DOKEZO Ahadi ya serikali, ajira hewa za walimu wa economics

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

MC CU

New Member
Joined
May 16, 2016
Posts
2
Reaction score
1
Ndugu wasomaji na wanajukwaa naomba mfumo ufiche majina yangu niliyosajilia humu na hili jambo liende public tupate majibu ya serikali.

Tarehe 5 Juni 2025 serikali kupitia sekretarieti ya ajira ilitangaza nafasi za ajira nyingi katika kada mbalimbali, miongoni mwake zilikuwa nafasi 850 za walimu wa economics. Agost 13 waliitwa kwenye usaili wa mahojiano na maelekezo ikawa ni baada ya wiki mbili tangu tarehe hiyo wataanza kupangiwa vituo vya kazi.

Tangu pale kulikuwa na kimya kingi sana, mwezi Oktoba walipangiwa walimu 12 tu kati ya 850 na 838 kubaki bila kujua hatima yao.

Siku chache baada ya hapo katibu wa sekretarieti Mick Kiliba alitoa taarifa ya kuelekeza watendaji wake kupanga vituo kwa ajira ya mwaka wa fedha uliopita kabla ya November kuisha lakini halikutokea.

Baadaye waziri Ridhiwani Kikwete akatoa press kuelekeza kuanza kwa mchakato wa ajira 12000 na hizo ndio sauti ya kila kiongozi.

Ningependa tusaidieni mwenye kumfikia Kiliba atujulishe je, hizi 838 zilizobaki zitatoka lini? Au mpango wake umepitwa na wakati kwa hiyo tuondoe matumaini? Maana wale wa physics na biashara wameitwa interview tena kabla ya majibu ya Agosti.

Nimeuliza kuhusu Economics kwa sababu miaka mingi sasa sio somo la kipaumbele kwenye ajira za serikali. Sasa Katibu Mick Kiliba au Waziri Ridhiwani watupe mwelekeo wa hizo nafasi ili tujue mbivu na mbichi.

Bahati mbaya sana kupitia email ya sekretarieti, kupitia serikali mtandao nimelihoji mara nyingi na hawakuwahi kutoa response yoyote hata ya kuvunja moyo. Ahsante
 
Tutawaita hivi karibuni mambo fulani yalikua hayajakaa sawa kwanini hujatumia Account yako ya Zamani?
 
"Kwa wale ambao majina yao hayapo
katika tangazo hili watambue kuwa hawakupata nafasi/hawakufaulu usaili, hivyo wasisite kuomba kwa mara nyingine nafasi za kazi zitakapotangazwa"

Hiki kipengee hakikuepo kwenye hilo tangazo?
 
😀😀😀 Kwamba 12 tu ndio walifaulu. Halafu hizo 838 kwa nini hawajazitangaza tena ili watu waombe upya
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom