GE2025 Ahadi za CCM zinavyobua mjadala

GE2025 Ahadi za CCM zinavyobua mjadala

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Parabolic

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Posts
2,743
Reaction score
2,601
CCM-25-1024x726.jpg

Tangu Chama cha Mapinduzi (CCM) kilipozindua kampeni zake za uchaguzi mkuu wa Oktoba 28, 2025 katika uwanka wa Tanganyika Packers Kawe jijini Dar es Salaam, kumekuwa na mijadala kuhusu ahadi zinazotolewa na mgombea urais wa chama hicho, Samia Suluhu Hassan.

Miongoni mwa ahadi zilizotolewa na Samia ni pamoja na kuzindua awamu ya majaribio ya mpango wa Bima ya Afya kwa Wote, ikiwalenga awali wazee, watoto, wajawazito, na watu wenye ulemavu, huku gharama za matibabu zikifadhiliwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.

Serikali itagharamia kikamilifu matibabu na vipimo vya uchunguzi kwa wananchi wasioweza kumudu matibabu ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza, ikiwa ni pamoja na saratani, figo, moyo, kisukari, mifupa, na magonjwa ya neva.

Kuajiri wafanyakazi 5,000 wapya wa afya, ikiwemo wauguzi na wauguzi wa mama, ndani ya siku 100. Kuzuia hospitali yoyote kushikilia maiti kwa familia hata kama bili za matibabu hazijalipwa.

Kuandaa mkakati wa kisayansi ili kuhakikisha kila mwanafunzi wa darasa la tatu anaweza kusoma, kuandika, na kufanya hesabu kwa ujasiri, ikiwemo kuajiri walimu 7,000 wapya wa sayansi na hisabati.

Kurekebisha na kutilia mkazo sekta zisizo rasmi, ikiwa ni pamoja na wafanyakazi wa lishe, waendeshaji bodaboda, madereva wa bajaji, na wajasiriamali wadogo, ili waweze kupata huduma za serikali na kushirikiana na mamlaka.

Kuzindua mpango na waajiri, Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (VETA), na vyuo vikuu kwa wanafunzi wa VETA kufanya mafunzo ya kiwanda. Kuongeza matumizi ya nishati safi ili kupunguza utegemezi wa kuni na makaa ya mawe.

Kutoa TZS bilioni 200 kusaidia upatikanaji wa mtaji kwa biashara ndogo na za kati, kuanzisha programu za viwanda vya mtaa ili kuunda ajira, na kujenga gridi ya taifa ya maji.

Kuweka mifumo ya uwajibikaji ambapo mawaziri, makatibu wa mikoa, na watendaji wa serikali wataripoti na kujibu maswali ya wananchi kwa njia ya kidigitali bila malipo. Kuendelea na mashauriano na wadau wa kisiasa, mashirika ya kiraia, na sekta binafsi kwa kuunda kamati ya kuanzisha mazungumzo ya maridhiano na kuandaa msingi wa mchakato mpya wa katiba.

Utata wa ahadi

Kumekuwa na utata wa utekelezaji wa ahadi hizo tena ndani ya siku 100.
Watanzania wanajiuliza kama ahadi hizi zinawezekana kiutendaji na kifedha. Je, kwa nini zilishinmdikana kutekelezwa kwa miaka minne ambayo Samia amekuwa madarakani kama Rais wa Jamhuri ya Muungano?

Ahadi ya kutolipia maiti hospitali

Katika ahadi zake, Samia alisema atakapochaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano, atahakikisha wananchgi hawatozwi fedha za kuchukua maiti za wapenda wao waliofia hospitali.

Licha ya suala hilo kuzua mijadala mingi miaka iliyopita, lakini Serikali kupitia iliyokuwa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ilishatoa mwongozo wa suala hilo.

Katika waraka uliotolewa Oktoba 4, 2021na aliyekuwa Katibu wa Afya katika wizara hiyo, Profesa Abel Makubi ulikataza hospiali kuzuia maiti.

Ukurasa wa 4 unasema:

“3.1.2 Iwapo marehemu alikuwa anahudumiwa kwa msamaha wa matibabu, ndugu waruhusiwe kuchukua mwili wa marehemu.

3.1.3 Iwapo marehemu alikuwa anachangia gharama za matibabu na mauti yamemfika akiwa na deni la gharama za matibabu, ndugu aruhusiwe kuchukua mwili baada ya kufanya malipo.

3.1.4 Iwapo ndugu wa marehemu hawatakuwa na uwezo wa kulipa deni pale mgonjwa atakapokuwa amefariki, ndugu wataingia makubaliano ya maandishi na kituo cha kutolea huduma ya namna ya kulipa deni na waruhusiwe kuchukua mwili.”

Ununuzi wa matrekta milioni 10
Akizungumza Agosti 31, 2025, mbele ya maelfu ya wananchi wilayani Chemba Mkoa wa Dodoma, Samia aliahidi mageuzi makubwa katika sekta ya kilimo kwa kuhakikisha serikali inanunua matrekta milioni 10 pamoja na zana nyingine za kisasa ndani ya kipindi cha miaka mitano.

Alisema mpango huo ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi, wenye lengo la kumrahisishia mkulima upatikanaji wa huduma bora za kilimo na kuongeza tija katika uzalishaji.

Kwa mujibu wake, serikali itahakikisha wakulima wanalimiwa kwa gharama nafuu zaidi kuliko sekta binafsi. “Kwa ekari moja, baadhi ya watu binafsi wanatoza hadi shilingi 80,000, na baada ya serikali kuanzisha vituo vya zana gharama zimeanza kushuka hadi shilingi 40,000. Lakini kwa bei yoyote sekta binafsi itakayowatoza wakulima, serikali itatoza nusu ya bei hiyo,” amesisitiza.

Hata hivyo, hoja ya kununua matrekta milioni 10, imeibua mjadala, ikielezwa kuwa idadi hiyo ni kubwa mno. Wakati ahadi hiyo ikitolewa, Ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2025 hadi 2030 imeahidi kutoa matrekta 10,000 kwa mkopo kwa wakulima.

Kwa mujibu wa mtandao wa Indexbox, Uzalishaji wa dunia uliongezeka kwa haraka sana mwaka 2023 – kiasi hicho kiliongezeka kwa takriban 13 % ikilinganishwa na mwaka 2022

Mwaka 2021 ndiyo ulikuwa kilele cha uzalishaji, ulifikia kiasi cha takriban 5.1 milioni za matrekta

2013–2024, uzalishaji umeongeza kwa wastani wa takriban asilimia 2.0 kila mwaka. Baada ya kilele cha 2021, uzalishaji uliendelea kushuka kidogo kwenye miaka ya 2022–2024.

Kwa takwimu hizo, bado haijajulikana Samia atatoa wapi matrekta milioni 10.

Isitoshe, gharama ya kununua milioni 10 kwa bei wastani $30,000 (sawa na Sh75, milioni) ingefikia $300 bilioni (zaidi ya Sh750.7 trilioni), zaidi ya GDP ya Tanzania inayokadiriwa kufikia $89 bilioni (zaidi ya Sh222.7 trilioni).

Kutenga Sh200 bilioni za mitaji ya biashara

Katika ahadi hizo pia, Samia aliahidi kutoa Sh. bilioni 200 kusaidia upatikanaji wa mtaji kwa biashara ndogo na za kati, kuanzisha programu za viwanda vya mtaa ili kuunda ajira, na kujenga gridi ya taifa ya maji.

Akizungumza kwa njia ya mtandao Agosti 29, 2025, aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole alirejea mchango alioutoa bungeni mwaka 2021 akipendekeza mifuko ya uwezeshaji wananchi isomane ili kuwasaidia wananchi kupata mitaji.

Alisema walishakubaliana kwenye chama na Waziri Mkuu alipewa maelekezo ya kushughulikia mfumo wa pamoja wa uwezeshaji.

“Leo unasema tutatendga Shj200 kwa uzoefu upi, kama yale mabilioni tayari yapo hatukuyapeleka kwa wananchi, leo kwenye kampeni ndiyo tunasema tutapeleka. Tulikuwa na miaka mitano, mambo hayaendi, ni lazima kumwaga oili,” alisema.

….Itaendelea
 
Back
Top Bottom