kwa kutumia jukwa hili niwakumbushe juu ya ahadi walizotoa wakati wa kuomba ridhaa ya uwakilishi kwetu, nianze na ahadi za mh. diwani wangu kama ifuatavyo;

  1. Alliahidi kutumika zaidi kwa wananchi wake kwa kuitwa "Mtumishi" na wala si "Mheshimiwa"
  2. Kuondoa kero kwa wananchi kwa kufuta michango yote ya shule na nk, kwa kutumia raslimali iliyopo ndani ya kata ya Iganzo kama kifusi kama mbadala wa michango hiyo,
  3. Kuwalipia ada karo za shule wanafunzi wote Yatima katika kata ya Iganzo, Hususani secondary ya Iganzo kwa kutumia wafadhili kikiwemo chama.
  4. kuboresha barabara za mitaa
  5. kutoa taarifa ya maslahi yake kama diwani yaliyopo kutoka halmashauri kwa kila mwezi, na taarifa ya ruzuku ikiwepo mauzo ya kifusi cha kujenga barabara kwa jiji kwa ujumla wake (ambapo kila tripu hulipwa shs 30,000)
  6. kujenga vyumba vya madarasa kwa kuchangisha wafadhili mbalimbali ikiwepo mchango mdogo kwa wananchi wake wa shs 2000/= na si zaidi.
  7. kufanya mikutano ya hadhara kia mwezi kwa minajili ya kutoa taarifa kwa wananchi juu ya mipango ya maendeleo.
  8. kusimamia kwa karibu mgawanyo wa raslimali kutoa halmashauri.
Sisi wananchi wako tunataka kufahamu nini kimejili kwa ukimya unaoemndelea?, tunataka kujua umekwama wapi? nini tufanye kujinasua?

Mh.Sana Mbunge wangu SuguAHADI ZAKO KWETU HIZI HAPA

  1. kuendeleza mapambano ya kuimarisha mpango mzima wa elimu kwa wana Mbeya (leo watoto wamefaulu hawana shule za kwenda) kwa sababu madarasa hakuna.
  2. ujenzi wa lami kwa barabara za ndani ya jiji mbeya barabara hazipitiki mambo ni bora liende kila kukicha tunasikia mwenzetu na mashairi
  3. hosptali za kata ktk maana ya zahanati hatuoni mchango wako tunasikia hapa na pale kama waliotukutagulia, kuwa umepeleka msaada KATA YA IZIWA, NSALAGA, ITEZI, wa kujenga bwawa la samaki, Pia umepeleka hosptal ya rufaa VITANDA vya wagonjwa katika wodi wa wazazi Meta na vitanda pale rufaa, umejenga madarasa sec ya uyole, umechangia wahanga wa mafuriko ikuti, na pia umewawezesha waheshimiwa madiwani wako kwa ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa kata 12 ikiwepo ya kwangu tafadhali kama mpiga kura wako naomba uweze kutoa publically mchanganua na namna michango hiyo ilivyowafikia wananchi husika ili kukanusha uvumi kwamba mbeya uongo huvuma zaidi ya ukweli.
  4. uliahidi ukipata madaraka kuuza gari ya mkuu wa mkoa hebu tupe umekwama wapi maana naona Mh kandoro bado anayo V8 na wewe pia umeonekana kuungana naye kwa kununua aina inayofanana kwa namana fulani yaani (BMW vogs) tupe hiyo yako inauhusiano gani na kupambana na hali ya kuepuka matumizi starehe zaidi
  5. kufuatilia ajira kwa TBL na ikiwezekana kuhakikisha wafanyakazi wanaotoka kaskazini wanarudishwa kwao ili sie vijana wenzio tupate ajira.
Mafanikio niliyoyaona
  1. KUPIGA MAWE VIONGOZI AHADI IMETIMIA
  2. MAANDAMANO NIMEKUBALI, NI LINI SASA TUTANDAMANA KUPATA WATOTO WETU WAENDE TBL, NA NI LINI KWENDA SEC.NK
 
Back
Top Bottom